Tundu Lissu unakumbuka kitu?

Tundu Lissu unakumbuka kitu?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,613
Katika maisha siku zote ni muhimu kukumbuka makosa tunayoyafanya mara chache sana sisi binadamu tunakumbuka na kukubali makosa ambayo tumeyafanya zamani na yanakuja kutuumiza leo.

Kama ndugu Tundu Lissu atapitia hapa ni vizuri akakumbuka kitu.

'Bunge la Katiba'.....

Hakuna mtu katika bunge lile la katiba aliekuwa na nguvu kama Tundu Lissu yeye alikuwa ndo 'roho' ya kila mtu alietaka 'Rasimu ya Warioba' hata UKAWA ni kama alianzisha yeye na wengine wakamuunga mkono.

Itoshe kusema kuwa kama Tundu Lissu angeweza kuwashawishi wenzie wabaki kwenye bunge la katiba kwa 'faida' zingine hilo lingewezekana

Tusisahau original wanaUKAWA walikuwepo hadi wana CCM ambao walikuwa
wanataka 'Rasimu ya Warioba' iheshimiwe.

lakini kosa kubwa kabisa la wanaUKAWA ni 'kubeba hoja za Tanganyika' mbele ya hoja zoote muhimu za Rasimu ya Warioba.

Rasimu ya Warioba ilikuwa ina faida nyingi zaidi

1.Tume huru ya uchaguzi
2.Kufuta wakuu wa wilaya
3.kupunguza madaraka ya Rais na kadhalika na kadhalika

Leo Tundu Lissu anakamatwa na polisi kwa 'amri za wanasiasa'
Bunge la katiba lilikuwa na nafasi ya kupiga marufuku polisi kupewa amri ya kumkamata mtu.

Hata Kenya now wametuacha Rais wa Kenya hawezi kuitumia polisi kukamata wapinzani wake washalimaliza hilo kwa kupitia katiba.

Leo Rais anateua makada kuwa wakuu wa wilaya na ma DAS.
Katiba hii iliyopo ambayo Magufuli anaitumia ni mbovu kuliko ile ya Samuel Sitta

Laiti kama Tundu Lissu angetumia ushawishi wake japo kupata 'katiba nafuu'
kuliko hii anayoitumia Magufuli now huenda leo wapinzani wasingekuwa 'wanalia kupigwa marufuku siasa'.

Leo Magufuli angelazimika tu kuheshimu na kufuata baadhi ya vitu
Polisi wasingepokea amri.
Wakuu wa mikoa na wilaya labda wasingekuwepo hawa waliopo na kadhalika.

Tukubali tu kwa Wana UKAWA then kususa kushiriki katika bunge la katiba na kuipinga Katiba ya Sitta ambayo laiti wangeshiriki ingekuwa better kuliko hii ilikuwa a big mistake.

Sasa haya ndio mavuno, tumerudi nyuma miaka 50.

Some opportunities never comes twice.
 
Wanafiki waseme ndiooo ndiooooooooooooooooooooooooo ,wasiowanafiki waseme siyo siyo siyooo.

wanafiki ambao ni wengi kwa idadi ambao ni makada wa CCM kwenye bunge la katiba wangeshinda tu upinzani ungechemsha tu so lissu hana kosa hapo.
 
Katika maisha siku zote ni muhimu kukumbuka makosa tunayoyafanya
mara chache sana sisi binadamu tunakumbuka na kukubali makosa
ambayo tumeyafanya zamani na yanakuja kutuumiza leo....

Kama ndugu Tundu Lissu atapitia hapa ni vizuri akakumbuka kitu....

'Bunge la Katiba'.....

Hakuna mtu katika bunge lile la katiba aliekuwa na nguvu kama Tundu Lissu
yeye alikuwa ndo 'roho' ya kila mtu alietaka 'Rasimu ya Warioba'

hata UKAWA ni kama alianzisha yeye....na wengine wakamuunga mkono...

Itoshe kusema kuwa kama Tundu Lissu angeweza kuwashawishi wenzie wabaki kwenye bunge
la katiba kwa 'faida' zingine...hilo lingewezekana

Tusisahau original wanaUKAWA walikuwepo hadi wana CCM....ambao walikuwa
wanataka 'Rasimu ya Warioba' iheshimiwe.....

lakini kosa kubwa kabisa la wanaUKAWA ni 'kubeba hoja za Tanganyika' mbele ya hoja zoote
muhimu za Rasimu ya Warioba.....

Rasimu ya Warioba ilikuwa ina faida nyingi zaidi

1.Tume huru ya uchaguzi
2.Kufuta wakuu wa wilaya
3.kupunguza madaraka ya Rais... na kadhalika na kadhalika

Leo Tundu Lissu anakamatwa na polisi kwa 'amri za wanasiasa'
Bunge la katiba lilikuwa na nafasi ya kupiga marufuku polisi kupewa amri ya kumkamata mtu...

Hata Kenya now wametuacha.....Rais wa Kenya hawezi kuitumia polisi kukamata wapinzani wake
washalimaliza hilo kwa kupitia katiba.....

Leo Rais anateua makada kuwa wakuu wa wilaya na ma DAS...
Katiba hii iliyopo ambayo Magufuli anaitumia ni mbovu kuliko ile ya Samuel Sitta

Laiti kama Tundu Lissu angetumia ushawishi wake japo kupata 'katiba nafuu'
kuliko hii anayoitumia Magufuli now...huenda leo wapinzani wasingekuwa 'wanalia kupigwa marufuku siasa'.....

Leo Magufuli angelazimika tu kuheshimu na kufuata baadhi ya vitu
Polisi wasingepokea amri ....
wakuu wa mikoa na wilaya labda wasingekuwepo hawa waliopo na kadhalika.....

Tukubali tu kwa Wana UKAWA then kususa kushiriki katika bunge la katiba na kuipinga Katiba
ya Sitta ambayo laiti wangeshiriki ingekuwa better kuliko hii....ilikuwa a big mistake....

sasa haya ndo mavuno.........tumerudi nyuma miaka 50.......
some opportunities never comes twice....
Una hoja japo nadhani ile katiba ya CCM ingetuumiza zaidi hivyo kwa mtazamo wangu, tungelazimika kutumia nguvu nyingi kudai mchakato mpya.

Kwa sasa liko wazi kwamba hawakushiriki ule upuuzi na tuna kila sababu ya kuendelea kudai haki hii ya katiba ya wananchi
 
kwani katiba ya sasa na sheria zetu si zinatambua demokrasia na haki ya vyama kufanya siasa?, lakini mbona hawaiheshimu?, nakuhakikishia hata kama ingekuwa katiba ya Warioba, wangeamua kutoiheshimu wasingeiheshimu tu

Katiba ya sasa Rais anamteua mkuu wa polisi
ni rahisi kwake kumpa amri

ingekuwa katiba hana mamlaka ya kumteua mkuu wa polisi ingekuwa rahisi kuliko sasa
 
Umeongea kitu cha maana sana The Boss.
Kosa la ukawa ndilo hilo,ccm wanaweza kukubali tume huru na vitu vingine lakini siyo kukubali serikali tatu,ukawa walikuwa na nafasi kubwa kutengeneza mazingira mazuri ya wao kufanya kazi kupitia bunge la katiba.
 
Ni kweli bt si kwa gemu ambayo refa wao uwanja wao hata mpira ni wao ukiwafunga wanagomea matokeo ukiwashtukiza bao la dk ya mwisho wanaweka mpira kwapani kama Jecha alivyofanya pande zile

Hapa inaitaji nguvu ya umma uliochoka na kukubali kwa lolote wakina Tundu ni wachache kuwin hili battle
 
Hatulilii maji yalokwisha mwagika, pia ilikuwa ni kujidhalilisha mno kipindi kile. Usife moyo, kuna siku pambazuko litatokea tu
 
Bado katiba hii yenye viraka chungu nzima pamoja na ubaya wake inaruhusu maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani ambayo hakuna yoyote mwenye ruhusa ya kuwaamulia wapinzani nini cha kuzungumza kwenye mikutano yao na wapi pa kufanyia mikutano yao bila kujali kama wana mbunge kwenye jimbo husika au la. Na yeyote anayewazuia wapinzani kufanya hivyo anakiuka katiba ya nchi.
 
Back
Top Bottom