Tuongee kisomi: Kijana mwenye diploma na shahada inakuwaje unajitolea kwenye Taasisi miaka 5 na ziadi? Ni kwamba huna plan B kabisa?

Paploman

JF-Expert Member
Apr 13, 2019
1,720
3,237
Habari zenu wanazengo?

Leo naongea na hawa vjana wenzangu wanaojiita wasomi, hawa wenye diploma na degree hivi huwa wanaelewa umuhimu wa muda na umri?

Najua familia nyingi walizotoka ni za hali ya chini sana, na suala la ajira hapa nchini lishakuwa gumu ni kuomba
mungu kama mambo yatakuja kubadilika baadae. nikachonishangaza ni kwamba hawa vijana wameshindwa hata kutumia hayo maarifa madogo kujikwamua.

Just imagine, mtu anamaliza chuo ana miaka 23 - 25 anaanza kujitolea taasisi X bila malipo anatumia nauli yake, chai then mchana anapiga deshi, nauli ya kurudi nyumbani huyu anamaliza mwaka wa kwanza, wa pili ....mpaka wa sita yupo tu anajitolea akiwa na matumaini siku moja ataajiriwa kibaya zaidi yuko taasisi ya umma ambapo kwa leo ajira zote zinapitia psrs hapa utakuta anarundikiwa kazi nyingi za waajiriwa zinazoingizia taasisi mamilioni ya pesa huku yeye akiambulia patupu na matumaini ya kupata ajira taasisi husika hayapo maana lazima zitangazwe na utumishi na akashindanishwe.

Nina marafiki zangu wawili wako pale TEMESA wanajitolea mwaka unaenda wa 5 sasa ni mae - enginer wazuri na ni watu waliokuwa na uwezo mkubwa darasani, na kabla ya TEMESA walikuwa taasisi nyingine wanajitolea umri wao sasa unaelekea 34, hawa watu nimeshawashauri sana ni bora waangalie namna ya nyingine ya maisha kukimbizana na umri na kama ni ajira zikitangazwa wakutane psrs, bado wamenogewa na 200k ya lunch wanayopewa na TEMESA kila mwezi na 100k ya nauli but kwa umri kama huo ni vema kuishi maisha hayo? kibaya zaidi wanafanya kazi zinazoingizia temesa mabillion ya pesa na TEMESA wana shortage ya watumishi hivyo wanawategemea hawa wa kujitolea ili wafanye kazi zao .. na wapo wengi kweli. HUKU NI KUKOSA MAARIFA KWA WASOMI?

Mwingine ni mechanical Engineer mzuri tu huyu yeye naye umri ushamtupa mkono mwaka wa4 huu yuko pale bandarini kama kibarua wa SUMA JKT akiwa nafanya kazi za Suma mle bandarini analipwa 10k kwa siku ale humo, nauli na matumizi mengine na unalipwa unapoingia kazini.... na bado sioni kama ana mpango hata kufikiria nje ya box na umri unaenda.

Hapa kazini wapo vijana wengine tushawafanya kama sehemu ya wafanyakazi wanafanya kazi kwelikweli, lakini management inawachakulia kama ni watu wa kujitolea tu pamoja na kufanya kazi lakini hamna maslahi yoyote wanayopata ...., mpaka wengine wanakuwa na umri ambao unaona kabisa inatakiwa angalau wawe na maisha yao na ukimuangalia yeye bado anadhani kujitlea ndio sifa kuu ya kumpatia kazi baadae.

VIJANA KUNA SEHEMU TUNAKWAMA

Ni ukweli serikali imeshindwa kukabiliana na changamoto za ajira kwa vijana, na kwa serikali na aina ya viongozi wa kiafrica kuendelea kupiga kelekele bila kuchukua hatua za kujikomboa mwenyewe ni sawa na machozi ya samaki, mtalalamika kila siku na hamna cha kuifanya serikali ....AMKENI

Mimi sio muumini wa kujitolea hasa bila malipo kwa mda mrefu tena kwa mtu aliyesoma... haya ni matumizi mabaya ya akili, upotevu wa mda na kuzikimbia fursa kwa matarjio yaliyo na matokeo chanya ya asilimia chache kufanikiwa, kwa sababu wengi wa wanaojitolewa lengo lao ni kupata ajira na leo ajira nyingi zinapitia sekretariati ya ajira huko wanaangalia uwezo na hawaangalii ulijitolea wapi na taasisi unayojitolea itakuwa haina nafasi kukufanya upate kazi serikalini.... sasa kwa nini upoteze mda kujitolea bila malipo huku ukitumia pesa zako kwa ajili ya nauli kwenda kufanya kazi sizizo na malipo ?

Ulisoma ili ujitolee? mimi nadhani miezi sita au mwaka mmoja ni mda unaotosha kabisa kujitolea zaidi ya hapo ni matumizi mabaya ya mda, vijana anzeni na endelezeni ndoto za maisha yenu taratibu taratibu najua changamoto ni nyingi lakini ni bora kuliko kujitolea, bila hivi mtakufa na stress umri unapowatupa mkono na kujikuta mambo yenu hayaendi.

nawasilisha kwa ushauri tu
 
Hakuna kitu kigumu kama kukubali Ukweli vijana wanaangamia kwa kukosa ujasiri mtu anaogopa akiacha kujitolea itakuaje? kalmakenge hawa graduates wa sasa ni tegemezi kupitiliza wanashindwa maisha ya mtaani na wasio soma. Aibu tupu.....Elimu inatoa ujinga ila usipokuwa makini inazidisha ujinga. bila kujitoa akili she
 
10000k kwa siku mkuu. basi huyo atakuwa billionaire. labda km umekosea figure @[/QUOTE]
 
Hakuna kitu kigumu kama kukubali Ukweli vijana wanaangamia kwa kukosa ujasiri mtu anaogopa akiacha kujitolea itakuaje? kalmakenge hawa graduates wa sasa ni tegemezi kupitiliza wanashindwa maisha ya mtaani na wasio soma. Aibu tupu.....Elimu inatoa ujinga ila usipokuwa makini inazidisha ujinga. bila kujitoa akili she
Sasa swali la kujiuliza anaogopaje kuacha kazi ya kujitolea wakati halipwi sanasana anatumia pesa yake mfukoni ya nauli na matumizi mengineyo
 
Ni rahisi sana kusema hivi hasa ikiwa ulitafutiwa kazi na mme wa dada yako.

Nyinyi mliosoma enzi za Nyerere ndiyo mliosababisha taifa hili kuendelea kuwa maskini kwa sababu vichwani mwenu mliondoa ujinga bila kupata maarifa.

Nalog out
 
Mleta mada inaonekana wewe ulisoma enzi za wakina kawawa! Kujitolea ni sehemu ya kupata uzoef, ujuzi pamoja na connection, tatizo lako unataka kuona graduate anaenda kuuza karanga na chapati wakati kasomea vitu vingine huko chuo pia ujasiriamali sio option ya kitoto kama unavyofikiria.

Mahali nilipofanyia field ndipo nilipopata connection ya kupewa nafasi ya kujitolea ( nilifanya miezi yangu 3 tu mpaka hapo nikawa nishajenga connection niliyokuwa naitaka mimi then nikaaga kwa wema kabisa kuwa naenda kusoma japo haikuwa kweli.

Baada ya miezi 6 niliitwa hapo hapo na boss mmoja wa kwenye shirika hilo na kupatiwa full time employment.
 
Back
Top Bottom