Pamoja na salamu za heri na baraka za mwaka mpya watanzania wenzetu.
Kimekuwa ni kilio kutoka kwa wananchi ambacho hakisikiki na wala hakigusi hisia ya kiongozi yeyote wilayani Ukerewe.
Taxi ama gari aina ya saloon hubeba watu kama abiria wasiopungua KUMI (10). Dereva hukaa na abiria watatu hadi wanne, nyuma hukaa zaidi ya sita wakati mwingine hata kwenye BUTI! Ni ngumu kupata picha inakuwaje watu idadi hii wanaweza kukaa ndani ya gari, wanakaaje?? lakini unahitaji kuona kwa macho ndipo uamini.
Polisi trafiki wanajua na wanalishuhudia hili na katu hawachukui hatua yoyote. Sasa tunamuomba waziri husika ama taasisi husika waje Ukerewe washuhudie mateso tunayoyapata sisi wananchi. Ni aibu kumlilia na kumuomba MH. RAIS JPM Wakati viongozi wanaomsaidia wapo. Mh Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mh. Spika Mstaafu wa Bunge la Afrika wanashuhudia na wanalijua hili na hawasemi lolote kwa vile wana magari yao. Nini faida kuwa na viongozi hata kama ni wastaafu hawatetei adha zinazowakumba wananchi waliowapa kura na kula katika awamu zilizopita?
Pamoja na kukaa kwa mateso watu wote mtalipa nauli sawasawa yaani tozo ni kwa kichwa. Hakuna bei ya jumla ya taxi wala bajaji. Kila kichwa hulipia safari nzima.
Matatizo na shida Ukerewe ni nyingi mno na vile ni kisiwa basi kimesahaulika.
Hatuna hata Police posts wala zima moto!
Tuuokoeni jamani Mh Mwigulu njoo utembelee Jamaica ya Africa uone wtu wanavyoishi kimaskini, kiyatima yatima!!!
Tulipata mkombozi MH. MKIRIKITI, tukadhani tumekumbukwa lakini alipoonekana kuchapa kazi tukanyang'anywa!! jamani! turudishieni MKIRIKITI wetuuuu! tunamumisi..
Ahsanteni,
wakatabahu,