Tundu Lissu: Tutathmini kazi tuliyoifanya na matokeo tuliyoyapata. Tupate mafundisho sahihi ya kazi

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Anaandika Mwanasheria wa Chadema Tundu Lissu.

Waheshimiwa na makamanda poleni kwa mapambano na hongereni kwa kazi kubwa mliyoifanya kwenye chaguzi hizi. Naona kila mmoja wetu anasikitika jinsi matokeo ambavyo yamekuwa tofauti na matarajio yetu na kazi tuliyoifanya.

Ni rahisi, katika mazingira haya ya kushindwa na kabla vumbi halijaisha, kuanza kulalamika, kunyoosheana vidole na kukatishana tamaa. Hii haitusaidii sana. Badala yake, tunachohitaji zaidi ni 'brainstorming' kuliko 'blamestorming.' Naomba nifanye ya kwanza. Chaguzi ndogo za ubunge au udiwani ni ngumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi yetu.

Mifano michache inathibitisha ukweli huu. Katika election cycle ya '05-'10, tulishinda Jimbo la Tarime lakini tukapigwa Biharamulo Magharibi na Busanda. Tarime lilikuwa Jimbo letu tangu Uchaguzi Mkuu wa '05, Busanda lilikuwa la maCCM na Biharamulo Magharibi lilikuwa la TLP. Sikumbuki vizuri kama tulishinda Kata hata moja katika mzunguko wa uchaguzi wa kipindi hicho.

Katika election cycle ya '10-'15, tulipigwa Igunga licha ya kazi kubwa tuliyofanya, lakini tukashinda Arumeru Mashariki iliyokuwa chini ya maCCM. Vile vile tulishindwa Kalenga, Chalinze na Ulanga Magharibi yaliyokuwa ya maCCM tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwenye chaguzi za Kata za '12 kama mnakumbuka, licha ya kazi kubwa na rasilimali nyingi, tulipata Kata tatu tu kati ya 26 zilizokuwa zinagombaniwa. Ukiachia Ifakara Mjini ya Mh. Juakali, Kata nyingine mbili - Kiboriloni na Iseke - zilikuwa zetu tangu Uchaguzi Mkuu wa '10.

Kwa mantiki hii, matokeo ya jana sio ya kushangaza sana. Kata ya Duru ilikuwa ya kwetu na tumeitetea, nyingine zote tulikopigwa zilikuwa za maCCM. Hatujanyang'anywa iliyokuwa yetu, hatujanyakua zilizokuwa zao. Hata hivyo, funzo kubwa zaidi la historia ya chaguzi hizi ni hili hapa: licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo hizi, tumeendelea kufanya vizuri zaidi katika kila Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha chaguzi ndogo.

Mwaka '10 tulifanya vizuri zaidi licha ya kupigwa Busanda na Biharamulo Magharibi katika mzunguko wa '05-'10. In fact, tulichukua Jimbo la Biharamulo Magharibi mwaka huo. Na tulipata Kata nyingi zaidi '10 kuliko ilivyokuwa '05. Mwaka '15 tulipata ushindi mkubwa zaidi katika Kata na majimbo licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo za mzunguko wa '10-'15.

Hoja yangu hapa ni kwamba uchaguzi wa marudio hauna direct and negative bearing kwenye matokeo yetu ya Uchaguzi Mkuu unaofuatia. On the contrary, uchaguzi wa marudio unatupa fursa ya kupanda mbegu ambayo, ikitunzwa vizuri, inakuwa na mazao bora kwenye chaguzi zinazofuatia.

Kwa upande mwingine, chaguzi za marudio - kwa sababu ya udogo au uchache wa maeneo yanayogombaniwa - yanawapa maCCM fursa ya kutumia nguvu kubwa za rasilimali na za kidola ukilinganisha na tunazotumia sisi. Kwenye Uchaguzi Mkuu unaofuatia, nguvu hizo zinasambazwa nchi nzima na kwa hiyo effectiveness yake inapungua.

Ndio maana tumefanya vizuri zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko kwenye chaguzi ndogo za marudio. Hili, kwa maoni yangu, ndilo fundisho kuu la chaguzi hizi za marudio. Hatuna sababu kubwa ya kushangilia kutokana na matokeo ya jana. Hata hivyo, hatuna sababu yoyote ya kuomboleza pia. Obviously, maCCM na wapambe wao wataandika 'wasifu wa marehemu' wa CHADEMA/UKAWA na kuutangaza dunia nzima na kwa sauti kubwa. Hilo lisitupofushe macho yetu, hata kama linakera sana.

Tutathmini kazi tuliyoifanya na matokeo tuliyoyapata. Tupate mafundisho sahihi ya kazi hiyo na matokeo yake. Tutumie mafundisho hayo kwa kujipanga vizuri zaidi kwa ajili ya 'the real prize': 2020.
 
Tundu Lissu amesahau juzi alisema nini kwenye Radio DW ya Ujerumani wakati akihojiwa na mtangazaji Mohammed Abdulrahman.

Tundu Lissu alisema hizi chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zitatoa tathmini ya utawala wa Rais Magufuli kwa mwaka mmoja akiwa Rais wa Tanzania. Well, tathmini ameipata.

Kwa kifupi ni kwamba, UKAWA wamepata ''kipigo cha mbwa'' katika chaguzi.

Badala ya kuukubali ukweli ili watafute majibu sahihi wanachofanya ni kuanza spin za kitoto.

Inashangaza kwa sasa anakuja na ngojera zingine ili kuwaaminisha tofauti na pia kuwafariji wenye kumbukumbu finyu.

Ndio yaleyale ya kutuambia kwa zaidi ya miaka minane kuwa Lowassa ni fisadi papa na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini kabla ya miezi mitatu kuingia kwenye uchaguzi mkuu, akampatia nafasi ya kugombea Urais.

Tanzania kuna vituko vya wanasiasa!
 
ukawa tumepigwa, tatizo tunatumia muda mwingi jamii forumas, fb, instagram, twitter kwa inshu za akina saanane, Mara njaa, Mara Anne kilango, Mara kiwanda cha dangote, Mara ukuta, Mara kata funua, Mara miili saba ya MTO ruvu, yaan hata hatueleweki ajenda yetu nini kila tukio tunadandia tena kwa mbele!! tujifunze
 
Siasa sio mchezo. Kwahiyo chadema na ukawa wanakiri wataendelea kupigwa tu. Kwanini wasitunze rasilimali zao?
 
Kwa wezangu na mimi tusiopenda kufikiri tunaona kila anachoandika jamaa ni kweli.

Ukweli ni kuwa hata wao wameongeza nguvu sehemu zote kama CCM wanavyofanya wao. Cha ajabu kiko hapa, CCM wanafanya kampeni wakati CDM Lowassa yuko kwenye kampeni huku Mbowe anapanga safu ya uongozi wake watakaomuunga kwenye chaguzi za ndani.

Ndo mmeona kanda ya Ziwa akipambana na uchaguzi wa ndani badala ya kunadi sera za chama chake.

Mbowe katelekeza makamanda kwa sababu ya nafasi yake inanyemelewa na EL.
 
Tundu Lissu amesahau alisema nini kwenye Radio DW ya Ujerumani wakati akihojiwa.

Tundu Lissu alisema hizi chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zitatoa tathmini ya utawala wa Rais Magufuli kwa mwaka mmoja akiwa Rais wa Tanzania.

Inashangaza kwa sasa anakuja na ngojera zingine ili kuwaaminisha tofauti na kuwafariji wenye kumbukumbu finyu.

Tanzania kuna vituko vya wanasiasa!
Naomba nifanye ya kwanza. Chaguzi ndogo za ubunge au udiwani ni ngumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi yetu.
Tundu Lissu.
 
Hatuna sababu kubwa ya kushangilia kutokana na matokeo ya jana. Hata hivyo, hatuna sababu yoyote ya kuomboleza pia. Obviously, maCCM na wapambe wao wataandika 'wasifu wa marehemu' wa CHADEMA/UKAWA na kuutangaza dunia nzima na kwa sauti kubwa.
 
Nafikiri sasa Lissu na UKAWA yote , vyama vya upinzani, watetezi wa haki Za binadamu na wapenda mabadiliko wote lazima tuje na Agenda moja ya kitaifa...KATIBA MPYA iliyotokana na rasimu ya Warioba ambayo itatupatia TUME HURU YA UCHAGUZI... Basi.
Ni kweli kabisa mkuu bila TUME HURU YA UCHAGUZI basi upinzani wasahau kushinda uchaguzi .
 
Narudia tena ni muda muafaka kwa chadema na wapinzani wa kweli kujipanga upya na kujitadhimini kwa marefu na mapana ni wapi pa kurekebisha ili kuuzika kwa wananchi.

Safu ya uongozi chadema ni ya kufumuliwa yote, mbowe si mpinzani ni chuma ulete wa ruzuku tu.

Lowasa si mpinzani na jeshi lake lote.

Wana chama wa chadema na wafuasi wake uendeshwa na miemuko sana bila ya akili yakinifu.

Chadema kina wapiga kelele wengi na si wapiga kura wengi.
 
Tundu Lissu amesahau alisema nini kwenye Radio DW ya Ujerumani wakati akihojiwa.

Tundu Lissu alisema hizi chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zitatoa tathmini ya utawala wa Rais Magufuli kwa mwaka mmoja akiwa Rais wa Tanzania. Well, tathmini ameipata.

Inashangaza kwa sasa anakuja na ngojera zingine ili kuwaaminisha tofauti na pia kuwafariji wenye kumbukumbu finyu.

Ndio yaleyale ya kutuambia kwa zaidi ya miaka minane kuwa Lowassa ni fisadi papa na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini kabla ya miezi mitatu kuingia kwenye uchaguzi mkuu, akampatia nafasi ya kugombea Urais.
Tanzania kuna vituko vya wanasiasa!
Tunafahamu kote ulikuwa unazunguka lakini lengo lako ni Lowassa hapa. Ukirudi kwa tathmini ya Lisu hujaonyesha kwanini una criritisize hoja yake kuwa uchaguzi huo utatoa tathmini ya utawala wa JPM kwa mwaka mmoja. Yeye ameonyesha kwamba CCM chini ya utawala wa mwaka mmoja wa JPM wameshindwa kuwanyang'anya Chadema kata yao!
 
Kwa sasa viongozi WA mikoa, wilaya, kata ni wateule na makada ya chama ccm. Hapo hapo ndio wasimamizi wa chaguzi. Mfano kwa kata ya Kimwani wilayani Muleba, kamati ya siasa ya ccm ilikaa Wiki mbili kabla chini ya mkoa wa kagera. Aliagiza kuwa wao ndio serikali hivyo kushindwa kimwani hapana. Vijana wa chadema wakatwe wakati wanahangaika kujitoa ndani sisi tuna maliza mambo yetu. Siku ya uchaguzi jana vyombo vyote vya dola vilihamishiwa Kimwani. Viongozi takribani watano waliwekwa ndani. Vituoni kulifanywa kwa watakavyo yaani a kuitwa b, hapo wapi wapinzani walaumiwe au ccm wasifiwe?
 
Kwa wezangu na mimi tusiopenda kufikiri tunaona kila anachoandika jamaa ni kweli.

Ukweli ni kuwa hata wao wameongeza nguvu sehemu zote kama CCM wanavyofanya wao. Cha ajabu kiko hapa, CCM wanafanya kampeni wakati CDM Lowassa yuko kwenye kampeni huku Mbowe anapanga safu ya uongozi wake watakaomuunga kwenye chaguzi za ndani.

Ndo mmeona kanda ya Ziwa akipambana na uchaguzi wa ndani badala ya kunadi sera za chama chake.

Mbowe katelekeza makamanda kwa sababu ya nafasi yake inanyemelewa na EL.
Joto la Lowassa lililowasumbua CCM ndo linalommyemelea na kumtoa jasho Mbowe.
Ukikaribisha tembo kwenye hema....ndo matokeo yake haya sasa...
Chadema haiwezi kuwa na mafahali wawili na Lowassa hawezi kuwa chini ya mtu huko Chadema.
Hilo liko wazi tangu mwanzo....anafika kwenye vikao baada ya Mbowe na anaondoka kabla ya Mbowe..
Hapo boss nani?
Na ilw kugoma kuvaa vaa magwanda na kupiga marufuku harakati za chadema....
It was just a matter of time..
 
Tundu Lissu amesahau alisema nini kwenye Radio DW ya Ujerumani wakati akihojiwa.

Tundu Lissu alisema hizi chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zitatoa tathmini ya utawala wa Rais Magufuli kwa mwaka mmoja akiwa Rais wa Tanzania. Well, tathmini ameipata.

Inashangaza kwa sasa anakuja na ngojera zingine ili kuwaaminisha tofauti na pia kuwafariji wenye kumbukumbu finyu.

Ndio yaleyale ya kutuambia kwa zaidi ya miaka minane kuwa Lowassa ni fisadi papa na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini kabla ya miezi mitatu kuingia kwenye uchaguzi mkuu, akampatia nafasi ya kugombea Urais.
Tanzania kuna vituko vya wanasiasa!
Sasa unashangaa nini na wewe, kama anaweza kusema mzee fulan ni fisadi tena hadharan halafu kesho akakataa atashindwa kwa hili? Hawa tuwazoee tu
 
Tundu Lissu amesahau alisema nini kwenye Radio DW ya Ujerumani wakati akihojiwa.

Tundu Lissu alisema hizi chaguzi ndogo za ubunge na udiwani zitatoa tathmini ya utawala wa Rais Magufuli kwa mwaka mmoja akiwa Rais wa Tanzania. Well, tathmini ameipata.

Inashangaza kwa sasa anakuja na ngojera zingine ili kuwaaminisha tofauti na pia kuwafariji wenye kumbukumbu finyu.

Ndio yaleyale ya kutuambia kwa zaidi ya miaka minane kuwa Lowassa ni fisadi papa na hafai hata kupewa fomu ya kugombea Urais lakini kabla ya miezi mitatu kuingia kwenye uchaguzi mkuu, akampatia nafasi ya kugombea Urais.
Tanzania kuna vituko vya wanasiasa!
Mkuu kwani ccm mmefanikiwa kunyakua kata ngapi zilizokuwa zinashikiliwa na chadema
 
Mkuu kwani ccm mmefanikiwa kunyakua kata ngapi zilizokuwa zinashikiliwa na chadema
Mkuu;
Hufahamu kama hizo kata zilikuwa ziko wazi/hazina madiwani ndio maana uchaguzi ukafanyika?

Hakuna kata iliyokuwa inashikiliwa na yeyote. Kama kata zingekuwa zinashikiliwa na mtu/chama basi hata uchaguzi usingefanyika.

Hii ni mantiki ambayo hata mtoto wa darasa la nne atafahamu.
 
Back
Top Bottom