Tundu Lissu: Tusishabikie maamuzi ya kijinga kwasababu tu yamefanywa na Rais

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia CHADEMA ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu amesema wabunge wanatakiwa kutoshabikia maamuzi ya kijinga hata kama yamefanya na Rais.

"Gharama tutakayolipa kwa kuzuia mchanga kusafirishwa nje kinyume na sheria ni kubwa kuliko mchanga wa madini wa ACACIA. Tusishabikie maamuzi ya kijinga kwasababu tu yamefanywa na Rais"-alisema Mbunge Tundu Lissu.

Mbunge Tundu Lissu akizungumzia kuzuiwa usafirishaji wa mchanga wa madini wakati wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje 2017/18.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chadema ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu asema wabunge wanatakiwa kutoshabikia maamuzi maamuzi ya kijinga hata kama yamefanya raisi.
"Tusishabikie maamuzi ya kijinga kwasababu tu yamefanywa na raisi"- Mchanga wa Makanikia

"Hawa wengine wabunge wanaopiga kelele, wasio jua kitu!" by TL
 
jambo la msingi bunge limsaidie rais kwa kuomba mikataba yote ipitiwe upya. pia bunge liache tabia ya kupitisha mambo kwa hati ya dharura. pia bunge liwanyang'anye vyeo vya bunge watu wote waliohusika kupitisha mikataba hii ya kimangungo .pia bunge lipendekeze kuvua kinga viongozi wastaafu walioliingoza taifa katika mikataba mibovu. vinginevyo waache vigelegele vya kimsifu rais kinafiki.
 
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kupitia Chadema ambaye pia Mwanasheria Mkuu wa Chadema Tundu Lissu asema wabunge wanatakiwa kutoshabikia maamuzi maamuzi ya kijinga hata kama yamefanya raisi.
"Tusishabikie maamuzi ya kijinga kwasababu tu yamefanywa na raisi"- Mchanga wa Makanikia

Mzee Strikes again! Mzee warns everyone not to temper with his publications! by Mzee Punch, 1983.
 
Ila si wanatuibia lakini? Lissu to a njia sahihi ya kulimaliza hili! Siyo kuponda bhana!!!!
Nani wanatuibia? Kwani mkataba ulikuwa wa upande moja? Huu ujinga mnautoa wapi? Wakati wazalendo wanalalamikia hii mikataba ya kifisadi nyie si mlikuwa mnakula pamoja na wezi wenzenu. Kwa nini sasa msikae pamoja mmalize tofauti zenu badala ya kutuingiza wananchi kwenye mipango yenu ya wizi...wapuuzi sana ninyi!
 
jambo la msingi bunge limsaidie rais kwa kuomba mikataba yote ipitiwe upya. pia bunge liache tabia ya kupitisha mambo kwa hati ya dharura. pia bunge liwanyang'anye vyeo vya bunge watu wote waliohusika kupitisha mikataba hii ya kimangungo .pia bunge lipendekeze kuvua kinga viongozi wastaafu walioliingoza taifa katika mikataba mibovu. vinginevyo waache vigelegele vya kimsifu rais kinafiki.
....Umeongea vema but wenzio haya ndiyo hawapendi kuyasikia kabisa, watakuambia wewe siyo mzalendo.
 
Back
Top Bottom