choupa moting
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 1,508
- 2,577
Habarin za mchana waungwana, poleni na majukumu ya kujenga taifa letu pendwa la Tanzania.
Niende kwenye mada husiku, nimekua mtumiaji wa mwendokasi mara nyingi ninapoenda kwenye mizunguko yangu. Kuna vitu haviko sawa na sijui kwanini havifanyiwi kazi na mamlaka husika inayotoa huduma hii. Sisi kama wananchi na wanufaika wa hizi huduma lazma tusema ukweli maana hatupandi bure, tunalipa pesa hivyo huduma mnazotupatia lazma ziendane na mnachochukua kwetu. Kuna hizi kero ambazo mara nying nakumbana nazo na abiria wanapiga kelele kila siku ila hamna dalili ya kutatuliwa.
1. Magari kupita vituoni yakiwa tupu wakati abiria wapo wanasubiri. Hii imekua kero ya muda mrefu sijui tatizo ni nini. Inawezekana vp magari yanazunguka tu na abiria wapo vituoni hawachukuliwi. Na kwanini kama kuna tatzo kuhusu hili msitoe tamko. Nadhan namna nzur ya kuoandoa dukuduku kama hizi ni kuwasiliana na abiria kuwaeleza mustakabal wa mambo ila sio kama mfanyavyo.
2. Vituo vya mwendo kasi kutokua na sehem za kukaa abiria. Logic ya mwendo kasi mwanzo ilikua ni kufika na kupanda kwenye gari kias ambacho hakuna haja ya kuwa na siti au sehem za kukaa wakat wa kusubir gari, lakn kwa sasa watu wanasubiri vituoni mpaka lisaa limoja au zaidi. Hivi mnategemea abiria awe amesimama muda wote huo? Laki pia kuna wagonja ambao kwao afya inawanyima uhuru wa kusimama muda mrefu. Ina maana hamulioni hilo kweli?
3. Magari kujaza abiria kupita kiasi. Hii ni mbaya sana hata kiafya, kumbukeni kwenye mchanganyiko wa watu wengi vile kuna wagonjwa ambao kwa namna moja au nyingne wanaweza kuambukiza wengine. Magonjwa kama TB na mengine yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya hewa ni hatar kwenye mikusanyiko kama hii. Kwanini muwe kisababishi cha maambukizi ya magonjwa?
Kwa namna hizi kero zilivyo za muda mrefu na hakuna mabadiliko ya aina yoyote tuongee tu kiume kwamba MWENDOKASI WAMEFELI.