Tundu Lissu na Membe waende NCCR-Mageuzi ili kuwa na chama kingine cha upinzani hawa CHADEMA na ACT-WAZALENDO wanatuchanganya tu

Dr Shekilango

Senior Member
Dec 30, 2013
192
117
Imeonekana NCCR-Mageuzi ndiyo chama pekee chenye kuamua kwa niaba ya Taifa. Kwa siasa za chama kile za kidiplomasia na za kipadre ni wazi hatuwezi kuwa na vyama vya harakati ngumu kwa mazingira ya sasa!

Tunataka chama chenye Itikadi na falsafa unganishi na kinachotanguliza maslahi ya watu kwanza na Taifa, hivyo Tundu Lissu na Membe waende NCCR-Mageuzi ili kuwe na chama ambacho ndo kiasisi cha MAGEUZI ya kisiasa. Hawa CHADEMA na ACT-WAZALENDO wanatuchanganya tu.
 
Chadema wamefanya lipi la kukushangaza?
Imeonekana NCCR-Mageuzi ndiyo chama pekee chenye kuamua kwa niyaba ya Taifa. Kwa siasa za chama kile za kidiplomasia na za kipadre ni wazi hatuwezi kuwa na vyama vya harakati ngumu kwa mazingira ya sasa!...
 
CHADEMA ni brand, hata kama mtalazimisha vyama vingine, ifahamike CHADEMA ndio iko mioyoni mwa wengi wenye mitazamo ya kipinzani.

Namna pekee labda ni kuifuta CHADEMA, lakini hakuna uwezekano wa chama kingine kukua na kukizidi cdm kwa kizazi hiki. Tiss wana mpango wa kuanzisha chama kingine cha siasa, lakini hawatakuwa na uwezo wowote wa kufanya chama hicho kikubalike kama kilivyo CHADEMA.

Halafu Membe sio mpinzani, ni mzee muhuni toka ccm aliyepoteza ramani.
 
Imeonekana NCCR-Mageuzi ndiyo chama pekee chenye kuamua kwa niyaba ya Taifa. Kwa siasa za chama kile za kidiplomasia na za kipadre ni wazi hatuwezi kuwa na vyama vya harakati ngumu kwa mazingira ya sasa!..
Mkuu kuna VIRUS katika vyama vya siasa,jawabu ni kuondoa virus kwa vyama vyote na kwa pammoja na dawa ni katiba mpya.
 
Imeonekana NCCR-Mageuzi ndiyo chama pekee chenye kuamua kwa niyaba ya Taifa. Kwa siasa za chama kile za kidiplomasia na za kipadre ni wazi hatuwezi kuwa na vyama vya harakati ngumu kwa mazingira ya sasa!..
NCCR Mageuzi eti ndio chama cha kuamua kwa niaba ya taifa. Man are you serious?

Yaani wakajimalize kisiasa kama Mbatia?
 
Back
Top Bottom