Uchaguzi 2020 Tundu Lissu, Kura yangu umepata

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
13,226
26,048
Salamu kwako Tundu Antiphas Lissu, Shalom,

Leo napenda kukwambia rasmi kuwa , Kura yangu iko kwako! Na hii ndo sababu yangu kuu ya kukupa kura!

Katika maisha yangu nimekuwa nikifanya utafiti sana juu ya dhana ya umasikini wa watanzania na Tanzania kwa ujumla, Moja ya sababu ambayo niligundua kwenye utafiti wangu ni kuwa Tanzania tuna mfumo mbovu sana wa utawala ambao vyovyote vile hatuwezi kuendelea kwa mfumo huu!

Mfumo huu ninaousema ni mfumo kuwa fedha zote za watanzania zinakusanywa na kuwekwa chini ya mtu mmoja( raisi ambayo yeye ndo anayeamua kuwa hizo fedha zigawanywe kivipi)

Madhara ya mfumo huu ni kuwa umeondoa uwajibikaji kwa wananchi na viongozi, umeondoa ubunifu kwa wananchi na viongozi na mwisho umepelekea tabia ya ombaomba na unafiki kwa wananchi na viongozi

Mfumo huu pia umechochea ufisadi wa kiwango kikubwa sana kwa wananchi na viongozi na kama Kuna mtu anabisha Leo hii aniambie maisha ya ukwasi wanayoishi maraisi wastaafu yametokana na nini???

Hapa Tanzania hakuna raisi mstaafu mwenye maisha ya utajiri wa kuwaida. Wengi wana utajiri mkubwa wa real estate, kilimo kikubwa na hata pia makampuni makubwa ya uzalishaji. Na kibaya ni kuwa vyote hivi huwa wanavipata wakiwa maraisi. Sababu ya haya yote ni kuwa tumekuwa na mfumo wa kuziweka fedha zote za nchi chini ya mtu mmoja.

Leo hii raisi ni kama Mungu hapa Tanzania. Kila aendapo watu ni kulia shida, awafanyie hiki na awaletee hiki, haya yote ni kwa sababu ya mfumo mbovu tulionao ambao umeondoa uwajibikaji na ubunifu kwa watanzania na viongozi wetu

Kwa nini Mfumo wa Majimbo ndo suluhisho wa haya yote?

1. Mfumo wa majimbo utafanya hela zote zinazokusanywa kwenye sehemu husika zitumike kwa matakwa ya wananchi wa sehemu husika mf. Kujenga barabara , hospitali, shule bora na huduma bora za Maji na umeme!! Hili litafanya wananchi wasiwe wajinga kwa viongozi wao na kamwe was iwe ombaomba na watu wa kujipendekeza kwa viongozi wao.

2. Mfumo wa majimbo utachochea ubunifu kwa wananchi kufanya shughuli mbalimbali bora za uzalishaji ili majimbo yao yakusanye fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo yao.

Kama jimbo husika linategemea kilimo basi wananchi wa hilo jimbo watafanya kilimo bora na watakifanya cha biashara ili wapate mapato mazuri ya kuendeleza jimbo lao kimiundombinu na Pia kimaendeleo. Hakuna sehemu watu watalala au kuwa wazembe na watakuwa wakali kwa viongozi wao kuwahamasisha wawe agressive kwenye kubuni miradi bora ya maendeleo kwa maendeleo yao.

Mfumo huu utatengeneza wananchi wanaojiamini na Kuwajibika kweli katika kutunza rasilimali zao ili ziwasaidie wao na uzao wao. Wananchi hawatakuwa wazembe na watawawajibisha kweli viongozi wasio wabunifu kwenye kutengeneza vyanzo vya mapato kwa sababu watakuwa wanajua bila vyanzo vya mapato bora na vya uhakika kwenye maeneo yao basi watakuwa nyuma kimaendeleo na hawataweza kunsurvive.

Mfumo wa majimbo utafanya kama sehemu Kuna mbuga za wanyama basi wananchi wa maeneo husika wazitunze rasilimali kweli kwa sababu watajua kweli bila mbuga hizo utalii utakufa na hawatapata mapato ya kulipa mishahara wafanyakazi wao, kujenga barabara na mitaa bora, kuhudumia Bima za afya na madawa hospitali. Kwa iyo Kama jimbo litategemea utalii basi watautunza na kuuthamini kweli utalii.

Kama jimbo linategemea viwanda au biashara basi jimbo hilo litatunga Sera bora ili kuhamasisha uwekezaji mkubwa wa viwanda na biashara kwa sababu wananchi wa sehemu husika watajua bila hivyo basi hawawezi pata mapato ya kununulia dawa, kupata Maji safi na salama na kujenga barabara nzuri!

Kama jimbo husika linategemea kilimo na migodi basi wananchi wa viongozi wa maeneo husika wataumiza kichwa kuweka Sera bora katika hayo maeneo ili kuhakikisha zinawapatia mapato makubwa ya kufanya miradi ya maendeleo. Watu watajiona kweli kuwa wao ni sehemu sahihi ya maendeleo husika.

Imefika wakati watanzania lazima tuseme kuwa mfumo wa utawala wa Chama cha mapinduzi, umechochea sana ufisadi, umasikini, kujipendekeza, uzembe, ubabaishaji na kutowajibika kweli kwa Watanzania!!!

Mfumo huu wa sasa umefanya watanzania tudharauliwe na viongozi na kuendeshwa Kama watoto wadogo kuwa tusipowachagua watu wao basi tusahau maendeleo kwa sababu wao ndo wanaamua hela zetu wazigawe vipi!! Hii sio sawa kabisa

Mfumo huu wa sasa umesababisha watu kuwa ombaomba na watumwa kwenye nchi yao kuwa kila wakimuona Raisi basi wamnyenyekee kama Mungu n kumuomba hiki na kile. Kama Raisi tunaomba Maji, barabara, umeme na shule bora

Kwa maendeleo ya kweli ni lazima Watanzania tuamue kwenye uchaguzi huu kumchagua Tundu Antiphas Lissu ili atubadirishie mfumo.

Hamasisha watu wengi zaidi kumchagua Lissu na Chadema kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania na Watanzania!

Sambaza kwa watu wengi zaidi waelimike pia!!

Asanteni!
Lord denning.
 
Kama kuna kijana nchi hii hataelewa Lissu anasema nini juu ya kesho ya vizazi vyetu itabidi mniletee nimwombee mana shetani wa Kijani atakuwa amemteka.

Wakati wa vijana kujenga upya nchi yetu kiuchumi ni sasa. Wakati wa kuonyesha Ustaarabu wetu,utu wetu ,umoja wetu,mshikamano wetu na vizazi vyetu ni sasa..twende tukafanye hatima yetu kwa Chama chenye Sera wezeshi..CDM!!
 
Kama kuna kijana nchi hii hataelewa Lissu anasema nini juu ya kesho ya vizazi vyetu itabidi mniletee nimwombee mana shetani wa Kijani atakuwa amemteka.

Wakati wa vijana kujenga upya nchi yetu kiuchumi ni sasa. Wakati wa kuonyesha Ustaarabu wetu,utu wetu ,umoja wetu,mshikamano wetu na vizazi vyetu ni sasa..twende tukafanye hatima yetu kwa Chama chenye Sera wezeshi..CDM!!
Ni sahihi kabisa, vijana wa sasa ndio watakaoamua hatma sahihi ya nchi yetu miaka 100 mbele. Ni wakati sahihi kwa vijana kufanya uamuzi sahihi kwa mustakabali wa taifa hili kwenye uchaguzi wa mwaka huu!!
 
Mimi ameipata siku nyingi sana. Ya kwangu, familia yangu, kazini kwetu wote, marafiki, ndugu, jamaa na mtaani kote sisi ni Tundu Lissu. Tumaini letu ni Tundu Lissu tu.
Asante sana. Tuwaelimishe kweli watanzania wenzetu juu ya haya!! Mfumo umewageuza kuwa watumwa na inabidi waelewe na wafanye maamuzi sahihi mwaka huu!!
 
KURA yako Moja haitamtosha kuwa Rais. Watanzania, tutampa Magufuli ili amalizie kazi alizozianza.
 
Safi sana jimama26 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾 Mimi naamini kwamba kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki Lissu atashinda kwa asilimia 80% kwenda juu kwani Watanzania hatutaki kumsikia huyo dhalimu jiwe na wala chama chao cha majizi, mafisadi na wauaji.

Mimi ameipata siku nyingi sana. Ya kwangu, familia yangu, kazini kwetu wote, marafiki, ndugu, jamaa na mtaani kote sisi ni Tundu Lissu. Tumaini letu ni Tundu Lissu tu.
 
Safi sana jimama26 🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾 Mimi naamini kwamba kama uchaguzi utakuwa huru na wa haki Lissu atashinda kwa asilimia 80% kwenda juu kwani Watanzania hatutaki kumsikia huyo dhalimu jiwe na wala chama chao cha majizi, mafisadi na wauaji.
Kwa maslahi mapana ya Tanzania na vizazi vijavyo vya Tanzania ni lazima watanzania mwaka huu tuhakikishe kuwa Vyovyote vile uchaguzi uwe huru au usiwe huru, Tundu Antiphas Lissu anaingia madarakani mwaka huu
 
Kura yangu, kura za majirani zangu, wahangaikaji wenzangu na ukoo wangu zote kwa Lisu.

Lisu aanze kuandaa hotuba ya siku ya kuapishwa kuwa rais.
Hata mimi pia !! Ninampigia kampeni kwa nguvu sana Tundu Antiphas Lissu
 
Ni yeye tu
IMG_20200917_190951.jpeg
 
Back
Top Bottom