TUONGEE KIUME: Mambo 5 ya kuzingatia kabla hujaingia baa

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,640
Inawezekana zaidi ya nusu ya wanaume wote duniani wanaokunywa pombe wanafurahia zaidi kunywea baa. Hivyo huenda ni muhimu pia kufahamu mambo ya kuzingatia kabla hujaanza safari ya kwenda huko ili usijutie pesa na muda wako. Anza kwa kuzingatia haya matano.

1.SABABU YA KWENDA BAA
Kila mtu huingia huko akiwa na sababu tofauti na mwenzake. Wapo wanaokwenda kupunguza msongo wa mawazo, wanaokwenda kujipumzisha baada ya mizunguko ya siku, wanaokwenda kupata fursa mpya za kibiashara, wanaokwenda kusubiri foleni ipungue na ambao wao ni ratiba yao ya kawaida ya kila siku.
Kwa hiyo kabla hujaanza safari jiulize kwa nini nakwenda baa, kisha fanya tathmini ya baa unayotaka kwenda kama inaweza kuwa sehemu nzuri ya kufuata unachokitafuta vinginevyo utajuta.

2.DARAJA LA BAA
Siyo kwa sababu wewe ni mlevi basi unatosha vigezo kuingia kwenye kila baa, utafeli. Ifahamu baa unayoingia ni ya daraja gani? La juu, la chini au la kati, kisha jitathmini na wewe ni mlevi wa daraja gani.
Kuna baa zinauza bia moja Sh15,000, ukiingia hizo wakati wewe ni wa bia za Sh2,500 unaweza kuagiza, ukanywa kama komba, halafu ukaletewa bili ya ajabu usiamini. Usipokuwa makini unaweza kupewa kazi ya kupanga makreti stoo.

3.UMBALI WA BAA HADI NYUMBANI.
Kiuhalisia hakuna mlevi aliyewahi kulewa hata akapasahau nyumbani kwake. Iwe isiwe, walevi wote hufika nyumbani hata baa iwe mbali kiasi gani. Yaani hata mtu anywe hadi azimie, atafika nyumbani hata kwa kubebwa. Kufika ni kufika.
Ila ni vyema zaidi kunywa karibu na nyumbani kwa sababu kadri baa inavyokuwa mbali na nyumbani ndivyo ambavyo mlevi hufika nyumbani na hali mbaya.
Ulishawahi kusikia mtu karudi nyumbani hana chochote, hata nguo. Hayo ni miongoni mwa madhara ya kulewea mbali na nyumbani.
Watu wanagawana kila ulichokuwa nacho huko huko njiani.

4.POMBE ZITAKUGEUZA KUWA NANI?
Kila mtu anabadilishwa na pombe kuwa mtu fulani. Kuna wengine wakilewa wanakuwa wanamuziki, wataimbaa weeee mpaka mwisho. Wengine huwa waandishi wa habari, wengine huwa ‘usalama wa taifa’ na zaidi.
Wewe ukilewa unakuwa nani? Hili ni swali muhimu kujiuliza kabla hujaingia baa kwa sababu kwa mfano yawezekana ukilewa unakuwa Mike Tyson, unajisikia kupigana tu na kila mtu. Hii ni bora uende baa zenye ma bodyguard ili hata ukianzisha ugomvi, utatolewa nje na kama kupigwa utapigwa kistaarabu. Ila ukienda kwenye baa za kawaida, ukaanzisha ugomvi, hakutakuwa na kuamulia utapigwa mpaka watu wahakikishe wamekuchomoa meno yote ya barazani. Litafakari hili.

5.WANAO WATAKULA KESHO.
Kama unaishi kwa kuamini kesho itajisumbukia hata usifikirie hili swali. Nenda katumbue fedha yote. Ila kama unafahamu kuwa wewe ndiyo nahodha wa familia yako ni muhimu kujiuliza ukiingia leo baa, utatoka na pesa ya kuwanunulia wanao chakula. Liweke kichwani hili.

Credit: Kelvin Kagambo
 
🙌🙌🙌🙌🙌 nakazia kabisa haya ni maswala ya muhimu sana
 
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
 
Mbona stresss?
 
Hivi kila mada ni lazima uchangie! Napita zangu mdogomdogo

Bazazi
 
Presha ya nini wakati ajali kazini
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
 
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
Mbona kama umepaniki aseeeee?
 
Swali moja tuu najiukiza
Je Nitalewa? Kama jibu ndiyo hayo maswali mengine nayapotezea kwani mimi huenda Bar Kulewa!
 
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
Wahuni wanaeza mmwagia mumeo mayai kisha wanakuletea na machela walahi lazima ufe kwa Presha!
 
Plan B, usipendelee kuwa bar bila mtu/watu wako wa karibu kuna kuzima
Arusha kuna machalii 2anavizia ukizima wanajifanya ndugu zako wanaenda kukulawiti! Na suala hili limeongeza ushoga Arusha... Kuna chalii anaitwa papii wa sekei anatajwa sana kuhusika na ulaji na utengenezaji mashoga.
 
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
Kuna watu wengine tunalewa Sinza tunakaa Bunju tunaenda baa saa 2 usiku tunakunywa hadi saa nane..tunawasha gari na tunafika salama tunapokwenda..hatutapiki, hatuyumbi, hatujikojolei, kimsingi huwezi kuona umuhimu wa kitu usichokifanya..sio swala la kushukuru kwamba wewe hunywi pombe wala mr wako hanywi pombe...kunywa pombe ni swala la starehe kama ilivyo starehe ingine..
 
Cha kwanza nakunywa ndio furaha yangu si angalii gharama cha pili na angalia mziki kuna bar moja kama ukienda unaenda mgeninani mbagala kuu nime isahau jina wana piga live copy za mamtoni hadi raha
 
Kuna watu wengine tunalewa Sinza tunakaa Bunju tunaenda baa saa 2 usiku tunakunywa hadi saa nane..tunawasha gari na tunafika salama tunapokwenda..hatutapiki, hatuyumbi, hatujikojolei, kimsingi huwezi kuona umuhimu wa kitu usichokifanya..sio swala la kushukuru kwamba wewe hunywi pombe wala mr wako hanywi pombe...kunywa pombe ni swala la starehe kama ilivyo starehe ingine..
Pombe iheshimiwe nakuunga mkono mkuu kama hajielewi itakua hivyo tu hata asipokuwa vibe
 
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
wanaofanya hayo mabaya uliyoyasema ni wale walevi wa mataptap. kama ni umaskini wapo maskini wengi tu hawanywi na wapo matajiri wengi tu wanakunywa.
 
Usioni umuhimu wa pombe.
Namshukuru Mungu Mr nae hatumii pombe.
Ukinywa pombe ukilewa unajidharirisha
Pombe inaongeza umasikin ktk familia.

Kuishi bila kunywa pombe inawezekana,

Swali? Kwa wanawake
Hv mwanamke mwenzangu unajisikiaje mumeo anarud kalewa njwiiii, na au kajikojolea na kero nyingine nyingi za ulevi au anasukumwa kwenye mkokoten wanamleta nyumban hajitambui c unaweza ukafa kwa presha jaman.
Mbona Mimi nakunywa na sio maskini?
 
Back
Top Bottom