TUPATIENI MREJESHO ZIARA ZA MAALIM SEIF

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Salaam wakuu.

Kwanza niseme nimekuwa mfuatiliaji wa siasa za Zanzibar na kwa kiasi zinanivutia.

Ni muda sasa wa kama miezi sita hivi tokea kurejewa kwa Uchaguzi wa Zanzibar uliogubikwa na malumbano kule visiwani. Uchaguzi huu uliitishwa baada ya Bw. Jecha mwenyekiti wa ZEC kufuta uchaguzi wa 2015 kwa njia zilizolalamikiwa na Wapinzani(CUF) na kuitwa BATILI.

Baada ya yote kufanyika na Dr Shein mshindi wa uchaguzi wa marejeo wa Machi,2016 kuunda serikali tuliona moto wa siasa kuanza upya.

Maalim Seif alianza kwa kufanya safari kisiwani Pemba(Ngome ya kuaminika ya CUF) na kulakiwa kishujaa kiasi cha jeshi la polisi kutishia kumshtaki maalim kwa Uchochezi.

Aliendelea kuzungumza na vyombo vya habari kwa tarehe tofauti na kuahidi kupigania kile alichokiita haki ya Wazanzibari na kuahidi kuwa haki yao itapatikana.

SAFARI YA KWANZA YA MAREKANI NA CANADA
Alisafiri na kupata mialiko mbali mbali alianza na Kituo cha Mikakati cha marekani (CSIS), alikwenda kuonana na msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa wa mambo ya kisiasa, alionana na uongozi wa Kituo cha kimataifa cha demkrasia kama sikosei (NDI) na kufika maeneo mengi nyeti. Aliporudi aliahidi kwamba Watawala aliowaita madhalimu watatoa haki na alitumia maneno "... wataitema tu...", "... tumewabana na ukuta..." .. siku zao zinahesabika....)
Aidha alipata kuzungumza na jumuiya za Wazanzibari/Tanzania na kueleza mafanikio kadhaa

SAFARI YA PILI. ULAYA,SCANDINAVIA NA MAREKANI
Hakuchukuwa muda baada ya kurudi alisafiri na kwenda Ulaya na Scandinavia na kwenda tena Marekani kwa mualiko wa Chama cha DEMOKRATIC cha marekani.

Akiwa Ulaya kulikuwa na taarifa za kufika ICC na kuwasilisha vielelezo vya kesi kwa wakili mashuhuri wa makampuni ya uwakili ya Uholanzi na iliarifiwa kufanikiwa sana safari hii ya pili.

Sasa ni kama wiki amerudi safari ndefu ya Ulaya na Marekani. Taarifa za chini chini hazithibitishiki na inakuwa ni uvumi tu(binafsi siziamini)

Tunaomba mrejesho wa safari hizo na tunataka kujuwa ahadi zile zimefikia wapi.

Wana mabadiliko wana hamu ya kujuwa nini hatma ya Zanzibar kwa ustawi wa demokrasia na kile kilichotokea baada ya uchaguzi wa Oktoba 2015.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom