Tundu Lissu, ndani ya Star TV katika Medani za Kisiasa na mstakabali wa Siasa za Upinzani

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Hallow wana JF,

Mbunge wa Singida mashariki mh. Tundu Lissu ni mgeni mualikwa ndani ya kipindi cha medani za kisiasa akijaribu kudadafua mwelekeo wa Upinzani na siasa za chama tawala.

Pia atazungumzia dhana nziama ya kujilinda ambayo inapigiwa kelele na CCM na msajili wa vyama bwana Tendwa.

Tindu Lissu anawatahadharisha ccm hawajawahi kupata upinzani mkali kama wa cdm zaidi ya miaka 50 tangia uhuru,mfano uchaguzi wa Arusha ambao ccm wote mawaziri,nwabunge isipokuwa Raisi tu walikuja kwenye kampeni za uchaguzi wa kata tu,anasema CUF wamo msafara mmoja na CCM

Anasema kuna wakati quantitative change inabadilika kuwa qualitative change.

Anasema CUF ni chama cha Zanzibar, na ngome yao ya kisiasa ipo huko. hawajawahi hata kufikisha zaidi ya wabunge watatu bara.

Anasema kama unataka kushinda uchaguzi wa nchi hii huitaji kwenda Zanzibar

chadema ni chama pekee cha upinzani katika historia ya vyama vingi kushinda viti vingi.

Anasema nguvu yao ya hoja bungeni ndio iliwafanya watake kufunga matangazo live bungeni.

Yupo live ana elezea uhalali wa Red Guard
"tunajilinda kwasababu tuna akili"

Sheria ya Tanzania inasema tuna haki ya kujuilinda

Dunia nzima nchi inaendeshwa kwa kodi si michango,
Kwa mujibu wa sheria zetu hakuna michango,hivyo haikagiliwi na kutoa mwanya kwa walafi kuila.
Kwenye jimbo lake hakuna michango

Anamalizia kwa kuwatahadharisha waliopo madarakani
"Tumekaribia ngome"

Lissu: Cuf ni chama cha zanzibar.


Akizungumza na ktk kipindi cha medani za siasa cha Star tv Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chadema Lissu Tundu Antipasi alisema cuf ni chama cha zanzibar ndiyo maana wana wabunge wengi toka zanzibari huku alisema haihitaji elimu ya universit kutambua kwamba cuf ni chama cha zanzibari...

Amesema Cuf hakijawahi kuwa na wabunge hata wa tatu huku bara tangu 1995!
Huwa wanaishia kupata mbunge mmoja au wawili kama ilivyo sasa..

Kuhusu wao kutokuwa na mbunge wa kuchaguliwa znz alisema, si lazma kuwa na mbunge kwa kuwa kuna siku watashinda.. kuhusu kura za urais za zanzibar alisema kura laki 5 si muhimu.. Kwani hata ubugo tu kuna kura milioni 2..
 
Habari wakuu?
wapenda haki, amani, usawa na ukombozi
1. fungulia startv sasa kamanda Tundu Lissu yupo recorded akizungumzia maswali mbalimbali ya kisiasa na sasa ndio anaanza

2. jioni tukumbuke kwenda mabibo mwisho kwenye mkutano mkubwa sana wa chadema juu ya rasmi ya katiba.
 
Mh tundu yupo ndani ya star tv kwenye Medani za siasa na uchumi kama una mda tune in ili tusiulizane
 
Yupo live ana elezea uhalali wa Red Guard
"tunajilinda kwasababu tuna akili"

Sheria ya Tanzania inasema tuna haki ya kujuilinda

Dunia nzima nchi inaendeshwa kwa kodi si michango,
Kwa mujibu wa sheria zetu hakuna michango,hivyo haikagiliwi na kutoa mwanya kwa walafi kuila.
Kwenye jimbo lake hakuna michango

Anamalizia kwa kuwatahadharisha waliopo madarakani
"Tumekaribia ngome"
 
..Huyu dada bado sana. Hata Red Brigade haijui!? Eti ni Red Guard!
 
Anatokwa povu kwamba wanaruhusiwa kutumia nguvu kujilinda, huu si ndio ugaidi wenyewe huu
 
Back
Top Bottom