Tuongee kuhusu ufugaji wa wanyamapori

Masamila

JF-Expert Member
Jun 22, 2014
6,411
7,306
Hello members

Aisee kuna fursa pia ufugaji wa wanyama pori ila fursa hii ni mahsusi kwa wenye mitaji mikubwa (ujenzi wa miundombinu)

Mathalani kufuga viboko : kiboko wakati wa kumchinja kama amefikia ukubwa (adult) unapata zaidi ya tani moja ya nyama

Nilikuwa na tafiti nchi gani wanakula nyama pori jibu likawa ni China. yes ni Wachina, hawa kwao watu wa daraja la kati wanakula sana nyama pori na hilo limepelekea pia China kuwa na meli nyingi zinazovua samaki katika bahari ya kimataifa (Wachina wana meli zipatazo 2,600 zinavua bahari kuu ukidhani ni idadi ndogo hiyo basi USA wao hata hawana meli zikafika 260 zinazovua bahari ya kimataifa).

Kama mtu anachukulia poa nyama basi angejua kuna zipo nchi nyama ya ng'ombe kg moja bei ni zaidi ya TSH 30,000 KWA KILO!! yaani bei ni zaidi ya mara tano ya hapa nchini.

Wanyama wa kufuga nyamapori wapo aina nyingi mno , na ningechambua hapa mmoja mmoja kila mmoja kuna njia ya kumfuga na mfugaji akapata faida sana.

Njia ya kuzalisha chakula kwa ajili ga ufugaji huo ni kwa kulima nyasi (ziko nyasi aina nyingi sana kutosha kutoa mlo kamili wa mifugo inayokula nyasi na ziada)

Ningepiga thread ndefu bahati mbaya niko natumia simu kuandika huu uzi.

Ataeshindwa ubunifu wa kuandaa miundombinu ya kuwaweka hao wanyama pori anaweza kunitafuta (niko vizuri kwenye ubunifu)
 
Kwa Tanzania inaruhusiwa ukifata Taratibu.Kuna bucha dodoma ilifunguliwa mwezi uliopita kwaajili ya kuuza nyama ya wanzama poli
 
Kuna jamaa alifuga nyoka kule bagamoyo akitegemea kuja kuuza venom, walimwambia soko ni uhakika na atavuna pakee ya kutosha!

Sasa Nyoka wakanawili vizuri na kutema venom ya kutosha, balaa likaja kwenye "mteja"!!! Mteja hayupo! Hakuna Mnunuzi! Jamaa akaleta Uzi hapa JF akiomba namna ya kuiua hiyo Mijoka!

NB: Sina lengo la kuharibu Uzi wako,ni ktk kukumbushana tu!

Tuendelee Kujifukiza.
 
Kwa Tanzania inaruhusiwa ukifata Taratibu.Kuna bucha dodoma ilifunguliwa mwezi uliopita kwaajili ya kuuza nyama ya wanzama Poli.
 
Mathalani kufuga viboko : kiboko wakati wa kumchinja kama amefikia ukubwa (adult) unapata zaidi ya tani moja ya nyama
mkuu viboko huwa vinahusihswa na ushirikikina yaani ni kama kufuga nyoka ama fisi. kwa hiyo kijijini unaweza kufukuzwa ama kuchomwa moto.

Kuna mzee aliwafugaga wengi sana, alipokufa walimfuata wakaenda kufukua kaburi lake - yaani hawakubali kwamba boss wako kafa.

Kwa wanyama fuga sungura ama kmoto.
 
mkuu viboko huwa vinahusihswa na ushirikikina yaani ni kama kufuga nyoka ama fisi. kwa hiyo kijijini unaweza kufukuzwa ama kuchomwa moto.

Kuna mzee aliwafugaga wengi sana, alipokufa walimfuata wakaenda kufukua kaburi lake - yaani hawakubali kwamba boss wako kafa.

Kwa wanyama fuga sungura ama kmoto.
Duuuuh kwahio viboko wakaenda kufukua kaburi?aiseee
 
Back
Top Bottom