Tundu lisu aliomba kwenda ikulu alikubaliwa?

lendila

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
5,680
2,000
Tundu lisu aliwai kuomba kwenda ikulu kuonana na mh rais je alikubaliwa? Lisu alimwandikia mh,rais barua akiomba kuonana naye ili washauriane mambo yanayohusu sheria je ameshajibiwa barua yake?
Mh,tundu lisu aliweka wazi kabisa anataka kwenda kumpa mh,rais ushauri wa mambo ya kisheria,je kwanini barua yake haijajibiwa mpaka leo?
Wazungu tuliaminishwa ni wezi wameomba kuonana,na mh rais wamekubaliwa haraka haraka,lkn tundu lisu mtanzania anaheshimika kwenye nyanja ya sheria ameomba kuonana na mh rais amekataliwa,huoni kukataliwa kwa lisu ambaye ni mswahili mwezetu ndio kinachofanya wazungu watuzarau?
Nimemsikia mh rais akisema vita hii ya wizi wa rasilimali haina vyama,na mm nakubaliana naye vita hii haina vyama,je mh rais kwanini asikae meza moja na vyama vyenye wabunge bungeni waridhiane kwa pamoja njia sahihi ya kupigana vita hii ya wizi wa raslimali zetu kwa pamoja?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom