Tundu Lissu kushtakiwa Mahakama ya Kimataifa kutokana na mahojiano aliyofanya na BBC

Cyprian Musiba ambaye ni mkurugenzi mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, leo kautaarifu umma kupitia wanasheria na mawakili maarufu hapa nchini wanakusudia kumfungulia mashtaka Tundu Lissu mahakamani hapa nchini lakini pia kuna mawakili wengine watakwenda katika mahakama ya kimataifa (The Hague) kupeleka kopi ya mashtaka dhidi ya Tundu Lissu.

Alikuwa akizungumza katika kipindi cha Focus on Africa kinachorushwa na BBC mwandishi aliyemuhoji anaitwa Victor Kenani wiki mbili zilizopita.

"Tundu Lissu alisema Tanzania kwa sasa ni nchi hatarishi kwa siasa pamoja na pamoja na wote wanaohoji utendaji wa Serikali. Akaongeza kusema watu wanauawa hovyo na wanatupwa baharini kwenye viroba. Tunataka atupe uthibitisho wa madai yake hayo ndani ya siku mbili zijazo kuanzia leo".

--------------
Kumbukizi: Mahojiano aliyofanya Tundu Lissu na BBC

Wow, I am good! Nilisema Lissu before kuwa Lissu kakipaka kwa kauli zisizo na uthibitisho.
 
Jina la Muaiba anataka kuliingiza Taifa kwenye matatizo kama jina lake kabisa hebu ajaribu kufunga mdomo wake ili angalao maneno ya Trump yasithidbite kuwa ni kweli
 
Hivi toka lini Lisu akaogopa mahakama na lini alikutwa na hatia?
Mkuu mimi si mpenzi wa siasa ila ulivyoa ndika niliposoma tu nikakumbuka "the law of averages" .Je watafute wastani amepelekwa mara ngapi mahakamani na ameshinda au ameshindwa mara ngapi then ,ikiwa law of average inaonyesha hushindwa watamshinda otherwise I am not a politician ila jibu wanalo it is not me it is the law of averages.Please note it is not me speaking it is the law of averages.
 
Think tank ya ccm imeishiwa maarifa!
Badala ya kufikiri jinsi ya kurejesha uchumi wa Tanzania kwenye hali ya kawaida,wanawaza uharo!Shame on you Cyprian
 
Lissu anapata faida gani kuiichafua nchi kwa kitu ambacho hakina ushahidi kua serikali imehusika.y asisubiri uchunguz ufanywe illi wahusika washtakiwe???? Mzalendo gan anaeichafua nchi bila ushahid na ni mwanasheria anajua kabsa ushahid ni kitu mhim katika kutoa hukumu???
Kwa kauli za lissu zisizosubiri uchunguz anawapa hata morali majambazi kuua watu maana watakua wanajua hata tukiua itasingiziwa serikali sio hao majambaz..
Watz tuwe makini sana na tutumie akili zetu vzur hakuna mtu amependa lissu kilichomkuta but asiseme vitu ambavyo bado havijatolewa majibu ya uchunguz
Wazalendo ni wale wanaotumia bunduki kufikisha hoja. Huyu Musiba kama hajatumwa na Sizonje basi katumwa na DAB maana hoja ni za kiwango cha umbumbumbu.
 
Sasa ndo nimemuelewa Mwalimu kwa hii kauli yake
 
Attachments

  • VID-20180115-WA0013.mp4
    649.4 KB · Views: 21
Takukuru imejaza watu mahabusu wengine wako huko zaidi ya Miezi 6 sababu ya ushahidi haujaatipatikana,kwani nini wasitafute kwanza ushahidi halafu wakishaupata ndio wapelekwe mahakamani?
Viongozi wa uwamsho kutoka zanzibar wapo jela sasa miaka mitano, serikali itupe huo ushahidi wa ugaidi huko mahakamani, kama kweli magaidi wahukumiwe. ..yaani hawa mawakili wanataka Kiki, ,waje tu the Hague natanguliza na mie hapo hapo case yangu ya uwamsho
 
Hilo jamaa kipindi lilipokuwa Channel ten nilikuwa naliona jitu la maana lakini kumbe ni shwain tu,
Inaonekana kabisa hata anavyoongea kuwa dhamira yake inamsuta na anajishtukia-shtukia kila mara...
 
Mtangazi na kiongozi wa Radio Free Africa bwana Cyprian Musiba ameamua kuacha kazi kutokana na issue ya maadili mara baada ya mahojiano ya Rc Makonda.

Kupitia ukurasa wake wa insta amebainisha hayo.
 
Musiba hahahahaaha eti haya mambo yalikuwepo tangu zamani sema hayakuwa yanasemwa huko nje,sasa huyu Lisu ndo anayasema hayo.

Huyu alipaswa awe ameshakamatwa na polisi kesho anasubiri apelekwe kisutu mahakamani
 
Cyprian Musiba ambaye ni mkurugenzi mkuu wa CZ Information & Media Consultant LTD, leo kautaarifu umma kupitia wanasheria na mawakili maarufu hapa nchini wanakusudia kumfungulia mashtaka Tundu Lissu mahakamani hapa nchini lakini pia kuna mawakili wengine watakwenda katika mahakama ya kimataifa (The Hague) kupeleka kopi ya mashtaka dhidi ya Tundu Lissu.

Alikuwa akizungumza katika kipindi cha Focus on Africa kinachorushwa na BBC mwandishi aliyemuhoji anaitwa Victor Kenani wiki mbili zilizopita.

"Tundu Lissu alisema Tanzania kwa sasa ni nchi hatarishi kwa siasa pamoja na pamoja na wote wanaohoji utendaji wa Serikali. Akaongeza kusema watu wanauawa hovyo na wanatupwa baharini kwenye viroba. Tunataka atupe uthibitisho wa madai yake hayo ndani ya siku mbili zijazo kuanzia leo".

--------------
Kumbukizi: Mahojiano aliyofanya Tundu Lissu na BBC

Musiba nafikiri atakuwa anaumwa lakini mwache aende mahakamani ila ajiandae pia na kutajiwa mtuhumiwa wa mauaji Daud Albert Bashite
 
Back
Top Bottom