Tundu Lissu kutetewa na mawakili 17, aongea neno baada ya kuachiwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Kesi ya maneno ya kuuzi yanayodaiwa na watawala, inayomkabili Tundu Lissu.anatetewa na mawakili kumi na saba (17) akiwemo john maly peter kibatala nk
13524414_1038708339546977_8966361714285263622_n.jpg

Jopo la wanasheria 17 wakiongozwa na wakili wa mahakama kuu kijana zaidi John Mallya na Peter Kibatala, tayari wapo mahakamani kumtetea Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutoa kauli za kuudhi na kichochezi.
13567378_202833703450562_4520922414317893845_n.jpg

Tundu Lissu akiwa Mahakamani. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana, kesi yake yaahirishwa hadi Agosti 2.
4a6914e6-99e8-4ac2-abea-95233c5d9b1f.jpg

Baada ya Kutoka Mahakamani aliongea na waandishi wa habari
 
Kesi ya maneno ya kuuzi yanayodaiwa na watawala, inayomkabili Tundu Lissu.anatetewa na mawakili kumi na saba (17) akiwemo john maly peter kibatala nk
View attachment 361520
Jopo la wanasheria 17 wakiongozwa na wakili wa mahakama kuu kijana zaidi John Mallya na Peter Kibatala, tayari wapo mahakamani kumtetea Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu, ambaye anashtakiwa kwa kosa la kutoa kauli za kuudhi na kichochezi.
View attachment 361521
Tundu Lissu akiwa Mahakamani. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana, kesi yake yaahirishwa hadi Agosti 2.
Huo ni mshikamano mzuri. Kitaeleweka tu.
 
Leo naona kidomodomo kimemwisha baada ya kudhaminiwa tu katoka mkuku hakuongea utumbo wake na vyombo vya habari.Kajua akiropoka tu anadakwa anawekwa ndani mpaka jumatatu.Leo katii sheria bila shuruti.
Ulikuwepo au umehadisiwa tu!? Mbona amezungumza na amemtaka huyo anajihisi yeye ndiye alieambiwa ni dikteta uchwara aende mahakamani kuthibisha kuwa si dikteta uchwara.
 
LIVE TOKA MAHAKAMA KISUTU

Anaandika YERICKO

Tupo mahakamani, tayari Mh Lissu ameshaletwa Mahakamani,

Lissu anatetewa na wanasheria 17 wakiongozwa na John Mallya Peter Kibatala na timu nyingine toka makao makao makuu ya Chama.

Viongozi wote wa makao makuu wameshawasili,

Tunasubiri Hakimu tu aingie kwenye ukumbi wa mahakama...

UPDATES,

Tayari Hakimu Mh Jongoro anayesikiliza shauri ameshawasili, sasa ni utambulisho wa mawakili wa pande zote,

Kesi inaanza kusomwa,

Mwendesha mashitaka: Tundu Lisu anashitakiwa kwa makosa ya uchochezi, mnamo tarehe 28/06/2016 akiwa eneo la mahakama kwania ya kudhalau umma dhidi ya mamlaka yao walioyoichagua kihalali, alisema huyu dikteta uchwara lazima tumpinge kila kona"

Hakimu: Mshitakiwa, unakubali au unakataa?

Lissu: nakataa yote

Mwendesha mashitaka: Mh Hakimu ushahidi wa shauri hili umekamilika, tunaomba tarehe ya kuanza usikilizwa,

Hakimu: Mawakili wa utete mnalololote la kusema?

Wakili: Mheshimiwa kwamjibu wa kifungu cha sheria na.... Mshitakiwa kosa aliloshitakiwa linadhaminika, hapa tunao wadhamini na zaidi mshitakiwa ni mbunge na mwanasheria wa chama, hivyo anadhaminika, na zaidi mshitakiwa aliliripoti mwenyewe mbele ya polisi baada ya kuitwa tu kwa simu. Ni hayo tu mh

Mwendesha mashitaka: Mshitakiwa aliyembele yako, mnamo tarehe 28 mwenzi huuhuu alifikishwa mahakamani kwa kosa...... Aaah nimesahau sina nakala ya mashitaka, na wenzake watatu na kudhaminiwa. Hivyo akatenda kosa hili, huyu ana nidhamu mbovu, ameona kutenda kosa ni kawaida,

Hakimu: Kwanini unamhukumu kwa kosa ambalo mahakama hii haikumtia hatiani...na siajabu akitoka hapa atatenda kosa tena....

Wakili: Mh hakimu nashindwa kujua huyu wakili wa serikali anajipa kazi ya hukumu kwa kesi iliyopo mahakamani, nimshauri arudi kwenye kesi iliyopo mezani kwakuwa kesi ya nyuma ni tuhuma tu na sio hukumu inayoweza kutumika kama kielekezo hapa.

Mwanasheria: Mh huyu mtuhumiwa ni mzoefu wa kutenda makosa...... Watu wanaangua kicheko kwa kwa kwa...

Hakimu..... Wakili

Wakili: Kwanza Mh hakimu naomba ifahamike kwamba upande wa serikali wamekubali kuwa suala la dhamani liko wazi, hili liweke katika kumbukumbu... Haya anayoyaleta sasa huyu mwanasheria hayana msingi, kwani kwa mjibu wa vifungu vya sheria na.....na... Vinampa haki yakupata dhamana, izingatiwe kuwa katika dhamana ya kesi ya mwanzo hakukuwa na mashariti ya mtuhumiwa kutotoa maoni ama kutenda kosa nje ya lile.. Izingatiwe kuwa sababu za kukidhi dhamana tumeshazitoa

Hakimu: Mahakama inaamua kuwa mtuhumiwa apewe dhamana, wadhamini wa mtyhumiwa waje mbele...kuhakiki nyaraka zao

Mwanasheria: Anainuka... Mh Hakimu...

Hakimu: Mwanasheria tambua sehemu iliyosalia ni maamuzi ya mahakama, hivyo wadhamini njooni mbele.....

Kesi itatajwa tarehe 2/8/2016
 
Tunatangaza kulinda/kujenga amani huku tunafarakana bungeni,tunatishiana mitaani,tunaitana majina Mara malofa,mavilaza,dikt. uchwara...gharama za maisha zinapaa,elimu inachechemea!!! Ukifikiri sawasawa we are heading to no good!!
watu makini hutofautiana kwenye mambo ya kimsingi na hukaa na kuyachambua kitaalamu ili kuafikiana AMA kukubali kutokukubaliana kamwe hawawekeani visasi na kuvutana kwa mambo yaso na tija kwa taifa. Lazima tukumbuke NOBODY KNOWS EVERYTHING BUT EVERYBODY KNOWS SOMETHING.
 
Back
Top Bottom