La Biblicana
JF-Expert Member
- Jan 1, 2013
- 556
- 344
Katika maisha ya mwanadamu, awe tajiri au maskini, matatizo na shida za maisha zipo. Haijalishi kiwango chako cha elimu wala ukoo unaotoka, shida na taabu za maisha zitaambatana na wewe kwa kadiri ya majaaliwa yako toka kwa Mungu. Lakini ni kawaida ya mwanadamu kuamini kuwa ni yeye tu ndie mwenye shida duniani kwa kuwa huwa tunaangalia yanayotusibu pasina kutafakari nini kesho yetu itatuletea; faraja au matatizo zaidi?
Kuna mwenye fedha, hana mtoto. Kuna mwenye mtoto, hana afya. Kuna mwenye afya, hana fedha. Kuna mwenye fedha na mtoto, hana afya, na kadhalika na kadhalika. Sasa swali linakuja: Ni namna ipi unakabiliana na yanayokusibu? Namna yako inaongeza au inapunguza madhila yako?
Hebu tupate tunu za HEKIMA, tuongeze ufahamu:
Badili maisha yako, badilika ndani kwanza. Katika yote yanayokusibu, usimsahau Mungu wako. Kama tajiri Ayubu alijaribiwa; Ayubu yule mcha Mungu, mbona sisi tuyakwepe?
[SUP]13[/SUP]Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya mwanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
1Wakorintho 10:13
Kumbe tunazeeka bure kwa kujishughulisha na yaliyo nje ya uwezo wetu?!

[SUP]21[/SUP]Usijizamishe roho yako katika huzuni,
wala kujikwaza katika shauri lako.
[SUP]22[/SUP]Changamko la moyo ndiyo uzima wa mtu,
na shangwe huzidisha siku zake.
[SUP]23[/SUP]Ujifurahishe roho yako na kuuburudisha moyo wako;
uiondoe huzuni yako mbali nawe;
kwa kuwa huzuni umewaangamiza wengi,
wala ndani yake hamna faida.
[SUP]24[/SUP]Wivu na hasira pia hupunguza maisha,
na kujisumbua kwaleta uzee kabla ya wakati wake.
[SUP]25[/SUP]Bali mtu mwenye moyo mkarimu hufurahi,
na chakula chake chamfaa.
Yoshua Bin Sira 30:21-25