Heshima Kwenu,
Nimesoma maelezo ya Mchungaji Msigwa, mbunge wa Iringa Mjini kuhusu ugumu wa safari ya kumpeleka TL Narobi, gharama za fedha na kujitolea, nimeshangaa.
Kwa mujiibu wa Msigwa, mpaka sasa wametumia kiasi cha TSh. 160 milioni kwa matibabu tu. Wakati wa safari Mh. Mbowe alishikilia mirija ya mtungi wa gesi kwa kuwa ilikuwa imetoboka, Much. Msigwa alishikilia kitanda kwa kuwa kilifyatuka. Madaktati walikuwa na kazi ya kushikilia dripu za maji.
Kumekuwa na juhudi za kutafuta ndege maalum(air ambulance) kwa ajili ya kumpeleka Mh. Lisu Marekani au Uingereza na gharama ya usafiri ni $ 250,000 au Tsh. 550 milioni ingawa,imeshauriwa kusubiri. Hizi ni fedha nyingi.
Waheshimiwa wabunge wote wamechanga nusu ya posho zao za siku. Wananchi nao kwa ujumla wao wamechanga kupitia simu.
Kuna gharama za viongozi waliokaa Nairobi kwa wiki mbili sasa. Hizi si gharama ndogo.
Chama cha Wanasheria wa Uingereza kutuma barua Tanzania kuhoji mkasa wa Tundu Lisu kunaonesha thamani na umuhimu wake kwa wananchi, wabunge wenzake na serikali pia. Kuna watu wamebeba mzigo kwa ajili ya maombi.
Watu wengi wamejitolea muda, hali na mali.
Huu ndiyo uzalendo wa kweli.