Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais Magufuli asitufanye wote wajinga, jipya ni kujenga uwanja na mbuga Chato

Kosa kingine kwa Tundu lissu
Lissu hatakiwi kumshambulia Magufuli
Lissu anatakiwa atuambie atafanya Nini,kukomaa na Magufuli ni sawa na kuzidi kujipunguzia kura tu
Hivi kujenga hospital kubwa 69 sio maajabu
Kukarabati shule za sekondari ambazo haziguswa toka mkoloni si maajabu
Chadema mjipange sana na lissu wenu mtajikuta mmeishiwa maneno baada ya wiki moja tu toka kuanza kampeni
Kuna mahali mna kosea.. Nimesoma enzi za Mwalimu JK na kumaliza kipindi cha Mwinyi chuo. Kwa taarifa yenu nyie vijana, tulikuwa tuna tumia dawati moja watu wawili. Na tuna kula shule. Mwalimu wakati huo hakuwahi kuchimba madini. Tulisomwshwa na kahawa, katani, pamba na korosho. Utalii haukuwepo, madini hayakuchimbwa na wazazi wetu hawaku lipishwa ada zetu. Vyuoni na sekondari tukisafirishwa na serikali. Kwa kitu walivho kiita warrant.
Vyuoni tulipewa hadi sabuni za kufua na kuogea. Juu ya hayo tulipewa na allowances kila mwezi.
Leo kuna madini, kuna watalii mnajidai kuna ndege ambapo hata mimi nilipanda ndege wakati wa Mwalimu tena kwa warrant bado watoto hawana madawati, wanakaachini, hakuna madarasa wanakaa chinibya miti. Vyuo hamuwapi pesa japo ni mikopo. Bado mnawanyanyasa nayo. Hakuna ajira. Na mnawakebehi wasitegemee ajira wakati nyie mnapeana ajira kichama.. Hebu tuache ushabiki wa kujaza matumbo ya famila.. Tuwaze kukitumikia Taifa la Tanzania. Mahali JPM amekosea mwambieni alikosea, huo ndio uzalendo.. Sio kumpamba uongo..
 
Kwa hiyo na Lisu nae ni Mchaga?
Lol watetezi wa CCM bana?
Ni kwa sababu akiwa rais Singida wasahau maendeleo, na kwa sababu chadema iko dominated na kaskazini, tutegemee hilo.

Mwambieni aendelee kutaja maajabu yote yaliyofanyika nchi hii kwenye awamu hii, asichague maajabu.

Vinginevyo ataonekana anabagua baadhi ya maeneo.
 
Acha chato nayo ikuwe kiongozi jasiri alitoka pale, Pakinoga Sana hamia name familia maana hiinchi yeti unaruhusa y'all kuishi popote upapendapo blaza..
Hizi ndio hoja za kijinga kabisa,nchi inaongozwa na kujengwa kwa mipango,hatujengi kwa kuwa kiongozi fulani anatoke huko.Mjinga sana wewe.

Nchi huwa ina mipango ya maendeleo,Chato haikuwa na mpango wa kujenga Uwanja wa ndege. Kuna mipango mingine kwa Chato Kama sehemu ya Tanzania lakini sio Uwanja.Amka wewe Mtz.
 
Hiyo mbuga inapakana na Rwanda kapeleka wanyama pori ili wakizaliana wengine wavuke boda angalau ndugu zake wapate vivutio vya utalii amka Mtanzania asili.
Hifadhi ya chato ilikuako tangu enzi za nyerere kilichofanyika ni kupandisha hadhi kuwa mbuga ili kuongeza nguvu ya uhifadhi.
Kila hatua ya hifadhi ina kiwango maalum cha kuipa rasilimali na matumizi yake yameainishwa
 
Wengine waliwaweka wanawe kuwa meneja wa kampeni...naxwengine walikua na ndg Ao sehem nyingine ila mitandao na majukwaa ya kushea taarifa haikuwa inapatika km sasa
Katika Marais wote waliotangulia hakuna Rais aliyemuweka mpwa wake kuwa Paymaster General. Haya ndiyo mapya ya utawala wa awamu ya tano.
 
Hizi ndio hoja za kijinga kabisa,nchi inaongozwa na kujengwa kwa mipango,hatujengi kwa kuwa kiongozi fulani anatoke huko.Mjinga sana wewe.

Nchi huwa ina mipango ya maendeleo,Chato haikuwa na mpango wa kujenga Uwanja wa ndege. Kuna mipango mingine kwa Chato Kama sehemu ya Tanzania lakini sio Uwanja.Amka wewe Mtz.
Hahahaa unapanic Kama umeshikwa pabaya... Kujengwa uwanja Chato mipango yote yanchi inakuwa imeharibika? Wewe unajua kujenga nchi kitaalamu kuliko serikali hii?? Mjinga asiyejijua Kuwa mjinga ni mpumbavu...pole!
 
Nimemsikiliza Tundu Lissu.. Yuko very outdated.. Mawazo yake ni ya mwaka 47. Tanzania imesha move km 10,000 mbele kutoka mahali ambapo Lissu amesimamia.
Lissu hana hulka ya uraisi.. Amekaa kiuana harakati.. Katika hotuba yake ameishia kubeza na kulaumu tu bila kutoa suluhisho.. Ameonesha kuyajua matatizo ya wananchi ila hajaonesha kuwa ana suluhisho hata moja la matatizo hayo.
Kwa sera hizi mfu na dhaifu, Tundu Lissu akipata hata kura laki tano kwenye uchaguzi huu, ashukuru Mungu.
 
Hayo siyo maajabu!
Mataga Bwana sijui wakoje:-

Lissu ametaja maajabu aliyofanya magufuli ni :-

1. Kujenga Mbuga ya wanyama Burigi Chato hilo ndio jipya halijawahi kufanywa na watangulizi wake.

2. Kujenga Uwanja wa ndege Chato maana hakuna hata rais aliyepita zaidi yake aliyejenga uwanja wa ndege kwao.

3. Kudhalilisha wanawake,wasichana,mabinti,wamama,shangazi,mabibi tena hadharani ,hayo hayajawahi "kufaniziwa" na watangulizi wake.

Nyongeza nyingine:-

4. Kununua Midege na manunuzi hewa bila kupitishwa na bunge.

5.Kutopandisha mishahara kwa miaka mi5 ya wafanyakazi wa umma.

6.Japo alipunguza wafanyakazi hewa ,mishahara hewa , warsha,semina ,makongamano lakini Malipo ya mishahara katika awamu yake ni makubwa kuliko hapo nyuma ambapo kulikuwa na vyote alivyoviondoa.

7. Kazuia matibabu nje lakini awamu yake ndio inayoongoza kwa gharama za matumizi ya matibabu ya viongozo nje.


Mambo ni mengi sana hayo ni machache ngoja kampeni zianze kwanza.
 
Sa chato kumekua ulaya mbona ni pa kawaida tu au na flyover imejengwa chato
Uwanja wa ndege wa kimataifa, mbuga mpya za wanyama, taa za barabarani zikiongoza punda, upendeleo kwenye miradi yote umeme, maji, barabara, afya, etc. Huu ni udhaifu mkubwa wa magu na ni kinyume na maadili ya uongozi.
 
Tundu Lissu akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi wasio na itikadi ya chama chochote mkoani Dodoma ametoa hoja kali ambazo CCM hawana uwezo wa kuzijibu zaidi ya kupanic na kukimbilia kwenye vyombo vya habari viwahurumie wasirushe mikutano ya Tundu Lissu.

Mosi, amezungumza kuwa jipya na la ajabu kwenye utawala huu ni Rais kujenga uwanja mkubwa Chato wakati marais waliopita hawakufanya maajabu haya, amesisitiza Tundu Lissu.

Pili, ni kitendo cha Rais kupeleka mbuga Chato. Hili ni ajabu kuu ambalo halijawahi kufanyika amesisitiza Tundu Lissu.

Tatu, Lissu amesisitiza kuwa watu wamedhalilishwa, hasa viongozi wa serikali na akina Mama kwa kauli chafu zinazotolewa.

Lissu amesisitiza hii nchi sio kila mtu ni mjinga na unaweza kuwadanganya kirahisi. Kuna watu werevu na wanakwenda kuwaambia wananchi kwa miaka mitano madudu yaliyofanyika.

Je, haya maajabu ni kweli yamefanyika huko Chato?

Je,wakazi wa Lindi, Dodoma, Mbeya, Ruvuma, Arusha, Mtwara, Kilimanjaro mnafahamu maajabu haya ya huko Chato?

Kwa hoja hizi ambazo hata mimi sikuzijua kwa miaka mitano, sasa nimeamshwa usingizini.

Hoja haipigwi rungu, bali hujibiwa kwa hoja. Hii ni kauli ya Dkt Jakaya Kikwete

CCM oyeee oyeeee oyeeee, jibuni hoja hizo!

Vyama vyote vya upinzani vilianza kwa siasa za namna hii tangu 1995, siasa za kutembea na issues za kuhamasisha chuki dhidi ya watawala na ccm hazikuwahi kufanikiwa lkn bado hawajifunzi. Chadema naiona ikipa anguko la karne uchaguzi huu. Binafsi hizi hoja za Lissu zimenitia kichefuchefu, ni mtaji kwa JPM sababu ni upuuzi kujifanya uoni alichokifanya wakati dunia yote inaona, mfano jinsi alivyoshughulikia corona bila kutumia sayansi.
 
Hili la ujenzi wa Airport Chato hata Mimi sikuwa na taarifa zake labda lilikuwa katika Ilani ya uchaguzi ya CCM.

Kuhusu mbuga ya Wanyama sidhani kama ni kweli TANAPA watatueleza vizuri Sisi tunajua zipo hifadhi za Ruha,Tarangire,Manyara,Serengeti..... Hii Mbuga ya Chato ilizaliwa lini na mpaka sasa watalii wangapi wameshaitembelea.

Haya mambo yalifanywa Mobutu Kuku Wazabanga Ngedu miongo mingi iliyopita kamwe haiwezekani kufanywa na kiongozi wa karne hii.Lissu anatudanganya mchana kweupe.
 
Mwambieni hapo sasa ameanza kufanya siasa kwa mbaali. Na hizo ndizo hoja za kisiasa sio kutusimulia juu ya yeye kupigwa risasi kwakua hayataleta maji pale kijijini kwetu Cherenganya au kule umamani Kiambankumbe
 
Nilisha wahi kuwashauri chadema humu kumshambulia magufuri hakuta wasaidia kwenye Sanduku la Kula Kwa kuwa magu kajenga ukaribu Sana na watu wa kipato cha chini na ndio wapiga Kula walio wengi ni lazima chadema iwe na njia mbadala kwenye compeni zake kama Wana Nia ya kuongoza
 
Yaani ajenge nchi aache kujenga Chato,?hayo majengo aliyojenga siyo yake binafsi,Hayati Nyerere hakujenga tulimcheka,Hayati Mkapa kazikwa juzi tumesema hakujenga kwao,Kikwete baba wa watu hakuwa na makuu lakini tulisema anazurura sana hadi tukahesabu safari zake humuhumu Jf,Chato hapajajengwa kwa Siri,nasidhani kama Kuna kilichoandikwa jina la Magu huko,wapinzani ni vizuri kujitathmini upyaa,maendeleo aliyoleta Magufuli ni makubwa a mbayo hata 2015 niliyotegemea Lowassa ashinde ayalete Magufuli kamzidi parefu,sisi wenyewe tunajua hata ukitaka kujenga kanyumba kakuishi,lazima ufunge mkanda kidogo,kwa hoja hizi Lisu kushinda ni ngumu,inaonekana hakujipanga vyema yupo too emotional than logical.

Hizo fedha za ujenzi wa Airport zilipitishwa na bunge lipi.
 
Back
Top Bottom