Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,072
- 19,210
Kuna huu mmea unaitwa Agave. Upo kama katani.
Unapandwa. Baada ya kama miaka 7 hukomaa na kuvunwa. Ukikomaa huwa kama nanasi hivi. Huvunwa. Majani hukatwa na kiini kama nanasi huchukuliwa.
Kiini hicho huchukuliwa na kuchomwa kwenye moto.
Baada ya kuchomwa hukamuliwa kutoa juisi. Juisi hiyo yenye sukari huchachushwa kutengeneza pombe. Pombe hiyo hufanyiwa distillation kutengeneza gongo inayoitwa Mezcal.
Tequila ni Mezcal inayozalishwa kwenye mji wa Tequila huko Jalisco, Mexico.
Brands Maarufu ni Jose Cuervo na Don Julio. Jose Cuervo ndiyo inaongoza kwa mauzo. Huyo jamaa Jose Cuervo(miaka ya 1800 huko) alioa mjane aliyekuwa na mashamba na distilleries za Tequila. Alipambana sana hadi brand yake kuja kuwa ndiyo kubwa.