Jimmy George
JF-Expert Member
- Nov 28, 2016
- 1,733
- 1,648
Habari ndugu zangu katika JF.
Uzi huu hauna lengo la kuwasema vibaya single mothers nawaheshimu na kuwapenda. Lengo ni kujua changamoto zipi unaweza kukutana nazo ukiwa na uhusiano nao, hii itasaidia hata yule anataka kuanzisha uhusiano nao. Changamoto ambazo nimeona mimi ni ;
1. Kuwasiliana na mzazi mwenza
★hapa unakuta anawasiliana na mzazi mwenzake kuhusu mtoto mara atumiwe hela au aombe hela kwa ajili ya mtoto au wanasalimiana kujuliana hali tu. Wengine ni changamoto maana tuna wivu
2. Kukulinganisha wewe na mzazi mwenzake
★hapa anaweza akasema baba naniii alikuwa ananifanyia hivi,mara tukiwa wote tulikuwa tunafanya hivi na mengineyo,muda mwingine akitaka tu nawe ufanye baadhi kama yule wakati tuko tofauti binadamu.
3. Muda mwingine humjali mtoto zaidi kuliko wewe.
★Huweza asifanye baadhi ya mambo kwa ajili yako maana huwa busy na mtoto. Pia endapo ikitokea umemfokea mwanae kidogo tu mnaweza mkagombana.
Kama unazijua changamoto zingine ongezea tujadili.