Tunyofoe mizizi ya ‘Soma sana uje kufanikiwa’ kwa kizazi kijacho cha watoto wetu

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Messages
2,997
Points
2,000

Machozi ya Simba

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2012
2,997 2,000
Hizi alama za shuleni zimekuwa zikitafsiriwa ndivyo sivyo kuwa ndio mafanikio pekee kwenye maisha ya wanafunzi mashuleni na vyuoni kabla hawajaingia rsmi mtaani, Vuta picha wewe ulipokuwa shuleni jinsi Yule kipanga wa darasa lenu alivyokuwa akisifiwa na walimu, kupewa zawadi za kufaulu, walimu na wazazi wenu kukuhamasisha uige mfano wake, n.k

Mfumo wetu ambao wengi tumupitia katika elimu, wazazi na walimu wetu walitujenga saikolojia kwamba kuna njia moja tu ya kufanikiwa ambayo ni kusoma kwa bidii ili uje upate maisha mazuri kwa kuajiriwa, Huu mzizi naomba ung’olewe vichwani mwa watoto wetu na wadogo zetu pindi utapomaliza kuusoma huu uzi.

Ijulikane ya kwamba kusoma sio njia pekee ya kupata maisha mazuri kama ambavyo wengi tulivyokua tukiaminishwa na wazazi / walezi / walimu wetu, Elimu ipo ili kupata maarifa ya ziada na kukuongezea ufanisi wa ziada katika maisha kwa kukuondolea ujinga,

Ukiona mtoto wako au mdogo wako anaweza mambo mengine nje ya masomo inabidi umwezeshe afikie kiwango cha juu kwa uhuru bila kubanwa kama sisi wakubwa zao enzi zile

  1. Mtoto unamuona anapenda mpira vunja bajeti yako mpeleke kwenye academy kila jioni
  2. Mtoto umeona anapenda kompyuta tafuta kijana wa IT awe anakuja kumfundisha
  3. Mtoto umeona hujui anachopenda mwandalie mpeleke ajifunze chochote ambacho unaona kinaweza kumsaidia akiwa mkubwa
Haya mambo ya kuwa mkali hadi kumgombeza au kumpiga mtoto kwasababu hajawa wa kwanza darasani yalipitwa na wakati, yanachangia sana mtoto kusoma kwa hofu bila raha na kumuharibu kisaikolojia, msingi wa mtoto inabidi ujengwe katika ustadi wa hali ya juu ili mbeleni akimaliza hata chuo ajue njia A na B za kutoka kimaisha, sio kamaliza chuo ana degree yake yenye first class ila hajui kingine kila siku anasubiria kazi za kuajiriwa tu yupo yupo miaka minne nyumbani anasubiri kuajiriwa,

Ndicho kinachotokea kwenye kozi ambazo wanachaguliwa vipanga ila hali ya ajira inakuwa ni mbaya, kwa mfano kozi ya petroleum chemistry ni kozi ambayo ili uchaguliwe inabidi uwe na division 1 matata sana ya form 6, darasa linakua limejaa vipanga wenye matumaini makubwa ila wanapohitimu vyuo matumaini yote huisha kwa sababu ajira hizi za mafuta na gesi ni ngumu mno kupata hii nchi, matokeo
Inabidi tuwakumbushe wadogo wetu kwamba despite wanaweza wakawa vizuri kwenye masomo bado inabidi wawekeze na kutilia mkazo kwenye vitu wanavyovipenda na sisi tuwe na jukumu la kuwapa wanachohitaji ili wawe bora

Kwa vile wanafunzi wengi hawajaandaliwa hivi, kumekuwa na matukio ya kujiua na kujiingiza katika ulevi kwajili ya kukata tamaa pale vijana wanapomaliza elimu za vyuoni wakiwa na alama za juu (first classs na upper second) wakiona kwamba dunia haijawatendea wema, hii inatokana na wao kukosa watu waliowajuza kwamba elimu ni mojawapo ya njia ya mafanikio katika njia kibao.
 
Joined
Jul 15, 2018
Messages
14
Points
45
Joined Jul 15, 2018
14 45
Hizi alama za shuleni zimekuwa zikitafsiriwa ndivyo sivyo kuwa ndio mafanikio pekee kwenye maisha ya wanafunzi mashuleni na vyuoni kabla hawajaingia rsmi mtaani, Vuta picha wewe ulipokuwa shuleni jinsi Yule kipanga wa darasa lenu alivyokuwa akisifiwa na walimu, kupewa zawadi za kufaulu, walimu na wazazi wenu kukuhamasisha uige mfano wake, n.k

Mfumo wetu ambao wengi tumupitia katika elimu, wazazi na walimu wetu walitujenga saikolojia kwamba kuna njia moja tu ya kufanikiwa ambayo ni kusoma kwa bidii ili uje upate maisha mazuri kwa kuajiriwa, Huu mzizi naomba ung’olewe vichwani mwa watoto wetu na wadogo zetu pindi utapomaliza kuusoma huu uzi.

Ijulikane ya kwamba kusoma sio njia pekee ya kupata maisha mazuri kama ambavyo wengi tulivyokua tukiaminishwa na wazazi / walezi / walimu wetu, Elimu ipo ili kupata maarifa ya ziada na kukuongezea ufanisi wa ziada katika maisha kwa kukuondolea ujinga,

Ukiona mtoto wako au mdogo wako anaweza mambo mengine nje ya masomo inabidi umwezeshe afikie kiwango cha juu kwa uhuru bila kubanwa kama sisi wakubwa zao enzi zile,

- Mtoto unamuona anapenda mpira vunja bajeti yako mpeleke kwenye academy kila jioni

-mtoto umeona anapenda kompyuta tafuta kijana wa IT awe anakuja kumfundisha

-Mtoto umeona hujui anachopenda mwandalie mpeleke ajifunze chochote ambacho unaona kinaweza kumsaidia akiwa mkubwa.

Haya mambo ya kuwa mkali kwa mtoto kwasababu hajawa wa kwanza darasani yalipitwa na wakati na yanachangia sana mtoto kusoma kwa hofu bila raha, mtoto inabidi ajengwe katika ustadi wa hai ya juu ili mbeleni akimaliza hata chuo aju A na B njia mbadala za kutoka kimaisha, sio kamaliza chuo ana degree yake yenye first class ila hajui kingine na kuanza kujutia ulipoitupa kompyuta yake aliyopenda kuitumia akiwa mdogo kwasababu alishika nafasi ya pili.

Ndicho kinachotokea kwenye kozi ambazo wanachaguliwa vipanga ila hali ya ajira inakuwa ni mbaya, kwa mfano kozi ya petroleum chemistry ni kozi ambayo ili uchaguliwe inabidi uwe na division 1 matata sana ya form 6, darasa linakua limejaa vipanga wenye matumaini makubwa ila wanapohitimu vyuo matumaini yote huisha kwa sababu ajira hizi za mafuta na gesi ni ngumu mno kupata hii nchi, matokeoInabidi tuwakumbushe wadogo wetu kwamba despite wanaweza wakawa vizuri kwenye masomo bado inabidi wawekeze na kutilia mkazo kwenye vitu wanavyovipenda na sisi tuwe na jukumu la kuwapa wanachohitaji ili wawe bora

Kwa vile wanafunzi wengi hawajaandaliwa hivi, kumekuwa na matukio ya kujiua na kujiingiza katika ulevi kwajili ya kukata tamaa pale vijana wanapomaliza elimu za vyuoni wakiwa na alama za juu (first classs na upper second) wakiona kwamba dunia haijawatendea wema, hii inatokana na wao kukosa watu waliowajuza kwamba elimu ni mojawapo ya njia ya mafanikio katika njia kibao.
Kwani lazima ututaje wana petroleum chem mzeee

Ebu acha nimalize kusoma
 
mimiks

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2013
Messages
973
Points
1,000

mimiks

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2013
973 1,000
Tatizo kuu ni mifumo yetu haijakaa vizuri. Mtoto kutoka kwenye maisha kwa kutumia kipaji chake Tanzania hii sio rahisi kihivo. Ukiritimba kila kona.

Hivi mfano una mtoto wa kike anapenda football au netball Tz hii utasema kweli umeendeleze kipaji chake kitamtoa.

Binti awe anapenda uigizaji au kuimba si kama unaenda kumueka sokoni kila mwenye uchu ajimegee anavyotaka.

Ndio maana wazazi wengi wanakomalia hapo hapo kwenye elimu. Anaona kidogo kuna mategemeo. Kwamba hata kama utachelewa kupata ajira, ila ipo siku utaipata tu.
 
Adverse Effect

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2017
Messages
650
Points
1,000

Adverse Effect

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2017
650 1,000
Nakubaliana na hoja zako ingawa hoja hizo zitategemea na shule au mfumo wa elimu anayopata mtoto.

Kuna shule hapo Dar watoto walikuwa na mahafali ya kumaliza darasa la saba nilipata bahati ya kuhudhuria. Kulikuwa na watoto kama 80 hivi wanaotarajia kuhitimu.

Mfumo wa elimu na taratibu za hiyo shule zinalazimisha kila mtoto ashiriki kikamilifu katika mchezo fulani au kipaji fulani na kuhakikisha anafanya vizuri sana, na mfumo wao umeweka walimu waliosomea katika maeneo hayo km kocha wa basketball, football, ping pong pia kuna michezo kama ya karate, judo, taekwando ambapo kila mwanafunzi ni lazima ajifunze bila kusahau muziki,ngoma, sanaa za maigizo n.k.

Katika hiyo shule katika ukuta wamechorwa wachezaji kama mbwana Samantha, messi na wengineo kwa ajili ya kuwa inspire vijana.

Kwa muktadha huo, hoja zako zitakuwa chanya na kutekelezeka kirahisi kutegemeana na shule pamoja na mfumo wa elimu unaotolewa, nimeona hata wazazi na walezi wa hiyo shule wanafahamiana kutokana na vipaji vya watoto wao na kwa pamoja wanashirikiana kuwasaidia watoto wao wafanye vizuri na kuendeleza vipaji vyao.

Mwisho ila sijamaliza, kwa mfumo wa elimu shule zetu za kata na kayumba safari bado ni ndefu sana, tusikate tamaa penye nia pana njia.
 
Pips Man

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Messages
1,135
Points
2,000

Pips Man

JF-Expert Member
Joined May 9, 2014
1,135 2,000

kila enzi na zama zake ingawa Kwan sasa inaonekana ajira ni chache ila nikwambie tu Hakuna kipindi kuna fursa nyingi za kufanya Kama kipindi hichi ktk maisha ya mwanadamu.

Vijana wenyewe tujiongeze na si kulalamika.
 
TruthLover

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2019
Messages
947
Points
1,000

TruthLover

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2019
947 1,000
Tatizo kuu ni mifumo yetu haijakaa vizuri. Mtoto kutoka kwenye maisha kwa kutumia kipaji chake Tanzania hii sio rahisi kihivo. Ukiritimba kila kona.

Hivi mfano una mtoto wa kike anapenda football au netball Tz hii utasema kweli umeendeleze kipaji chake kitamtoa.

Binti awe anapenda uigizaji au kuimba si kama unaenda kumueka sokoni kila mwenye uchu ajimegee anavyotaka.

Ndio maana wazazi wengi wanakomalia hapo hapo kwenye elimu. Anaona kidogo kuna mategemeo. Kwamba hata kama utachelewa kupata ajira, ila ipo siku utaipata tu.
Vipi kuhusu samata?
 
gwakipanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2011
Messages
627
Points
250

gwakipanga

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2011
627 250
Kuna mifumo na kujiongeza, wanafunzi wanaweza kushauriwa wafanye kitu nje ya masomo wanaona wanapoteza muda. Unaweza kuta nyumbani mama ni mjasiliamali lakini mtoto haoni kama ni fursa ya kujiongeza kwa vile anandoto kubwa, akifeli ndiyo anachanganyikiwa. Vijana waliowengi hawataki kufanya kazi nje ya taaluma zao hata kama fursa za kufanya hivyo zipo.
 
heradius12

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2011
Messages
10,104
Points
2,000

heradius12

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2011
10,104 2,000
Nakubaliana na hoja zako ingawa hoja hizo zitategemea na shule au mfumo wa elimu anayopata mtoto.

Kuna shule hapo Dar watoto walikuwa na mahafali ya kumaliza darasa la saba nilipata bahati ya kuhudhuria. Kulikuwa na watoto kama 80 hivi wanaotarajia kuhitimu.

Mfumo wa elimu na taratibu za hiyo shule zinalazimisha kila mtoto ashiriki kikamilifu katika mchezo fulani au kipaji fulani na kuhakikisha anafanya vizuri sana, na mfumo wao umeweka walimu waliosomea katika maeneo hayo km kocha wa basketball, football, ping pong pia kuna michezo kama ya karate, judo, taekwando ambapo kila mwanafunzi ni lazima ajifunze bila kusahau muziki,ngoma, sanaa za maigizo n.k.

Katika hiyo shule katika ukuta wamechorwa wachezaji kama mbwana Samantha, messi na wengineo kwa ajili ya kuwa inspire vijana.

Kwa muktadha huo, hoja zako zitakuwa chanya na kutekelezeka kirahisi kutegemeana na shule pamoja na mfumo wa elimu unaotolewa, nimeona hata wazazi na walezi wa hiyo shule wanafahamiana kutokana na vipaji vya watoto wao na kwa pamoja wanashirikiana kuwasaidia watoto wao wafanye vizuri na kuendeleza vipaji vyao.

Mwisho ila sijamaliza, kwa mfumo wa elimu shule zetu za kata na kayumba safari bado ni ndefu sana, tusikate tamaa penye nia pana njia.
Apo kwenye shule hata mimi nakusuport 100%. Mimi binafsi hili ninaexperience nalo.

O level nilisoma shule ya seminary iliyopo Uganda. Ile shule ilikuwa na extracurricular activities nyingi ambazo zinaweza mjenga mwanafunzi kujitegemea nje ya mfumo wa ajira.

A-level nilirudi Tz na nikasoma bording school ambayo mwanafunzi ni ;kusoma, sport, na kufua nguo zake tu. Yan unaamka asubuhi (saa 12) unakuta uji upo tyar mmeletewa kwenye mabweni. Wewe unatandika tu kitanda chako unakunywa uji na kwenda darasani. Mnakuta madarasa yameshafagiliwa...yani mwanafunzi hushiki ufagio wala dekio kufanya usafi. Na ukirudi bwenini unakuta pamedekiwa.
Meals ni kila siku mle wali na nyama. Jumapili ni pilau kuku. Breakfast chai na sikonzi mbili.

Chuo nikasoma chuo kimoja maarufu hapa Tz. Katika bylaw ya chuo, inazuia mwanafunzi kuwa na biashara au ajira. Yani ukiwa chuo wewe ni kusoma tu labda na michezo kidogo. Ila hii law ya kutokuwa na biashara niliivunja nikiwa mwaka wa kwanza, semista ya pili. Nilisave kamkopo kangu na kufungua duka la nguo za kiume maeneo ya chuo. Nikawa wekend naenda uganda au kenya kununua nguo. Faida nilyokuwa naipata kwa mwezi ni sawa na mwalimu wa secondary. Baada ya kumaliza chuo nikajiuliza, ni kwanini nikaajiriwe wakati naingiza pesa inayolingana na mishahara ya watumishi wengi? Nikaongeza na mradi mwingine wa ufugaji samaki na kilimo cha mbogamboga za kizungu. hii nilijifunza seminary nchini uganda.

Kwa sasa maendeleo niliyonayo miaka 4 baada ya kumaliza chuo sijaona hata classmate wangu yeyote aliyepata ajira kanifikia. Kila nikikutana nao wanatamani waachane na ajira wanifate mimi ila ajira nayo inakuwa kama wamefungwa jela, ni vigumu kutoka kwenye rat race.

Kwa kifupi. Nilitaka kuonesha kuwa mazingira ya shule zetu za tz hazijengi vijana wanaoweza jitegemea baadaye. Mimi hapa leo nisingesoma Seminary Uganda, nisingekuwa na idea ya kujushugulisha na kilimo/ ufugaji.

Ningefata sheria ya chuo ya kutokuwa na biashara ukiwa unasoma, nisingeweza kujifunza changamoto za ujasiliamali mapema. Ningemaliza chuo na kuanza kutangatanga na bahasha huku na kule ila mpaka leo sijawai peleka maombi yangu ya kazi popote. Hata cheti sijaendaga chukua kozi nilkuwa na deni chuoni.
Screenshot_20190825-081336_WhatsApp.jpeg
Ushauri wangu!

Serikali urudishe mfumo wa kuwa kila shule ile na shamba. Wanafunzi watengewe muda wa kuhudumia ayo mashamba. Kama ni mkoa unaolima alizeti, kuwe na shamba la alizeti, wanafunzi wajue jinsi ya kuilima. Kma ni dodoma ambapo kuna zabibu, basi kuwe na shamba la zabibu shuleni, wanafunzi wajifunze. Shule ziwe na waalimu wa kilimo. Somo la kilimo lirudishe mashuleni. Haiwezekani mtu anasoma primary had 4m6 hajui kushika jembe alafu unategemea akajiajiri.
 
Forum statistics

Threads 1,378,924
Members 525,244
Posts 33,728,369
Top