Tuongee asubuhi [Star tv] tarehe 9/9/2011: Wabunge na mchango wao katika maendeleo ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuongee asubuhi [Star tv] tarehe 9/9/2011: Wabunge na mchango wao katika maendeleo ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BENITOO, Sep 8, 2011.

 1. B

  BENITOO Member

  #1
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado wananchi wengi hasa vijijini hawaoni lolote linalofanywa na watu waliowapa dhamana ya kidemokrasia ya kuwaletea maendeleo..na wanadai zipo sababu nyingi zinazosababishwa na hali hii..je,wewe mbunge wako kafanya nini??shiriki katika kipindi hiki kuanzia sasa...HOST Mwanza,B ernard James..wageni Dokta charles Kitima makamu mkuu wa chuo SAUT na Bwana Donald Kasongi..toka ACCORD...Dar host ni Tom Chilala..wageni bado ila atakuwepo mbunge na mdau wa maendeleo..saa 1.30 asubuhi LIVE
   
 2. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Join Date : 7th September 2011
  Posts : 1

  Rep Power : 0
  Karibu sana hapa jamvini.
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bila hodi jamvini? Tumekupokea na ujumbe umefika
   
 4. Rutunga M

  Rutunga M JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2009
  Messages: 1,556
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kipindi cha tuongee asubuhi startv ni kizuri sana na nathubutu kusema ni kipindi bora cha asubuhi across all local tv stations.

  Tatizo lenu ni moja tu; baadhi ya watangazaji/waandaaji wa vipindi wanaweka mbele ushabiki wa kisiasa kuliko taaluma.

  Mna tabia ya kuwaachia sana viongozi/makada na wabunge wa magamba kujieleza kwa kireeeefu sana bila kuwarudisha kwenye hoja za msingi.

  Kwa mfano Tom Chilala, Ivona Kamuntu, Christina Mbezi, Paul Mabuga na James Range hawaulizi maswali magumu wageni wake hasa wanapokuwa viongozi na wabunge wa magamba ama serikali. Wakiwa na wageni toka vyama vya upinzani ama asasi zisizo za kiserikali ndipo utawaona wanajitutumua kidogo.

  Mtu ninayemuaminia kwa kuendesha kipindi ni Dotto Bulendu, jamaa yuko poa sana kwa uchambuzi na kuuliza maswali wageni wake. Pia Yahya MNohamed naye hujitahidi sana kuendesha kipindi vizuri. Mkijitahidi kuwa kama hawa waungwana kipindi kitakuwa juu sana kuliko ilivyo sasa.

  Nawasilisha.
   
 6. P

  Ptz JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 466
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Topic hii imenifurahisha sana. Binafsi mbunge wangu kwa kipindi hiki bado sijaona mchango wake katika maendeleo ya nchi yetu hususani jimbo ninaloishi la Sumbawanga mjini. Serikali kwa kupitia watendaji wake imekuwa ikionesha kuwa uchumi wa nchi yetu umepanda kwa kasi kwa asilimia 7, kwa kutoa hoja kuwa kuwepo kwa huduma bora za jamii ndiyo kigezo kikubwa. lakini chakusikitisha wananchi wengi bado ni masikini na wanaendelea kuwa masikini. Katika bunge hili la 10 na kwa mikitano yote miinne mbunge ameongea mara moja kwa kuchangia kwa kuongea, katika mahojiano yaliyofanywa na mtangazaji wa sumbawanga television ndugu Kisika yeye mbunge anajisifu kuwa kuongea si hoja kwani wabunge wengi wanaoongea ongea wanaropoka ropoka tu hawana lolote yeye anamtandao mkubwa kaujenga kwa mawaziri na anajivuna kuwa katekeleza ilani ya chama cha kwa kiasi kikubwa. Akiendelea kuhojiwa na mtangazaji aliongezea alikiri wazi kuwa amekua akitumwa mara kwa mara na chama chake, mfano alieleza kuwa wakati wa kipindi cha bajeti alitumwa na chama Igunga kwa ajili ya kungalia mambo ya kisiasa kwa muda wa majuma mawili. Ninachokiona kutoka kwa mbunge huyu ni kujikita sana na shughuli zake binafsi, chama chake na kutoa vijisenti vidogo vidogo kwa rafiki zake wale waliojiweka wazi wakati wa kampeni kuwa wako upande uwake na kwa kupitia umasikini na ujinga wetu sisi wananchi wa Sumbawanga baadhi yetu na hasa wnaopewa vijisenti anaonekana anafaa sana. Mfano anaweza akakutana na hao watu wake akawapatia hata alfu moja tu kwa ajili ya pombe tena ya kienyeji lakini cha kushangaza huyo mtu ana familia kaiacha nyumbani hawana cha kula wala mavazi, watoto wakiugua hata marelia hufariki kwa kukosa dawa mseto. Katika jimbo l a Sumbawanga mjini kuna wananchi zaidi ya asimilia 60 wanaishi chini ya poverty line la kushangaza zaidi hawa ndiyo wapiga kura wenye mamlaka ya kuwaweka wanasiasa akiwepo mbunge madarakani, nimeshuhudia watoto wengi wakikosa karo, na kuacha shule kwa kukosa huduma za msingi wakati mbunge anasimamia maslahi yake binafsi na ya chama chake. Mimi ninashi katika moja kati ya kata mbovu kimiundo mbinu utadhani haiko mjini. Kata hii inaitwa Malangali, kipindi cha masika huwa ni kero kubwa kwa vyombo vya usafiri na hata kwa watembea kwa miguu, kuna suala pia la maji ni shida sana hali kuna chanzo kikubwa cha maji karibu na kata hii, lakini sijaona jitihada zilizofanywa mbunge katika hili. Hii ni shida sana na ni kero kubwa kwa wanasumbawanga hususani wana Malangali. kata hii ya Malangali ina shule ya sekondari moja lakini ina walimu wachahe sana, haina maabara kwa ufupi miundo mbinu yake ni tatizo, kata haina huduma ya kiafya mfano zahanati. Wapo wananchi wakulima katika kata hii lakini la kusikitisha pembejeo zinazotolewa na serikali zinaishia mikononi mwa wajanja. Vijana zaidi asilimia 90 hawana ajira rasmi, wengI wao hao vijana pamoja na kujiunga katika vikundi vidogo vidogo hawakopesheki kwa sababu ya urasimu wa watendaji wa serikali, mfano kati ya vijana 236 wa kata ya malangali walioomba mkopo kupitia mabilioni ya JK hakuna hata mmoja aliyebahatika. JE, HUKU NDIYO KUPANDA KWA UCHUMI? MBUNGE HILI HALIONI, BUNGENI HALIPELEKI NA HALIJUI, ANAJUA TU MASLAHI YAKE, NA YA CHAMA CHAKE. BADO SIJAOONA MCHANGO WA MBUNGE WANGU KATIKA MAENDELEO YA NCHI.
   
 7. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mliwaondoa wafanyakzi wenu na kuwaachisha kazi mpaka leo hamjawalipa pesa zao huu mwaka wa tatu ushahidi tunao tokea mwaka 2008 mpaka hv leo mnawazungusha tu. Star tv imeoza kwenye suala la uongozi, ngono ndio imetawala tu. Hakuna kipindi kibovu kama hicho cha tuongee asubuhi kwani ni cha kukurupuka tu. Mnajisifia nje wakati ndani kuna oza.
   
 8. B

  BENITOO Member

  #8
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wadau?kipindi hiki baada ya kuahirishwa kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu sasa kitakuwa hapo kesho tarehe..16/9/2011 asubuhi saa 1.30 LIVE STAR TV..TUNAOMBENI MAONI YENU,KABLA NA WAKATI WA KIPINDI
   
Loading...