TUNDU LISSU: Kuporwa kwa mafao ya Wafanyakazi ni dhambi ya Bunge au tunalishwa matango pori?

Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
6,259
Points
2,000
Kurzweil

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
6,259 2,000
Wakubwa zangu salaam. Mimi ni Mbunge na kwa hiyo ninaweza kusemwa nina maslahi katika mjadala huu. Ninayo kweli.

Kwa vile 'mmetupiga' sana kwenye suala hili, ninaamini hamtajali sana nikijitetea mwenyewe, na kuwatetea wenzangu, hata kama hawajanituma.

Kuna hatari kubwa ya kutumia suala la mafao ya wafanyakazi kuwachonganisha Wabunge kwa wananchi, ili watu wenye agenda za kuua Bunge letu kama taasisi watimize matakwa yao. Naomba kufafanua.

Ni kweli kwamba utaratibu huu wa mafao hauwahusu Wabunge. Lakini sio Wabunge peke yao. Utaratibu huu hauwahusu pia Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote. Vile vile hauwahusu Mawaziri na Naibu Mawaziri wote, Rais na Makamu wa Rais.

Hawa wote sio 'wafanyakazi' kwa maana ya kisheria ya neno hilo. Ni watumishi wa kisiasa na mishahara na marupurupu yao yapo kwenye kundi la utumishi wa umma wa kisiasa.

Na sio wanasiasa tu ambao sio 'wafanyakazi.' Makamishna wa Tume mbali mbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa Katiba au sheria mahsusi, na wajumbe wa Bodi mbali mbali za taasisi na mashirika ya umma nao sio 'wafanyakazi', na kwa hiyo hawahusiki na utaratibu huu wa mafao ya wafanyakazi.

Wote niliowataja hawalipwi pensheni wanapomaliza muda wao wa utumishi. Hulipwa kitu kinaitwa 'gratuity' (mtanisaidia Kiswahili chake), yaani malipo ya mkupuo mmoja wanapomaliza utumishi.

Viwango vya gratuity hiyo vinatofautiana kulingana na cheo cha mhusika. Kwa Wabunge mnaotusema sana ni 40% ya mishahara yote ya miaka mitano. Hicho pia ni kiwango cha Wakuu wa Wilaya ambao hamjawagusa kabisa kwenye mjadala huu.

Kwa Wakuu wa Mikoa na Naibu Mawaziri, gratuity yao ni 50% ya mishahara yote ya muda wao utumishi. Hawa pia hakuna anayewasema.

Kwa Mawaziri (na kama sikosei Naibu Spika) kiwango cha gratuity yao ni 60% ya mishahara yote ya muda wao wa utumishi. Hapa pia sijasikia malalamiko wala hasira yoyote.

Kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika, hawa utaratibu wao ni mnono zaidi. Kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa ya mwaka '99, Rais anayemaliza muda wake anatakiwa kulipwa 80% ya mishahara yote ya Urais wake; mshahara wake wote wa miaka miwili kwa ajili ya maandalizi ya kustaafu; na baada ya hapo ataendelea kulipwa 80% ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani hadi atakapofariki dunia.

Mafao haya ni nje ya mafao mengine kama nyumba yenye furniture zote, magari, ofisi, walinzi na watumishi kadhaa wa ndani na wa ofisi. Sijaona wala kusikia mtu yeyote akimnyooshea kidole mtetezi wa wanyonge aliyeko Magogoni kwa sasa, wala kuhoji uzalendo au uadilifu wake.

Kwa Makamu wa Rais kiwango ni hicho hicho cha 80% ya mishahara yote na baada ya hapo pensheni ya kila mwezi ya 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais aliyeko madarakani hadi kifo. Na hii pia ni nje ya nyumba, furnishings, gari, walinzi, watumishi, etc.

Kwa Waziri Mkuu na Spika ni 70% kwa utaratibu huo huo.

Ukiachia Wabunge, hakuna yeyote ambaye amewalalamikia wote hawa, pamoja na ukweli kwamba mafao yao ni makubwa kuliko ya Wabunge.

'Ignorance is bliss', Waingereza wanasema. Ujinga ni amani. Watu wetu wengi ni wajinga, hawaelewi nchi hii inavyoendeshwa. Kwa hiyo ni warahisi sana kuaminishwa kwamba Wabunge wao ndio wabaya, wasaliti, etc.

Wakishaamini kwamba Wabunge ndio tatizo, itakuwa rahisi zaidi kujenga hoja za kulidhoofisha Bunge letu zaidi ya lilivyo sasa. Tayari Serikali ya Magufuli imefanya na inaendelea kufanya mambo mengi yenye kulidhoofisha Bunge letu.

Je, nitahojiwa, Wabunge si ndio waliopitisha sheria hii ya kuwanyonga wafanyakazi na kujipendelea wao na wakubwa wenzao???

Jibu la haraka haraka ni ndio, sheria hiyo, na hizo nyingine zimepitishwa na Bunge.

Lakini suala la msingi ni je, kwa Katiba yetu ya sasa na Sheria zake, na kwa historia yetu ya kisiasa na ya kibunge ya tangu Uhuru, Wabunge hawa walikuwa na uwezo wa kukataa kupitisha sheria hizi???

Angalau tangu Katiba ya Jamhuri ya mwaka '62, Bunge la Tanganyika, na baadae Tanzania, limeendeshwa, kwa kiasi kikubwa, na Ikulu.

Bunge la mpaka mwaka '85 liliendeshwa na Ikulu ya Mwalimu Nyerere; la mpaka mwaka '95 liliendeshwa na Ikulu ya Mzee Mwinyi; la mpaka mwaka '05 lilikuwa kwenye mabawa ya Ikulu ya Ben Mkapa; la hadi mwaka '15 lilikuwa chini ya kivuli cha Ikulu ya Jakaya Kikwete, na Bunge la sasa liko chini ya udhibiti mkubwa wa Ikulu ya Magufuli. Huu ndio ukweli mchungu wa historia ya nchi yetu.

Kwa miaka yote hii, kwa sababu ya kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme, Bunge letu limekuwa dhaifu sana. Bunge la aina hii, haliwezi - na halijawahi - kukataa Muswada unaopelekwa Bungeni na Ikulu. The very few, if any, exceptions only prove the general principle of our history.

Kwa hiyo, kuwalaumu Wabunge hawa kwa kupitisha sheria hii ya mafao ya wafanyakazi is simply to miss the point. Bunge la kondoo la miaka yote hii haliwezi kubadilika ghafla na kuwa Bunge la simba!!!

Nataka niwe wazi. Hapa ninazungumzia Bunge la wanaCCM. Sisi wapinzani tumekuwa wachache miaka yote hii tokea mwaka '95. Tumekuwa tunapinga mambo haya lakini, kwa sababu ya uchache wetu, 'tumefyekelewa mbali' na wale wanaosema: "Wanafiki waseme NDIYO!!!"

Na wanafiki wamesema 'NDIYO' kwa kila kitu walicholetewa na Ikulu ya Mwenyekiti wao wa Chama. Kwa hiyo, Sheria hii ya mafao ya wafanyakazi ni Sheria ya mpangaji wa sasa wa Ikulu pamoja na Wabunge wa Chama chao. Hili ni la kwanza.

La pili, na la mwisho kwa leo, linahusu sababu halisi ya mabadiliko haya ya sheria za mafao ya wafanyakazi.

Sababu halisi sio uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi wanaostaafu kama tunavyoambiwa na Mifuko yenyewe, au wakubwa wa Serikali hii. Hayo ni 'matango pori' wanayolishwa the blissfully ignorant.

Sababu halisi ni kwamba watawala wa CCM wameua mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kutapanya pesa za wafanyakazi kwenye miradi isiyokuwa na tija kwa wafanyakazi.

Pesa za wafanyakazi zimetumika kujenga 'White Elephants' kama majengo mengi na makubwa yaliyopo Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kwingineko.

Kwa kiasi kikubwa, na kwa sababu mbali mbali, majengo haya hayapangishiki. Hivyo, licha ya kugharimu matrilioni ya shilingi, fedha za wafanyakazi hazitarudi.

Mifuko ya hifadhi ya jamii ndiyo iliyojenga UDOM; na tangu mwaka '09 CAG amelalamika kwamba Serikali imeshindwa kurudisha fedha hizo za wafanyakazi kwa sababu ama hakukuwa na mikataba au mikataba yenyewe haieleweki.

Pesa za wafanyakazi ndizo zilizojenga Ofisi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi karibu na St. Peter's, Dar Es Salaam; nyumba za polisi Kurasini Dar; Machinga Complex Dar; Daraja la Kigamboni Dar, n.k.

Pesa za wafanyakazi zimetumika sana kuhonga baadhi ya Mawaziri na Wabunge kwa kuwapa miradi inayoitwa ya maendeleo, kama vile kununua mipira na jezi za michezo kwa timu za vijana kwa majimbo ya Wabunge na Mawaziri hao.

Waliofaidika na 'ukarimu' huu ni pamoja na Rais Magufuli mwenyewe, akiwa Waziri na Mbunge wa Chato. Hili nililizungumzia hata Bungeni takriban miaka minne iliyopita.

Lengo la hongo hizi ni kuwanyamazisha ili watu 'wapige' pesa za wafanyakazi. Ndio maana wala sio ajabu kwamba waliokamatwa na kushtakiwa kwa 'kupiga' pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii sio akina Ramadhani Dau au Sanga wa iliyokuwa NSSF na LAPF, au akina AG Masaju na Naibu Spika Tulia Ackson waliokuwa Wadhamini wa Mifuko hiyo, bali ni wakurugenzi na mameneja wa kati wa Mifuko.

Wakurugenzi Wakuu na Wadhamini wa Mifuko, waliofanya maamuzi ya utapanyaji huu wa fedha za wafanyakazi, wamepandishwa vyeo na kuwa mabalozi au wabunge wa kuteuliwa na Rais au Majaji wa kuteuliwa na Rais pia.

Baada ya kuifilisi mifuko ndio watawala wakaanzisha hizi hoja za mara kuiunganisha, mara kubadili mfumo wa mafao, etc.

Suala muhimu lisilozungumzwa ni je, mifuko hii ina fedha za kulipa wafanyakazi wanaostaafu au kuacha kazi kwa sababu mbali mbali??? Pesa 'zilizokopwa' kujengea miradi hii na mingine mingi zimerudishwa lini?

Naomba kumalizia. Kutupiga Wabunge ni sawa sawa. Bunge lina sehemu yake ya lawama kwenye hili. Lakini ni Bunge peke yake??? Kwa utaratibu halisi wa utungaji sheria wa nchi yetu chini ya Katiba ya sasa, Bunge ndio lenye mamlaka haya yanayosemwa??? Mjadala na uendelee.

Tundu AM Lissu (MB)
Tienen, Belgium
Novemba 23, 2018
 
For the English Audience
Following the release of new retirement pension regulations where the retired will be paid 25 per cent of his or her pension as lump sum and the remaining will be paid for 12.5 years, Singida East MP, Tundu Lissu has expressed his feelings.

Lissu, who is being treated in Belgium after being shot in Dodoma, Tanzania on 7th September, 2017 said that the principles do not apply to MPs, Regional and District Commissioners, Prime Minister, Ministers and Deputy Ministers, President and Vice-President.

"All of them are not paid a pension when they finish their time in the service. They are paid what is called gratuity, that is the payment of one payout when they finish their service."

"The rates of gratuity differ according to the title, MPs and District Commissioner are paid 40% of the salary for 5 years, Regional Commissioner and Deputy Ministers are paid 50%, Ministers are paid 60%, President, Vice-President, Prime Minister and Parliament Speaker are paid 80%"

"Since the passing of these regulations, many have been blaming the MPs for passing it in the Parliament, but Lissu says "Leaving the MPs aside, no one has complained to others I have mentioned, despite the fact that their benefits are greater than MPs"

"The real reason for this change in the salary benefits of employees is that CCM rulers have killed Social security funds by distributing Workers' money into projects that do not benefit them."

"Some of the projects that were funded by money from Social Security Fund are building of Machinga Complex in Dar, Kigamboni Bridge, Police Houses in Kurasini-Dar, Tanzania Intelligence and National Security Head quarter in Dar."

On the other hand, Parliament Speaker Job Ndugai was quoted said "The Parliament has been wrongly accused for the new pension refulations. It is The Government specifically the responsible ministry that is to blame"
Mazaya

Mazaya

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2015
Messages
554
Points
500
Mazaya

Mazaya

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2015
554 500
Hakuna lolote hapa wabunge wote hope.les.s tu, kwa mshahara wa Wabunge kwa miaka mitano na kwa idadi ya Wabunge wote, the Tundu Lissu haoni kuwa wao pia wanalitia hasara Taifa? Na kuwafanya Watumishi wa umma kunyanyasika ukizingatia hata hilo Bunge hakuna linachofanya?
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
23,476
Points
2,000
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
23,476 2,000
Hoja ya Lissu ni kama analipaka mafuta bunge kwa kushindwa kutimiza wajibu wake kwa wananchi dhidi ya sheria hizi mbovu zinazotungwa na bunge ( siyo sheria ya mafao tu).

Hoja kwamba Bunge halina mamlaka au linaendeshwa kwa remote control ni hoja dhaifu kwa sababu kadhaa.

1 bunge linafanya kazi kwa mujibu wa katiba na siyo kwa mujibu wa matakwa ya rais

2 bunge ndiyo lenye mamlaka ya kutunga sheria hivyo linanafasi kubwa zaidi ya kuwalinda wananchi kupitia sheria linazotunga.

3 Bunge lina mamlaka ya kuisimamia serikali mojawapo ni kwenye hizi sheria serikali inazozipeleka bungeni

4 Bunge halishurutishwi kupitisha kila sheria inayopelekwa bungeni na serikali.

5 Bunge linamamlaka ya kuiwajibisha serikali kwa kupiga vote of no confidence kwa waziri Mkuu au impeachment kwa rais lakini executive haina mamlaka hayo

6 Wabunge ndiyo watetezi wa wananchi hivyo wao ndiyo ngao pekee ya wananchi kujilinda na maovu yoyote yanayoweza kusababishwa na Sera za serikali.

7 Wabunge wote kwa ujumla wao wanawajibu kwa wananchi kwa mujibu wa katiba bila kujali itikadi zao, bunge linapoapishwa linakuwa bunge la jamhuri na siyo la CCM au la CHADEMA hivyo collectively linawajibika kwa kuwatetea wananchi.

Kuna nadharia inajengwa na wabunge kuwa bunge halina linaingiliwa mamlaka yake na serikali japo hakuna ushahidi wa wazi unaoonyesha hivyo , tunaweza kusema kuwa hii dhana ni perceived na siyo actual na lengo lake ni kulipaka mafuta bunge ambalo halitumii mamlaka yake sawa sawa kwa mujibu wa sheria.

Kuna changamoto Moja iko wazi kwa bunge letu pale wabunge wanapochaguliwa hujenga dhana kuwa wao ni wabunge wa chama na siyo wawakilishi wa wanachama.

Wabunge wa ccm ( ambao ni wengi zaidi)huenda mbali zaidi nakujiona wao ni wabunge wa serikali hivyo huipigania serikali bungeni badala ya wananchi huu ni ugonjwa unaoweza kutibika tutafute tiba tu.

Kulitetea bunge kwenye dhahama hii ni kutowatendea haki wapiga kura wetu.

Namheshimu sana lissu ila sikubaliani na hoja yake ni malalamiko yasiyo na mashiko na yanalenga kulipaka mafuta bunge kwa uzembe wake kuwatetea wananchi.
Aliposema "sheria inawachonganisha wabunge na wananchi" aliwakusudia pia watu kama wewe.
Kuna mahalia ama hukusoma au umekataa kupaelewa.
"Mamlaka na Utashi" mambo iko humo.!!
Spika:- "Wanafiki waseme ndiooo!"
Mibunge ya ccm:- (minafiki) "Ndiyooooooo"
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
16,359
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
16,359 2,000
Dawa ni moja tu; fungua mbele mwaga CCM yoote!!
 
D

dapangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Messages
405
Points
250
D

dapangi

JF-Expert Member
Joined Jul 28, 2015
405 250
Gratuity ni kiinua mgongo. Haijalishi ni kwa mkataba wa muda gani.
Hoja hizi za Lisu zinatoa mwanga wa hili janga. Dhuluma huambatana na laana.Utetezi wowote hauna manufaa kwa mstaafu.
 
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
23,476
Points
2,000
jogi

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
23,476 2,000
Hakuna lolote hapa wabunge wote hope.les.s tu, kwa mshahara wa Wabunge kwa miaka mitano na kwa idadi ya Wabunge wote, the Tundu Lissu haoni kuwa wao pia wanalitia hasara Taifa? Na kuwafanya Watumishi wa umma kunyanyasika ukizingatia hata hilo Bunge hakuna linachofanya?
Paaza sauti usikike!
Wapinzani wana/wamepambana sana kutetea maslahi yenu! Wanaishia kubambikiwa kesi za uchochezi!!

"It ..ne be done! Play your P."
 
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2016
Messages
2,785
Points
2,000
pureView Zeiss

pureView Zeiss

JF-Expert Member
Joined Sep 5, 2016
2,785 2,000
Hivi mkuu kwa akili yako huoni kuna umuhimu mkubwa wa kujadili kilichopo hapo juu kwa maslahi yako wewe na ndugu zako?
Aisee kwa hii comment yako nimeona huruma sana kwa huyo fola anayeshabikia upuuzi nafikiri anahisi sheria ile ya mafao ni kwa wapinzani pekee
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
30,934
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
30,934 2,000
Mkuu hilo bwege mtozeni haliwezi kukuelewa. Ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa
Weka andiko kama la Lisu, watu walitafakali, usilete mambo ya vijiwe. Lete andiko kuhusu usaliti na Acasia. make a comprehensive presentation on that siyo mapambio ya kitchen party! Lisu ameandika his views, discuss his ideas and make a challenge of them!
 
josam

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
2,054
Points
1,500
josam

josam

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
2,054 1,500

Umemuweza, ana maarifa ya kuchambua hoja zaidi ya kuleta maneno mawili matatu ya udaku!? Isha ataiwezea wapi, kwa maarifa yepi?! Asante
 
josam

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
2,054
Points
1,500
josam

josam

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
2,054 1,500
Hon Lisu is it possible to challenge unjust laws kama hizi in the court of law? Najua kama kuna sheria inapingana na katiba, hiyo unaweza (ingawa kwa ilivyo sasa na compromised/doomed judiciary itakuwa ngumu, LABDA MWALUSANYA, LUGAKINGIRA warudi). Kwa sheria kama hizi mfano ya vyama vya siasa, inaweza kupingwa mahakamani?
Pendekezo zuri!
 
jogoo_dume

jogoo_dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2014
Messages
2,090
Points
2,000
jogoo_dume

jogoo_dume

JF-Expert Member
Joined Oct 20, 2014
2,090 2,000
Wakubwa zangu salaam. Mimi ni Mbunge na kwa hiyo ninaweza kusemwa nina maslahi katika mjadala huu. Ninayo kweli.

Kwa vile 'mmetupiga' sana kwenye suala hili, ninaamini hamtajali sana nikijitetea mwenyewe, na kuwatetea wenzangu, hata kama hawajanituma.

Kuna hatari kubwa ya kutumia suala la mafao ya wafanyakazi kuwachonganisha Wabunge kwa wananchi, ili watu wenye agenda za kuua Bunge letu kama taasisi watimize matakwa yao. Naomba kufafanua.

Ni kweli kwamba utaratibu huu wa mafao hauwahusu Wabunge. Lakini sio Wabunge peke yao. Utaratibu huu hauwahusu pia Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote. Vile vile hauwahusu Mawaziri na Naibu Mawaziri wote, Rais na Makamu wa Rais.

Hawa wote sio 'wafanyakazi' kwa maana ya kisheria ya neno hilo. Ni watumishi wa kisiasa na mishahara na marupurupu yao yapo kwenye kundi la utumishi wa umma wa kisiasa.

Na sio wanasiasa tu ambao sio 'wafanyakazi.' Makamishna wa Tume mbali mbali zilizoanzishwa kwa mujibu wa Katiba au sheria mahsusi, na wajumbe wa Bodi mbali mbali za taasisi na mashirika ya umma nao sio 'wafanyakazi', na kwa hiyo hawahusiki na utaratibu huu wa mafao ya wafanyakazi.

Wote niliowataja hawalipwi pensheni wanapomaliza muda wao wa utumishi. Hulipwa kitu kinaitwa 'gratuity' (mtanisaidia Kiswahili chake), yaani malipo ya mkupuo mmoja wanapomaliza utumishi.

Viwango vya gratuity hiyo vinatofautiana kulingana na cheo cha mhusika. Kwa Wabunge mnaotusema sana ni 40% ya mishahara yote ya miaka mitano. Hicho pia ni kiwango cha Wakuu wa Wilaya ambao hamjawagusa kabisa kwenye mjadala huu.

Kwa Wakuu wa Mikoa na Naibu Mawaziri, gratuity yao ni 50% ya mishahara yote ya muda wao utumishi. Hawa pia hakuna anayewasema.

Kwa Mawaziri (na kama sikosei Naibu Spika) kiwango cha gratuity yao ni 60% ya mishahara yote ya muda wao wa utumishi. Hapa pia sijasikia malalamiko wala hasira yoyote.

Kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Spika, hawa utaratibu wao ni mnono zaidi. Kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa ya mwaka '99, Rais anayemaliza muda wake anatakiwa kulipwa 80% ya mishahara yote ya Urais wake; mshahara wake wote wa miaka miwili kwa ajili ya maandalizi ya kustaafu; na baada ya hapo ataendelea kulipwa 80% ya mshahara wa Rais aliyeko madarakani hadi atakapofariki dunia.

Mafao haya ni nje ya mafao mengine kama nyumba yenye furniture zote, magari, ofisi, walinzi na watumishi kadhaa wa ndani na wa ofisi. Sijaona wala kusikia mtu yeyote akimnyooshea kidole mtetezi wa wanyonge aliyeko Magogoni kwa sasa, wala kuhoji uzalendo au uadilifu wake.

Kwa Makamu wa Rais kiwango ni hicho hicho cha 80% ya mishahara yote na baada ya hapo pensheni ya kila mwezi ya 80% ya mshahara wa Makamu wa Rais aliyeko madarakani hadi kifo. Na hii pia ni nje ya nyumba, furnishings, gari, walinzi, watumishi, etc.

Kwa Waziri Mkuu na Spika ni 70% kwa utaratibu huo huo.

Ukiachia Wabunge, hakuna yeyote ambaye amewalalamikia wote hawa, pamoja na ukweli kwamba mafao yao ni makubwa kuliko ya Wabunge.

'Ignorance is bliss', Waingereza wanasema. Ujinga ni amani. Watu wetu wengi ni wajinga, hawaelewi nchi hii inavyoendeshwa. Kwa hiyo ni warahisi sana kuaminishwa kwamba Wabunge wao ndio wabaya, wasaliti, etc.

Wakishaamini kwamba Wabunge ndio tatizo, itakuwa rahisi zaidi kujenga hoja za kulidhoofisha Bunge letu zaidi ya lilivyo sasa. Tayari Serikali ya Magufuli imefanya na inaendelea kufanya mambo mengi yenye kulidhoofisha Bunge letu.

Je, nitahojiwa, Wabunge si ndio waliopitisha sheria hii ya kuwanyonga wafanyakazi na kujipendelea wao na wakubwa wenzao???

Jibu la haraka haraka ni ndio, sheria hiyo, na hizo nyingine zimepitishwa na Bunge.

Lakini suala la msingi ni je, kwa Katiba yetu ya sasa na Sheria zake, na kwa historia yetu ya kisiasa na ya kibunge ya tangu Uhuru, Wabunge hawa walikuwa na uwezo wa kukataa kupitisha sheria hizi???

Angalau tangu Katiba ya Jamhuri ya mwaka '62, Bunge la Tanganyika, na baadae Tanzania, limeendeshwa, kwa kiasi kikubwa, na Ikulu.

Bunge la mpaka mwaka '85 liliendeshwa na Ikulu ya Mwalimu Nyerere; la mpaka mwaka '95 liliendeshwa na Ikulu ya Mzee Mwinyi; la mpaka mwaka '05 lilikuwa kwenye mabawa ya Ikulu ya Ben Mkapa; la hadi mwaka '15 lilikuwa chini ya kivuli cha Ikulu ya Jakaya Kikwete, na Bunge la sasa liko chini ya udhibiti mkubwa wa Ikulu ya Magufuli. Huu ndio ukweli mchungu wa historia ya nchi yetu.

Kwa miaka yote hii, kwa sababu ya kivuli kirefu cha Urais wa Kifalme, Bunge letu limekuwa dhaifu sana. Bunge la aina hii, haliwezi - na halijawahi - kukataa Muswada unaopelekwa Bungeni na Ikulu. The very few, if any, exceptions only prove the general principle of our history.

Kwa hiyo, kuwalaumu Wabunge hawa kwa kupitisha sheria hii ya mafao ya wafanyakazi is simply to miss the point. Bunge la kondoo la miaka yote hii haliwezi kubadilika ghafla na kuwa Bunge la simba!!!

Nataka niwe wazi. Hapa ninazungumzia Bunge la wanaCCM. Sisi wapinzani tumekuwa wachache miaka yote hii tokea mwaka '95. Tumekuwa tunapinga mambo haya lakini, kwa sababu ya uchache wetu, 'tumefyekelewa mbali' na wale wanaosema: "Wanafiki waseme NDIYO!!!"

Na wanafiki wamesema 'NDIYO' kwa kila kitu walicholetewa na Ikulu ya Mwenyekiti wao wa Chama. Kwa hiyo, Sheria hii ya mafao ya wafanyakazi ni Sheria ya mpangaji wa sasa wa Ikulu pamoja na Wabunge wa Chama chao. Hili ni la kwanza.

La pili, na la mwisho kwa leo, linahusu sababu halisi ya mabadiliko haya ya sheria za mafao ya wafanyakazi.

Sababu halisi sio uboreshaji wa maslahi ya wafanyakazi wanaostaafu kama tunavyoambiwa na Mifuko yenyewe, au wakubwa wa Serikali hii. Hayo ni 'matango pori' wanayolishwa the blissfully ignorant.

Sababu halisi ni kwamba watawala wa CCM wameua mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kutapanya pesa za wafanyakazi kwenye miradi isiyokuwa na tija kwa wafanyakazi.

Pesa za wafanyakazi zimetumika kujenga 'White Elephants' kama majengo mengi na makubwa yaliyopo Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma na kwingineko.

Kwa kiasi kikubwa, na kwa sababu mbali mbali, majengo haya hayapangishiki. Hivyo, licha ya kugharimu matrilioni ya shilingi, fedha za wafanyakazi hazitarudi.

Mifuko ya hifadhi ya jamii ndiyo iliyojenga UDOM; na tangu mwaka '09 CAG amelalamika kwamba Serikali imeshindwa kurudisha fedha hizo za wafanyakazi kwa sababu ama hakukuwa na mikataba au mikataba yenyewe haieleweki.

Pesa za wafanyakazi ndizo zilizojenga Ofisi ya Idara ya Usalama wa Taifa na Ujasusi karibu na St. Peter's, Dar Es Salaam; nyumba za polisi Kurasini Dar; Machinga Complex Dar; Daraja la Kigamboni Dar, n.k.

Pesa za wafanyakazi zimetumika sana kuhonga baadhi ya Mawaziri na Wabunge kwa kuwapa miradi inayoitwa ya maendeleo, kama vile kununua mipira na jezi za michezo kwa timu za vijana kwa majimbo ya Wabunge na Mawaziri hao.

Waliofaidika na 'ukarimu' huu ni pamoja na Rais Magufuli mwenyewe, akiwa Waziri na Mbunge wa Chato. Hili nililizungumzia hata Bungeni takriban miaka minne iliyopita.

Lengo la hongo hizi ni kuwanyamazisha ili watu 'wapige' pesa za wafanyakazi. Ndio maana wala sio ajabu kwamba waliokamatwa na kushtakiwa kwa 'kupiga' pesa za mifuko ya hifadhi ya jamii sio akina Ramadhani Dau au Sanga wa iliyokuwa NSSF na LAPF, au akina AG Masaju na Naibu Spika Tulia Ackson waliokuwa Wadhamini wa Mifuko hiyo, bali ni wakurugenzi na mameneja wa kati wa Mifuko.

Wakurugenzi Wakuu na Wadhamini wa Mifuko, waliofanya maamuzi ya utapanyaji huu wa fedha za wafanyakazi, wamepandishwa vyeo na kuwa mabalozi au wabunge wa kuteuliwa na Rais au Majaji wa kuteuliwa na Rais pia.

Baada ya kuifilisi mifuko ndio watawala wakaanzisha hizi hoja za mara kuiunganisha, mara kubadili mfumo wa mafao, etc.

Suala muhimu lisilozungumzwa ni je, mifuko hii ina fedha za kulipa wafanyakazi wanaostaafu au kuacha kazi kwa sababu mbali mbali??? Pesa 'zilizokopwa' kujengea miradi hii na mingine mingi zimerudishwa lini?

Naomba kumalizia. Kutupiga Wabunge ni sawa sawa. Bunge lina sehemu yake ya lawama kwenye hili. Lakini ni Bunge peke yake??? Kwa utaratibu halisi wa utungaji sheria wa nchi yetu chini ya Katiba ya sasa, Bunge ndio lenye mamlaka haya yanayosemwa??? Mjadala na uendelee.

Tundu AM Lissu (MB)
Tienen, Belgium
Novemba 23, 2018
Anajitetea kwa hiyo kuwa ni poa yeye kuchukua mafao na sisi kukosa.
 
josam

josam

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
2,054
Points
1,500
josam

josam

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
2,054 1,500
hapa nimekuelewa vyema mkuu mungu akulinde hukohuko ulipo walishazoea kupiga tangu enzi hizo nyie ndoo watu wakusemea haya
Aendelee kuishi huko huko ili apate muda wa kuchambua haya mambo. Asante Hon Lissu
 
vesta

vesta

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2014
Messages
783
Points
1,000
vesta

vesta

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2014
783 1,000
Wabunge wa Tanzania ni mara chache sana kukubaliana kwa kauli moja. Mara chache hizo huwa ni kwenye mada zinazogusa maslahi yao
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
63,855
Points
2,000
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
63,855 2,000
Simba wa Yuda ameunguruma,swala huko Lumumba wanatafutana!

CCM hawana haki wala uhalali wa kulaumu mabeberu kwani wao ni mababeru hatari zaidi!

Hiki chama kimegeuka chama cha kunyonya masikini wa nchi hii.Ni wanyonyaji hawa watu.

Wanajitapa majukwaani kuwa wamepunguza mishahara mikubwa ya baadhi ya watumishi.Waulizeni mbona hawapunguzi masilahi yao haya manono manono?

Tuambieni uzalendo wa huyo Magu ni upi?

Tuambieni huu ndio ujamaa anaohubirI Magu japo hautamki rasimi?

Tuliochagua kuukataa moja kwa moja utawala huu wa awamu ya tano kama tulivyozikataa tawala zote za CCM zilizopita,kamwe hatujawahi kukosea na kamawe hatuna cha kujutia.

CCM ni ile ile kama walivyoimba wenyewe mwaka 2015.

Wajinga wanapumbuzwa na Bombardier, Dreamliner, flyover,SGR na vitu vya aina hiyo na kudhani maisha yao yatabadilishwa na hivI vitu na wala si kwanza kwa kubadili hii katiba mbovu tulionayo.
UTAFITI HURU UNAONYESHA KWAMBA MH TUNDU LISSU NDIYE MWANASHERIA BORA KABISA KUWAHI KUWEPO KWENYE ENEO LA MAZIWA MAKUU TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI
 
Forum statistics

Threads 1,335,238
Members 512,274
Posts 32,499,951
Top