Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,931
Baada ya wapinga maendeleo kuona kuwa wale tunaopenda maendeleo ya wananchi wa Tanzania tupo wengi humu jamvini, sasa wanatuita Pro CHADEMA. Nimeipenda hiyo. Mimi ni Pro CHADEMA kwa vile naipenda nchi yangu na napenda Watanzania wenzangu, napenda maendeleo na mabadiliko katika maisha yao.
Nimeanza hivyo kwa sababu tunaoitwa Pro CHADEMA humu jamvini tupo wengi ukilinganisha na wapinga maendeleo wa ccm. Hali hii vilevile inajirudia ukienda kwenye jamii zetu, ambako huko ndio maisha halisi yanatokea. Katika jamii wananchi wanataka mabadiliko, na wako wengi. Hii ina maana kimsingi, kutokana na maisha yao, nao wao pia ni Pro CHADEMA!
Kutokana na wingi wetu huu, kuna haja, hasa sasa hivi,kupambana na propaganda zinazoenezwa dhidi ya wapenda maendeleo. Wakati serikali ya ccm, ikishirikiana na vyombo vya dola inazidi kuikandamiza demokrasia, ni wajibu wa kila mmoja wetu, kwa nafasi aliyo nayo katika jamii kuwaelimisha watu wake juu ya propaganda hizi.
Kwa kutumia njia hii ni hakika kuwa tutashinda, kwa sababu sisi ndio wananchi, sisi ndio tunaolengwa na propaganda hizi, Hata hivyo ni sisi ndio tunaoishi maisha haya ya taabu ya kukosa chakula, ajira, afya, elimu, umeme, maji na mengineyo mengi. Wanaoeneza propaganda hizi wanataka hali hii ya shida kwetu iendelee, wakati wao wana umeme, wana maji, wana afya, wanashiba, wana umeme...wanaishi maisha mazuri.
Tuondoke sasa twende maofisini, mashuleni, mitaani, vijijini na mashambani tuendelee kuelimishana. Baba wa familia ana wajibu huo, mama, mjomba, babu na bibi. Haya tunayoyapigania ni maisha yetu na maisha ya vizazi vyetu vijavyo. ccm wanataka kuendelea kutunyang'anya maisha yetu! TUSIWAKUBALIE!