TUNDURU: Rubani aliyeruka na ndege Oktoba 18, 2021 hajaonekana mpaka sasa

Isee naomba tusaidiane kumuombea rubani, nikijana mdogo wa miaka thelathini ya mwanzo, kwa waliosoma Mirambo amemaliza 2011 na SUA amemaliza 2014 alikua akisoma bachelor of science in wild life management, alitoka kwenye familia ya kawaida kiasi amesoma kwa michango michango sana, alikua ndo amekua nguzo kwenye familia yake bahati mbaya anataka kupotea kama upepo, Mungu amtunze na kumlinda popote alipo.
O-level alisoma Magu day namfahamu
 
Siku 11 ni nying sana. Sijui kwa nn walkua kimya hivyo kwa public...poor pilot..ingekua nchi yenye taasis imara very same day wangetangaza na search/rescue ingeanza
Ndege ya Malyasia ilipotea Hadi leo Hakuna Cha search Wala binamu yake rescue aliyefanikiwa kuipata
 
Ndege ya Malyasia ilipotea Hadi leo Hakuna Cha search Wala binamu yake rescue aliyefanikiwa kuipata
Ila taarifa za kupotea zilitoka mapema sana, huku kwenu baada ya siku 11 ndio taarifa zinatoka! Li nchi la hovyo sana hili
 
Jamani , kabla ya kuanza kulaumu kwanza mnapaswa kufahamu ni jinsi gani Radar zinafanya kazi.

Tukio la kupotea kwa ndege siyo la kwanza kutokea Tanzania tu, ndege zimekuwa zikipotea dunia tena midege mikubwa kabisa ya abiria achilia mbali hako kandege kadogo.

Kama mnafuatilia habari mtakumbuka ile ndege ya Malaysian Airline MH370 ilipotea mwaka 2014 ikiwa na abiria 227 na mpaka wa leo haijulikani ilipo.

Licha ya Radar za kisasa kabisa zinazoendeshwa kwa technolojia ya juu kabisa lakini hii ndege ilipotea. Nawashangaa sana kulaumu Radar za Tanzania. Mnachotakiwa kujua ni kwamba Radar sio kila kitu, ndege inaweza kupotea na hata Radar isiweze kuona na hiyo siyo kwa Tanzania pekee ni mpaka huko Ulaya.
Huko Duniani ndege zinazopotea ni kweli ni kubwa zinazokatiza bahari sio vidogo kama hivi usikie kilipotea Marekani hakijaonekana siku 11 huwa tunaambiwa zilikopata majanga..ndege hairuki anga la kimataifa kapo tuu hapa juu mbugani hatukaoni tunasema hata Ulaya zinapotea kweli ?
 
Pole yake kwaujangili walewatu Kama walidungua inawezekana walichimba shimo wakaifukia mbona ndogo tu fukia rubani nambaki
 
Ila taarifa za kupotea zilitoka mapema sana, huku kwenu baada ya siku 11 ndio taarifa zinatoka! Li nchi la hovyo sana hili
Songea. Rubani Samwel Gibuyu aliyekuwa akirusha ndege aina ya BatHawk yenye numba za usajili 5H-WXO inayomilikiwa na Shirika lisilo la kiserikali (Ngo) ya Protectors Area Management Solution Foundation (PAMS Foundation) anadaiwa kupotea kwa muda wa siku 11.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro imesema rubani huyo anadaiwa kupotea tangu Oktoba 18, 2021 saa 9 jioni kuelekea pori la akiba la Selous kanda ya Kingipira.

Mtatiro amsesema ndege hiyo iliombwa na Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (Tawa) kupitia Shirika la Uhifadhi la Frankfurt Zoological Society (FZC) ili kusaidia zoezi la ufatiliaji wa Faru mweusi katika pori la akiba la Selous.

Amesema baada ya kuruka ilionekana na wachimba madini eneo la Matuli na baadaye Kijiji cha Kajima kata ya Jakika tarafa ya Matemanga wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma ilielekea mashariki mwa Kijiji cha Kajima.

Kijiji hicho kinakadiriwa kuwa na umbali wa 26 Km

"Ndege ilitarajiwa kutua kingiupira kati ya saa 5:30 alasiri hadi 6:09 alasiri kwa bahati mbaya haikufika ndipo walipoanza kuwasiliana pande zote mbili," amesema

Ameongeza kuwa baadhi ya watumishi waliwasiliana na Mkurugenzi wa Shirika la PAMS Foundation ambaye aliangalia kwenye spider Track ya ndege hiyo yenye uwezo wa kuonyesha alipopita na ilipo ndege hiyo.

Amefafanua kuwa track ilionyesha wakati akiruka hakukuonesha taarifa zozote hadi muda anatafutwa.

Oktoba 19 ndege tatu zilitumwa kuitafuta ndege hiyo kwa kukwagua njia ambayo ndege ilizaniwa ingepita, kukagua viwanja vya ndege vilivyopo karibu na njia hiyo pamoja na mito mikubwa.

Oktoba 21 ndege ya Tawa pamoja na helikopta ya polisi zilitumika kufanya utafutaji na uokoaji ambapo zilipita Katika njia hiyo.

Pia wakiendelea na ufatiliaji huo Oktoba 21 ndege ya Tawa na FZS pamoja na helikopta ya polisi ziliendelea na ufatiliaji na uokozi ambapo majira ya mchana walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa ndege hiyo ilionekana majira ya saa 11 jioni ikipita kimo cha mnazi ikirudi uwanja wa Matemanga

Amesema baada ya taarifa hiyo timu ya uokoaji iligawanyika makundi na kutawanyika kutafuta ndege hiyo kwa kutumia miguu, pikipiki na wengine magari

Mtatiro ameongeza kuwa siku ya Oktoba 24 na 27 ndege zingine mbili binafsi ziliongezwa kufanya ufatiliaji wa kina kwa siku nne mfululizo kwenye vijiji ambavyo vipo karibu na ndege hiyo iliporuka.

Amesema hata hivyo kikosi cha ufatiliaji na uhokoaji kilishauri operesheni za ndege zisimame huku zikiendelea kufanya utafutaji kwa kutumia taarifa za wananchi na taarifa za kiintelejinsia.

Amewataka watendaji na wenyeviti wa vijiji waitishe mikutano ya hadhara kwa lengo la kuwahamasisha watoe taarifa ya kuonekana kwa ndege hiyo kwenye maeneo yao.
 
Amesoma milambo then akaenda sua

Bachelor of science in wild life
Sina hakika kama huyu mwamba kwenye combination yake alikua na PCM au PGM

lazima alisoma PCB au CBG
Huwezi soma BAM alafu ukaenda rusha ndege, tue makini Sana ktk hili
Kurusha ndege unarusha tu mkuu ....vyuo viko vingi sana South Africa...basic English collage language
 
Shida ya pori la selou kuna eneo ambalo halijawahi kanyagwa na binadamu tokea Dunia Iumbwe na mwenyezi Mungu

Pori kubwa mnooo
 
Shida ya pori la selou kuna eneo ambalo halijawahi kanyagwa na binadamu tokea Dunia Iumbwe na mwenyezi Mungu

Pori kubwa mnooo
acha hizo kuna wakurungwa wanawinda kila siku humo mi nimewinda sana humo nikiwa mdogo tulikua tunaingilia msolwa wawindaji wanajua vituo vyote humo kuwa ukiingia hapa unatokea wapi na kuna wafugaji wanapita humo poli kwa pori kulisha mifugo yao
 
Rubani na ndege inapotea mnatoa taarifa kwa umma baada ya siku 11?
Hiyo mbona ya juzi tu,kuna askari polisi tena inspector amepotea tangu JUNE 26 2021 wa kituo cha polisi mtumba mji wa kiserikali dodoma na haijulikani aliko mpaka leo.
 
Back
Top Bottom