Tuondoe kwanza umasikini kabla ya ujinga na maradhi

Tuondoe kwanza umasikini kabla ya ujinga na maradhi

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
678
Na Elius Ndabila

0768239284


Baada ya hatua ya kwanza kukamilika ya kuhakikisha bara la Afrika linakombolewa kutoka kwenye minyororo ya ukoloni, hatua iliyofuata ni kujenga uchumi imara.Vita hii iliongozwa na Wafalume wa Afrika ambao baadhi ni Hayati Nyerere, Mandela, Nkuruma, Neto, Mugabe, Leopard, Toure nk. Historia inatukumbusha kuwa karibia nchi nyingi za Afrika kabla ya miakaa ya 1960 zilikuwa chini ya makoloni yao ambayo ni matokeo ya mapinduzi ya viwanda huko Ulaya isipokuwa Ethiopia na Liberia ambazo hazikutawaliwa.

Adhima kubwa ya viongozi walioongoza vita ya kumuondoa mkoloni ilikuwa ni kufanya mataifa ya Afrika kuwa huru, lakini uhuru wenye mipaka. Baada ya hapo ilikuwa kuanza kujenga uchumi imara katika mataifa yao na falsafa ya kujenga uchumi ilitegemea kati ya nchi na nchi. Kwa mfano bada ya uhuru wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere aliamini bada ya uhuru ni kuwa na Taifa la ujamaa na kujitegemea. Aliamini kuwa Taifa linalojitegemea ni lazima kuwe na uchumi imara na uchumi imara ungesaidia kuondoa Ujinga, Umaskini na Maradhi.

Mwalimu Nyerere aliamini fika ili taifa liitwe taifa imara na linalojitoshel eza lazima lipambane na ujinga, umasikini na maradhi. Lakini hadi Mwalimu anafariki mwaka 1999 bado kulikuwa na umaskini, ujinga na maradhi pamoja na taifa kuwa na rasilimali nyingi. Kwa siku za hivi karibuni pia ameingia mdudu rushwa ijapo mimi ninaamini kuwa huwezi kutenganisha rushwa na umaskini. Umaskini ndilo daraja la rushwa. Ukiondoa umaskini unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hii rushwa. Wakati wa joto tunashauriwa kuva nguo nyeupe kwa kuwa zinaakisi mwanga, ukivaa nyeusi hii inatabia ya kusharabu joto unaweza kuathirika. Ndivyo ilivyo kwa Umaskini na Rushwa.

Kwa mtazamo wangu ninadhani Umaskini ndilo tatizo kubwa. Ninamini ukishaondoa umaskini ni rahisi kufuta ujinga, kufuta maradhi na kufuta rushwa. Umaskini ndio mzizi wa matatizo yote. Unaweza kumuondolea mtu ujinga lakini ukashindwa kumuondolea umaskini na akawa corrupt person. Hatujaona watu wamesoma na kuwa na PHD lakini ni corrupt? Tunamini mtu anapokuwa ameenda shule basi anakuwa ameondoa ujinga, lakini kuondoa ujinga kunasaidia nini katika maisha ya kila siku ya mwanadamu kama kama bado ni masikini? Ninajaribu kuandika haya ili kukuchochea fikira na mtazamo mpya.

Nguvu ya umasikini ndiyo inayoweza kuamua aina ya kiongozi na si nguvu ya ujinga au maradhi.Watu wenye uchumi imara wanauwezo wa kumununua hata mtu aliyesoma ila maskini. Kitu kinachomfanya mtu aishi si kutokuwa mjinga bali kuwa na uchumi imara. Ili tuweze kupata viongozi bora kwenye jamii zetu ni lazima tuanze kwanza na suala la kuwakomboa kiuchumi kabla hatujapambana na ujinga na maradhi. Unaweza usikubaliane na hili kwa haraka lakini ukipata muda wa kufikiria utapata majibu.

Mathalani mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi. Madiwani na wabunge wengi wanajua hali halisi za wapiga kura wao. Kitendo cha viongozi kuwajua wapiga kura wao kinawafanya hawa viongozi wasiwajibike sana kwenye katazao au wilaya zao kwani wanajua muda wa uchaguzi ukifika ni rahisi kuwanunua wapiga kura. Mbunge anajua watu wangu ni maskini na shida yao ni fedha, basi atahakikisha kuanzia mwezi huu hadi October harusi zote, misiba yote, wagonjwa wote wanaompigia simu, matamasha yote n.k anatuma michango.

Akili hii wanaitumia sana wabunge ambao baada ya uchaguzi huwa hawarudi tena kwenye maeneo yao ya kazi. Wao wakichaguliwa basi utawaona tena kipindi kama hiki tu.Na kwa kuwa watu wako hovyo kiuchumi si rahisi kupima madhara ya kesho wao wanapima faida ya leo tu. Watu sasa hawafanyi siasa kama sehemu ya kwenda kupigania maendeleo ya maeneo yao, wengi sasa wanafanya siasa kama sehemu ya ujasiriamali. Watu wanatumia nguvu kubwa ya fedha kupata uongozi kwa kuwa anajua huko kuna mirija anwai.

Ni wakati sasa wa Serikali kuangalia mazingira ya kumsaidia mwananchi wa chini kujikomboa kiuchumi, ili unapofika wakati wa chaguzi asishurutishwe na fedha za wagombea bali aongozwe na akili yake. Kumsaidia mwananchi wa kawaida kujikomboa kiuchumi kutamfanya kuwa jasiri kuepukana na mapenzi ya dhati yanayoanza vipindi vya chaguzi na watia nia. Na si hilo tu, bali kuwawewesha watu kiuchumi kutapunguza wale watu wa katikati yani middle men ambao ni majasusi wa kisiasa.

Majasusi wa kisiasa ni wale wanaojua kucheza na watia nia. Jasusi anaweza kuwa na wagombea hata watano na wasijuane na kote akawa anapiga pesa. Kazi ya jasusi ni kuwachonganisha watia nia wote wachukiane na wasiwasiliane. Mana asipowagombanisha hazi kula kwani hawa wanaishi kwa sababu ya migogoro. Na wanasiasa wengii wanapenda kupongeza hata akikosea, hivyo majasusi haya mambo wanayajua na wanakuwa na timing.

Ninadhani ni muda mwafaka wa serikai kuandaa watafiti ili waje na njia ambazo mwananchi wa chini atashiriki moja kwa moja kula mkate wanchi kuliko sasa ambapo tabaka kubwa bado linaishi kwenye umaskini pamoja na kuwa ni wazalishaji wakubwa wa pato la taifa. Kuna tabaka kubwa kati ya masikini na matajiri. Tukiendelea kupambana na Ujinga, Umaskini na Mradhi tunaweza maliza miaka 1000 na vita hii isiishe. Njoo tuanze kwanza na vita ya Umasikini, mtu akishaondokana na umasikini ni rahisi kuondokana na UJINGA NA MARADHI. Huwezi kuondokana na Ujinga na Maradhi kama bado ni masikini.
 
Serikali ya jiwe inapenda wanyonge na masikini waongezeke wamwimbie mapambio.
 
Huwezi tenganisha umaskini na ujinga.
Maskini ni mjinga hajui Afanye Nini aondokane na umaskini.Yupo yupo tu
 
Umasikini na Maradhi Kwa Kiasi Kikubwa Ni Matokeo Ya UJINGA.Nadhani tutilie mkazo kutokomeza UJINGA.Tupeane Elimu yenye tija kulingana na Mahitaji.UMASIKINI NA MARADHI vitajiengua vyenyewe automatically.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga na umasikini ni mtaji wa wanasiasa kuviondoa ni kutoitakia mema ccm,ujinga ukiondoka na ccm itaondoka
 
Umasikini na ujinga uzalisha watu wanyonge ( futureless people ) wasiowezanunua hata ndala hawa ni mtaji mkubwa sana kwa wanasiasa ukiwa na millions 2 unaweza wanunua wote kwa kuwapa kilo moja moja ya sukari wao wakakupa kura
 
Huwezi kuondoa umasikini kabla ya kuondoa ujinga, kwasababu ujinga tuu wenyewe ndio chanzo cha umasikini.
P
 
Hakuna nchi ingependa kuona masikini na wajinga wanapungua. Maana huo ndio mtaji wao mkubwa.

Ili ukomboke na ujinga lazima uwe mtu wa kufikiria nje ya box

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom