Tundu Lissu kumburuta Kinana mahakamani

Tundu Lissu kumburuta Kinana mahakamani

Safi sana!!! hiyo ndio dawa ya watu wanaojidai hawana akili wakati wanazo. Nadhani huu utaratibu anaotaka kuuanzisha Lissu unafaa kusapotiwa, inabidi tuanze kuutumia upumbavu wa hawa magamba kwa faida. Kadri watakavyoona upumbavu wao unawagharimu ndivyo akili zitakavyoanza kuwasogea taratibu.


Sure thing mkuu
 
Namshangaa sana Kamanda Lissu ni kwnini hadi leo hajamfikikisha Kortinin Madelu Lameck
 
Safi sana!!! hiyo ndio dawa ya watu wanaojidai hawana akili wakati wanazo. Nadhani huu utaratibu anaotaka kuuanzisha Lissu unafaa kusapotiwa, inabidi tuanze kuutumia upumbavu wa hawa magamba kwa faida. Kadri watakavyoona upumbavu wao unawagharimu ndivyo akili zitakavyoanza kuwasogea taratibu.


Mkuu umenena sawa kabisa haiwezekani watu wanalala na njaa, nchi inamatatizo lukuki alafu wanaleta mambo ya kipuuzi namna hii, huu ujinga unatakiwa ukomeshwe
 
Ngoma inogile, mpaka huyu KINONO aombe poooh! Kwa DR. LISU. Saaaaaafi! Lisu, safi CDM
 
Lissu amesema katika kesi hiyo ya aina yake mbali na Kinana kama mshtakiwa namba moja atawaunganisha pia Bodi ya wadhamini wa CCM,Katibu Mkuu wa zamani Yusuph Makamba na Wakili Godfrey Wasonga aliyekuwa anaitetea CCM mahakamani.
Huku akicheka Lissu amesema ana uhakika wa kulipwa mamilioni Fedha ambazo amedai zitasaidia uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na ule mkuu wa 2015.
Anachokisema Mh. Lisuu hapa kama kitafanyika basi itakuwa tu ni mwendelezo wa njia za kiuchumi katika kuzungusha pesa kwenye jamii kwa sababu pesa zitakazolipwa ni pesa kutoka mifukoni mwa wafanyabiashara na walalahoi wanaoipa serikali pesa kwa njia ya tax ambazo baadaye zinazopelekwa kwenye vyama vya siasa (CCM) kwa njia ya ruzuku na zitarudi tena kwenye mikono ya wachache (campaigner, mawakala, n.k) kwa njia ya malipo ya faini kutoka CCM.

Hakuna kitakachotoka mfukoni mwa Kinana, Bodi ya wadhamini wa CCM na pia Wakili Godfley Wasonga.
 
Na hili litakuwa funzo kwa viongozi majangili na wanamipasho. Hizi siyo zama za ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA M/KITI. Dhuluma ya kila haki inaanza kuning'inia!!
 
Anachokisema Mh. Lisuu hapa kama kitafanyika basi itakuwa tu ni mwendelezo wa njia za kiuchumi katika kuzungusha pesa kwenye jamii kwa sababu pesa zitakazolipwa ni pesa kutoka mifukoni mwa wafanyabiashara na walalahoi wanaoipa serikali pesa kwa njia ya tax ambazo baadaye zinazopelekwa kwenye vyama vya siasa (CCM) kwa njia ya ruzuku na zitarudi tena kwenye mikono ya wachache (campaigner, mawakala, n.k) kwa njia ya malipo ya faini kutoka CCM.

Hakuna kitakachotoka mfukoni mwa Kinana, Bodi ya wadhamini wa CCM na pia Wakili Godfley Wasonga.

Ukereketwa wako kwa Magamba umekutia upofu...
 
Kinana yupo Tabora na tangu juzi hadi Jana si mmeona jinsi watu walivyotekwa na kukatwa mapanga! Mjiulize
 
Ukereketwa wako kwa Magamba umekutia upofu...
Eleza upofu wangu uko wapi na ukereketwa wangu kwa Magamba uko wapi na siyo kulalamika bila kutoa sababu ya malalamiko. Kwa kufanya hivyo, utanitendea haki na kuuelimisha ukeleketwa wangu ili upofu wangu uishe.

By the way, Magamba ndiyo kina nani?.
 
Baada ya Mahakama ya rufani kuafiki ombi la wakili Godfrey Wasonga la kuondoa kesi ya kupinga ubunge wa Singida mashariki,Tundu Lissu (CHADEMA).mbunge huyo ametangaza kusudio la kuwashtaki Katibu mkuu Kinana na mtangulizi wake Makamba.Lissu anadai kuwa viongozi hao ndio walioshinikiza afunguliwe kesi kupinga ubunge wake.
 
Eleza upofu wangu uko wapi na ukereketwa wangu kwa Magamba uko wapi na siyo kulalamika bila kutoa sababu ya malalamiko. Kwa kufanya hivyo, utanitendea haki na kuuelimisha ukeleketwa wangu ili upofu wangu uishe.

By the way, Magamba ndiyo kina nani?.

Magamba ni nyinyi CCM.
 
Baada ya Mahakama ya
rufani kuafiki ombi la wakili Godfrey Wasonga la kuondoa kesi ya kupinga
ubunge wa Singida mashariki,Tundu Lissu (CHADEMA).mbunge huyo
ametangaza kusudio la kuwashtaki Katibu mkuu Kinana na mtangulizi wake
Makamba.Lissu anadai kuwa viongozi hao ndio walioshinikiza afunguliwe
kesi kupinga ubunge wake.

kamanda songa mbele hao magamba wameshafulia tangu kitambo ila wataisoma 2015
 
Hapo makamba akiona tu lazima augue kuhara maana yeye hajui chochote kuhusu mahakama,anajua kuropoka tu, ila kwa kinana atauza mpaka kwato sasa na utakuwa ndo mwisho wa tembo wetu kuonekana.
 
Kinana na CCM wote wapumbavu walioishiwa na hoja. Kama kweli wapo makini walifuta kwa misingi ipi kesi waliyofungua wenyewe

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom