TUNDU LISSU: Kuporwa kwa mafao ya Wafanyakazi ni dhambi ya Bunge au tunalishwa matango pori?

Ni kwa sababu wanaangalia maslahi yao kwanza!

Mimi tokea 2007 nahoji kuhusu mishahara ya viongozi wetu wa juu na mpaka hivi sasa hakuna information za uhakika!!!

Lissu kagusia kidogo hilo suala.
Yaan viongozi wa kibongo ni shida sana. Ndio mana utaona Mkapa alihakikisha kajenga daraja la Mkapa, kikwete akatia kiwe la msingi Bandar ya bagamoyo ambayo pia imebumba leave alone mwendokasiya tegeta ambayo magu kauli ngumu. Sasa magu kaja na airport Chato mara uwanja wa mpira. Yaan miradi yote hii inaonyesha umimi mimi. Sasa sijui zinazoingia mfukoni mwao ni kiasi gani kwa kweli.
 
Sina lakusema nasubiri kisanuke nichukue changu labda ndio tutaeshimiana lissu long live our hero forever wewe ndio mwenye uchungu na taifa unajua nini watanzania wengi kama wangekuwa wamejitambua hakika ccm ingekuwa na hali mbaya kuliko unavyo iona ilivyo mkuu Kamanda tupe nyenzo tufanye nini?
 
Gratuity ni kiinua mgongo. Haijalishi ni kwa mkataba wa muda gani.
Hoja hizi za Lisu zinatoa mwanga wa hili janga. Dhuluma huambatana na laana.Utetezi wowote hauna manufaa kwa mstaafu.
Hivi mnamwelewa vizuri Rais? Haoni tabu kuzibani hata hizo na ikitokea hivyo mtaona huyo aliyetoa maada pia analialia.
 
Yote kwa yote,wa kulaumiwa zaidi pia ni vyama 'butu' vya wafanyakazi.

Naamini na wao kama wadau ktk majadiliano ya hiyo kanuni nyonyaji kwa watumishi wa umma na wao waliridhia udhalimu huo na ndio maana hadi sasa hakuna chama chochote kilichotoa tamko lolote la kuilaani serikali juu ya unyonyaji huo kwa kuwa na wao pia walishiriki ktk vikao.

Kikubwa hapa ni watumishi kujipigania wenyewe kupitia mikutano yao mbalimbali na ikiwezekana wapeleke mihtasari ya malalamiko yao kwa Mh.Rais kwani ni yeye tu mwenye mamlaka ya kuzuia kutumika kwa hiyo kanuni na si mwingine yoyote yule
 
Kwenye maslahi ya GREENS hakuna msaada wa "wanyonge",wanatumia wingi wao na wala hawaangalii athari ya kitu chochote,huwa hawajipingi hata.
 
Hii Sheria ni maangamizi makubwa. Wataalam kwenye Wizara ya kazi, katika na Sheria wamewasaliti wafanyakazi wenzao. Aibu
 
Bunge ni muhimili wenye mamlaka yaliyoclear sana kwenye katiba sema haliyatumii kwa sababu ya kujaa wabunge vihiyo na wahuni
 
Hiii nchi hakuna chakusema Rais wa wanyonge,hii serikali ni ya kibepari tuu
 
Kulalamika bila kuwa na solutions imekuwa desturi ya wa Tz. Sio vijana,wazee,wasomi mpaka viongoz wa dini. Ona huyu ni kiongoz mkubwa wa upinzani nae mule mule kulalamika. Bro njoo na soln nini kifanyike baada ya kushindwa mbinu zote zilizopita.

RAI KWA WATZ: mi nadhani Sasa ni muda wa kujadili nini kifanyike kwani ukipita mitaani ni kama kila mwananchi anajua tatizo liko wp. Yaani iwe muuza mchicha,mwalimu,Dr na wote. Ni mafundi wa kulalamika na kuonesha tatizo lilivyoanza mpaka lilipofikia ila hawaleti au kujadili nini tufanye ili kumaliza udhalimu unaoendelea. Tuache kulalamika Tuchukue hatua Ogopeshi
 
Huu uzi ni mzito kwake. Alijaribu kutupia vikoment kama viwili mwanzoni akaona hata wa mlengo wake hawamsapoti, akaamua kuishia. Hii thread imekwenda shule, watu wa aina hizo si size yao.
Ndy wazeee wa ndiyo walahi

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…