Tundu Lissu: Kama Polisi inamtaka Dereva wangu ni rahisi sana kumpata kwa kutumia Interpol au AG awasiliane na mwenzake wa Ubelgiji!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,003
142,027
Makamu mwenyekiti wa Chadema Mh. Tundu Antipas Lissu amesema kama kweli Polisi wanamtaka Dereva wake kwa ajili ya ushahidi njia ya kumpata ni rahisi sana.

Adam (Dereva) anaishi Ubelgiji na alikuwa anahudumiwa na Serikali ya huko kwa kila Kitu ila sasa amesomea ufundi na ameajiriwa. So kama polisi wanamuhitaji wanaweza kuwatumia Interpol, au balozi zetu na Hata Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaweza kuwasiliana na yule wa Ubelgiji ili amlete Adam kwa sababu ya Ushahidi wa jinai.

Chanzo: ITV

My take: Nadhani TAL amemaliza ubishi
 
Back
Top Bottom