Tuombee uchaguzi mdogo IGUNGA

Aug 20, 2012
7
1
Hakuna asiyejua nini kilitokea huko Igunga kwani pamoja na vurugu nyingine nyingi za hatari,kada wa chama kinachokuja kwa kasi katika siasa za Tanzania aliuwawa.

Pamoja nafuraha ya wapenda haki tusiache kuombea uchaguzi huo kwa imani zetu, hatutaki kuona damu inamwagika tena.Asanteni
 
Hakune asiyejua nn kilitoke huko Igunga kwani pamoja na vurugu zingine nyingi za hatari,kada wa chama kinachokuja kwa kasi ktk siasa za TZ ALIUWAWA, pamoja nafuraha ya wapenda haki tusiache kuombea uchaguzi huo kwa imani zetu.hatutaki kuona damu inamwagika tena,asanteni
Ahaa , mmelianzisha sasa mnaogopa nini? komaeni mpaka mwisho na msitangulize wasio na hatia, daima muwe mbele.
 
Hakune asiyejua nn kilitoke huko Igunga kwani pamoja na vurugu zingine nyingi za hatari,kada wa chama kinachokuja kwa kasi ktk siasa za TZ ALIUWAWA, pamoja nafuraha ya wapenda haki tusiache kuombea uchaguzi huo kwa imani zetu.hatutaki kuona damu inamwagika tena,asanteni

Pamoja sana mkuu, ILA NOMBA KUJUWA JINSI YA KUPOST TREAD HAPA
 
Wakuu wangu naombe mnipe mwongozo.
Mbunge anapochaguliwa na kuapishwa huwa anapewa 90m ikiwa 45m ni mkopo anaopaswa alipe ndani ya miaka 5 ya ubunge wake na 45m ni ya kuwezeshwa.sasa kwa hawa wabunge waliovuliwa ubunge na mahakama hizo pesa atazilipaje ?
Naomba mwongozo
 
Naomba mwongozo, hivi Magamba hawatakata rufaa Igunga? Wamekubaliana na hukumu?
 
Aiseee baba yangu nilikuwa naulizia ule uchaguzi wa simbawanga vip??? Miezi 3 haijakwisha au wanafikiri 2mesahau
 
Naomba mwongozo, hivi Magamba hawatakata rufaa Igunga? Wamekubaliana na hukumu?
Magamba yalivyoonja joto ya jiwe Arumeru, yatafanya kila mbinu kuchelewesha uchaguzi kwa kukata rufaa. Kwa sasa hayana ubavu wa kupambana na CDM, hilo liko wazi.
 
mi ningeshauri chaguzi zisitishwe mpaka 2015 kwa sababu sioni sababu ya kumchagua mbunge akae miaka 2 afu uchaguzi tena...tunapoteza hela za walipa kodi tu hapo
 
mi ningeshauri chaguzi zisitishwe mpaka 2015 kwa sababu sioni sababu ya kumchagua mbunge akae miaka 2 afu uchaguzi tena...tunapoteza hela za walipa kodi tu hapo

Hiyo ndiyo gharama ya demokrasia.Nyumbani ukifiwa mfululizo huwezi ahirisha mazishi lazima wafu watazikwa na kula watu watakula hakuna kisingizio.Mbona pesa zetu zinaibiwa na mafisadi na hayashitakiwi bora tuzifaidi kwa kutekeleza matakwa ya demokrasia
 
mi ningeshauri chaguzi zisitishwe mpaka 2015 kwa sababu sioni sababu ya kumchagua mbunge akae miaka 2 afu uchaguzi tena...tunapoteza hela za walipa kodi tu hapo

Upo sahihi kiasi maana hujaitendea haki demokrasia na haki za watu kuwakilishwa bungeni. Lkn pia kumbuka kuhimiza wezi wote walioficha pesa Ulaya wakamatwe,wafungwe na kulipa
 
Back
Top Bottom