Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,192
- 3,353
Hizi alama za shuleni zimekuwa zikitafsiriwa ndivyo sivyo kuwa ndio mafanikio pekee kwenye maisha ya wanafunzi mashuleni na vyuoni kabla hawajaingia rsmi mtaani, Vuta picha wewe ulipokuwa shuleni jinsi Yule kipanga wa darasa lenu alivyokuwa akisifiwa na walimu, kupewa zawadi za kufaulu, walimu na wazazi wenu kukuhamasisha uige mfano wake, n.k
Mfumo wetu ambao wengi tumupitia katika elimu, wazazi na walimu wetu walitujenga saikolojia kwamba kuna njia moja tu ya kufanikiwa ambayo ni kusoma kwa bidii ili uje upate maisha mazuri kwa kuajiriwa, Huu mzizi naomba ung’olewe vichwani mwa watoto wetu na wadogo zetu pindi utapomaliza kuusoma huu uzi.
Ijulikane ya kwamba kusoma sio njia pekee ya kupata maisha mazuri kama ambavyo wengi tulivyokua tukiaminishwa na wazazi / walezi / walimu wetu, Elimu ipo ili kupata maarifa ya ziada na kukuongezea ufanisi wa ziada katika maisha kwa kukuondolea ujinga,
Ukiona mtoto wako au mdogo wako anaweza mambo mengine nje ya masomo inabidi umwezeshe afikie kiwango cha juu kwa uhuru bila kubanwa kama sisi wakubwa zao enzi zile
Ndicho kinachotokea kwenye kozi ambazo wanachaguliwa vipanga ila hali ya ajira inakuwa ni mbaya, kwa mfano kozi ya petroleum chemistry ni kozi ambayo ili uchaguliwe inabidi uwe na division 1 matata sana ya form 6, darasa linakua limejaa vipanga wenye matumaini makubwa ila wanapohitimu vyuo matumaini yote huisha kwa sababu ajira hizi za mafuta na gesi ni ngumu mno kupata hii nchi, matokeo
Inabidi tuwakumbushe wadogo wetu kwamba despite wanaweza wakawa vizuri kwenye masomo bado inabidi wawekeze na kutilia mkazo kwenye vitu wanavyovipenda na sisi tuwe na jukumu la kuwapa wanachohitaji ili wawe bora
Kwa vile wanafunzi wengi hawajaandaliwa hivi, kumekuwa na matukio ya kujiua na kujiingiza katika ulevi kwajili ya kukata tamaa pale vijana wanapomaliza elimu za vyuoni wakiwa na alama za juu (first classs na upper second) wakiona kwamba dunia haijawatendea wema, hii inatokana na wao kukosa watu waliowajuza kwamba elimu ni mojawapo ya njia ya mafanikio katika njia kibao.

- Mtoto unamuona anapenda mpira vunja bajeti yako mpeleke kwenye academy kila jioni
- Mtoto umeona anapenda kompyuta tafuta kijana wa IT awe anakuja kumfundisha
- Mtoto umeona hujui anachopenda mwandalie mpeleke ajifunze chochote ambacho unaona kinaweza kumsaidia akiwa mkubwa