Uchaguzi 2020 Tundu Lissu na upotoshaji kuhusu vitendo vya Ushoga Tanzania

kipande

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
2,136
1,318
Mgombea Urais wa Tanzania jwa tiketi ya CHADEMA, Tundu Lissu alikutana na waandishi wa habari jijini Arusha na kuelezea msimamo wake kuhusu vitendo vya ushoga nchini.

Katika majibu yake kwa waandishi wa habari alipokuwa akijibu swali lililomuhusisha yeye kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja yaani vitendo vya ushoga, Tundu Lissu alisema Katiba ya Tanzania inatamka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa faragha yake.

Tundu Lissu alienda mbali zaidi na kusema maisha ya chumbani ya mke na mume au na yeyote yule ni marufuku kwa Serikali kuchungulia.

Kwa tafsiri ya jumla hapa ni kuwa Tundu Lissu anaunga mkono vitendo vya ushoga au mapenzi ya jinsia moja. Kwa nini nasema hivi?

Kwa sababu katika maelezo yake Tundu Lissu ametumia neno "...au na yeyote yule..." Maana yake ni kuwa hata wanaume kwa wanaume au wanawake kwa wanawake wakiwa kwenye hii faragha basi kwa Lissu ni sawa tu.

Lakini je ni kweli Katiba ibakubaliana na haya aliyosema Lissu au ni upotoshaji?

Tukisoma ibara ya 16 ibara ndogo ya kwanza [16(1)] ya Katiba inaeleza kama ifuatavyo:

16.-(1) Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake naunyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na
mawasiliano yake ya binafsi.

Ibara hii ya Katiba ndiyo aliyotumia Tundu Lissu kupotosha umma wa watanzania kwa malengo yake binafsi labda na ya wafadhili wake.

Katiba haikuishia hapa kufafanua juu ya utaratibu wa faragha za watu pasina kuingiliwa, hili limeelezwa kwenye ibara hiyo ya 16 ibara ndogo ya pili [16(2)]. Ibara hii ya pili imezungumzia kuhusu hali, namna na kiasi ambacho faragha au kujamiiana kunavyoweza kuchukua nafasi, kama inavyoeleza:

*16:-(2) Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali,namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.*

Hapa ndipo alipopotosha Tundu Lissu ama kwa makusudi ama ka kutojua tafsiri ya maneno hali, namna na kiasi kama yalivyoelezwa kwenye Katiba.

Ukisoma kwa makini unaona Katiba ilivyoweka wazi juu ya utaratibu wa hizo faragha na si mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzie au mwanamke kufanya na mwanamke mwenzie.

Hapa naomba niliweke sawa hili suala la hali, namna na kiasi lililoelezwa kwenye Katiba.

Inapozungumzwa neno 'hali na namna' ni kwamba katika hali na namna ya 'kawaida ya maumbile ya binadamu' inategemewa kwamba tendo la ndoa au kujamiiana kufanyika baina ya mwanaume mtu mzima na mwanamke mtu mzima kwa mwanaume kukutana kimwili na mwanamke kwa njia za kawaida zilizo maalumu kwa ajili ya tendo la ndoa au kujaamiina kwa maana ya uume na uke na si kwa kutumia njia ya haja kubwa yaani kinyume na maumbile.

Katika kuondoa vitendo hivi visivyo na maadili nchini *Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kifungu cha 154* kimeeleza:

154.-(1) Mtu yeyote ambaye-

(a) anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au,
(b) anamuingilia mnyama kimwili au
(c) anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile,

atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha
na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini.

(2) Ikiwa kosa limetendwa chini ya kifungu kidogo cha (1) cha
kifungu hiki dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika
kwa adhabu ya kifungo cha maisha.

Na katika kutilia mkazo maneno hali, namna na kiasi ambacho faragha itafanyika ibara ya 9 ya Katiba kifungu 'b' kinaipa nguvu Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kwa watakaofanya mapenzi kinyume na maumbile kwa kueleza ifuatavyo:

*9 (b) Kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa.*

Maana ya kifungu hiki 'b' katika ibara ya 9 ya Katiba ni kwamba Kanuni ya Adhabu sura ya 16 ni miongoni mwa sheria zinazolindwa na kutekelezwa kwa mujibu wa Katiba.

Inawezekana Tundu Lissu hafahamu maana ya maneno hali, namna na kiasi au anapotosha kwa makusudi sheria za nchi.

Kwa mfano, mtoto akizaliwa kwa kuanza na kichwa tunasema amezaliwa katika hali na namna ya kawaida akizaliwa kwa kuanza kutoa miguu huyu huelezwa kuwa amezaliwa katika hali isiyo ya kawaida. Vivyo hivyo tendo la kujaamiiana linapoelezwa kwenye Katiba kufanyika katika hali, namna na kiasi cha kawaida inamaanisha kuwa litafanyika kwa mwanaume kujamiiana na mwanamke kwa kutumia njia za kawaida za maumbile na si kutumia njia ya haja kubwa ambayo ni kinyume na maumbile ya mwanadamu au wanaume kujamiiana kwa wanaume hii ni kinyume na sheria. Tundu Lissu hajui haya?

Hivyo basi, kwa mujibu wa Katiba, maneno hali, namna na kiasi yanamaanisha mwanaume kujamiiana na mwanamke katika hali na namna ya kawaida na si mwanaume kumuingilia mwanamke kinyume na maumbile na pia si kwa mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzie au mwanamke kukutana na mwanamke mwenzake.

Kitendo cha Tundu Lissu kusema mtu yeyote anaweza akafanya tendo la kujamiiana au faragha na mtu mwingine yeyote yaani hata wanaume kwa wanaume ni kuunga mkono vitendo vya mapenzi ya jinsia moja au vitendo vya ushoga jambo ambalo ni kinyume na Katiba.

Na ikumbukwe wazi kuwa Kanuni ya Adhabu sura ya 16 imezungumzia vitendo ndiyo maana imetumia neno "anamuingilia" na "anamruhusu kumuingilia" hii inaonesha ni vitendo yaani mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzake au kuingiliwa.

Je mashoga hawaingiliwi na wanaume wenzao? Tundu Lissu anatetea nini hapo? Je ana ajenda gani ya siri katika hili la vitendo vya mapenzi ya jinsia moja?

Kimsingi Tundu Lissu ana lengo la kupotosha umma ili vitendo vya ushoga na usagaji vionekane vya kawaida Tanzania ndiyo maana anaita sheria kama hii inayozuia vitendo hivi haramu vya ushoga kuwa ni sheria kandamizi.

Hili lilidhihirika wazi wakati Tundu Lissu alipofanya mahojiano na Stephen Sackur wa BBC katika kipindi cha 'Hard Talk' pale alipoulizwa endapo ikitokea amechaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ataruhusu vitendo vya ushoga?

Bila ya aibu Tundu Lissu alisema yeye hatoingilia faragha za watu jibu ambalo amelitoa pia kwa waandishi wa habari kule Arusha.

Maana yake ni kuwa yeye Tundu Lissu yupo tayari kuacha vitendo vya ushoga vitapakae nchini jambo ambalo ni kinyume na maadili ya Mtanzania.

Katika kuonesha dhamira ya kuendeleza vitendo vya ushoga nchini, Ilani ya CHADEMA katika ukurasa wa 17 imeweka neno "uhuru wa faragha" ambalo Tundu Lissu alilitetea alipohojiwa BBC.

Na pia katika kuhakikisha sheria inayozuia vitendo vya ushoga ambayo Tundu Lissu anaona ni sheria kandamizi ilani ya CHADEMA katika ukurasa wa 15 imeweka mkakati wa kuifuta sheria hii inayozuia vitendo vya ushoga kwa kueleza kama ifuatavyo katika kipengele 'a':

a. Kutekeleza mikataba ya Kimataifa ya Haki za Binadamu itakayoridhiwa na Bunge na kufuta sheria zote za ndani zinazokandamiza haki za Binadamu.

Kwa Tundu Lissu suala la vitendo vya ushoga yaani mwanaume kumuingilia mwanaume mwenzie au kuingiliwa kinyume na maumbile kwake ni haki za binadamu ndiyo maana imekuwa sehemu ya kauli mbiu zake. Lakini haki hii anayotaka Tundu Lissu ya vitendo vya ushoga au mapenzi ya jinsia moja ni sahihi kwetu watanzania?

Vitendo vya ushoga ni haki ya binadamu kwa nchi kama Ubelgiji alikoishi au Marekani alikoenda au hata Uingereza alikofanya mahojiano na BBC lakini si Tanzania ambako tuna mila, desturi, tamaduni na miiko yetu ambayo inakataza mapenzi ya jinsia moja.

Ukitazama kwa makini kwa nini Tundu Lissu anapigania hili la mapenzi ya jinsia moja utagundua kuwa Ilani ya CHADEMA ni zao la mkakati wake wa kurasimisha vitendo vya ushoga nchini.

Hapa ndipo unapata maswali ya majibu ya kwa nini nchi kama Ubelgiji na Marekani zinaufuatilia sana uchaguzi wa Tanzania. Wanajaribu kuona namna gani mpango wao wa mapenzi ya jinsia moja yanafanikiwa Tanzania kwa kivuli cha neno haki.

Hii ni aibu kwa nchi yetu inayoheshimika.
 
Right to privacy mara nyingi Inakuwa katika maswala ya mawasiliano ndio maana huko mbele wenzetu wameangalia namna ya kuweka mipaka ya udukuaji wa mawasiliano ya watu.

Mwanasheria nguli kwakua amevuta mpunga wa mabeberu kwa maelekezo ya kusambaza agenda za ufirauni basi lazima apindishe maneno ili yafit vyema katika lengo lake akiwa na imani kuwa sio wengi wanasoma na kwakua wanamuamini hata akidanganya hakuna atayeshtuka.
 
Screenshot_20201002-025552.png

_104172054_capture.jpg
 
Right to privacy mara nyingi Inakuwa katika maswala ya mawasiliano ndio maana huko mbele wenzetu wameangalia namna ya kuweka mipaka ya udukuaji wa mawasiliano ya watu.

Mwanasheria nguli kwakua amevuta mpunga wa mabeberu kwa maelekezo ya kusambaza agenda za ufirauni basi lazima apindishe maneno ili yafit vyema katika lengo lake akiwa na imani kuwa sio wengi wanasoma na kwakua wanamuamini hata akidanganya hakuna atayeshtuka.
Mmekosa hoja ya maana ya kumkabili Lissu, sasa mnaokoteza vihoja vya mtaani, ambavyo ni very cheap. Wewe ukiamua kupumuliwa nenda kapumuliwe tuu, mbona pale mjengoni kuna wazito wanapakatwa kiroho safi tuu?
 
Umeandika ujinga. Hiyo ibara iko very clear wala haiitaji mambo mengi kufafanuliwa, na isitoshe pia nyie ndio mlioapa kuilinda nakuitunza katiba sasa kama mnaona hicho kipengele kinatumika isivyo stahili si mbadilishe serikali iwe inauwezo wakuchungulia ndani vyumbani mwa watu.

Swala la kujaamiana ni mambo yanayofanyika sirini kwahiyo swala la ushoga,usagaji,ulawiti linakua kosa likifika hadharani na sheria za nchi ziko wazi kwenye hilo.

Hoja ya Lissu imejikita kwenye faragha na hapa ndipo msingi wa hiyo ibara ulipo. Sasa wewe kinachokushinda kuelewa ni nini.
 
Rejea mada kuu ambapo umewekewa kifungu cha Sheria.

Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kifungu cha 154.
(1) Mtu yeyote ambaye-
(a) anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au,
(b) anamuingilia mnyama kimwili au
(c) anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile,

atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini.

(2) Ikiwa kosa limetendwa chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha.
Kama sheria ipo, sasa hofu ni nini? Watakaofanya ushoga watashtakiwa. Vitu vingine havihitaji hata mijadala
 
Back
Top Bottom