Tundu Lissu hakulitendea haki Jimbo letu la Singida Mashariki

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
295
679
Joel K. Nkurlu

Ikungi, Singida

Turudishe historia nyuma kidogo miaka ya 2010 ambapo Lissu alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA.

Lissu alikuta jimbo hilo likiwa lina mwanga wa kusonga mbele kimaendeleo lakini yeye akaondoa mwanga huo na kusababisha jimbo hilo kuwa na giza totoro. Kwa leo nitajikita kueleza baadhi ya mambo aliyoyafanya Bwana huyu kwa wananchi wa Singida Mashariki:

Kwanza, Lissu hakufanya juhudi zozote za kutatua au kuonesha nia ya kutatua kero ya maji jimboni kwake. Mpaka anavuliwa ubunge, LISSU hakuhamasisha wala kuwasaidia wananchi wake kuchimba visima vya maji katika maeneo yao ili wapate maji safi na salama, ikumbukwe baadhi ya maeneo kuna jimboni kwake kuna chemchem za maji hasa maeneo ya Dung’unyi. Kipindi chote hicho hata jimboni kwake alikuwa haonekani, akiulizwa alidai eti yuko busy kukijenga chama.

Pili, ukifuatilia uchangiaji wa Lissu akiwa Bungeni hutaweza kusikia akiwa anaeleza kuhusu changamoto za wananchi walio mtuma kuwawakilisha Bungeni, utamsikia akiwatetea wachimbaji wa madini wa kigeni na kuikejeli Serikali tu, hali iliyowapelekea wananchi wajimboni kwake kukosa muwakilishi wa changamoto zao Bungeni.

Tatu, Lissu alijilimbikizia fedha za mfuko wa jimbo kwa matumizi yake binafsi na wamilia yake, wala hakuwahi kuchangia maendeleo jimboni kwake kwa kutoa fedha au vifaa vya kusaidia katika kuleta maendeleo kwa wananchi hal iliyosababisha jimbo hilo kudumaa kimaendeleo.

Lissu alishindwa hata kusuluhisha mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya wananchi wa jimbo lake mpaka kupelekea mwaka 2016 mwananchi mmoja kuliwa kwa kuchomwa kisu kwa sababu ya mgogoro wa ardhi.
 
Jambo moja kubwa lililonifanya niwe mtu katili sana miaka hii mitano ya JPM, ni kuona kila kiongozi anatajataja jina la JPM na kumsifia kuliko hata anavyowataja wazazi wake au mume/mke ama watoto wake.
 
Joel K. Nkurlu

Ikungi, Singida

Turudishe historia nyuma kidogo miaka ya 2010 ambapo Lissu alichaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA.

Lissu alikuta jimbo hilo likiwa lina mwanga wa kusonga mbele kimaendeleo lakini yeye akaondoa mwanga huo na kusababisha jimbo hilo kuwa na giza totoro. Kwa leo nitajikita kueleza baadhi ya mambo aliyoyafanya Bwana huyu kwa wananchi wa Singida Mashariki:

Kwanza, Lissu hakufanya juhudi zozote za kutatua au kuonesha nia ya kutatua kero ya maji jimboni kwake. Mpaka anavuliwa ubunge, LISSU hakuhamasisha wala kuwasaidia wananchi wake kuchimba visima vya maji katika maeneo yao ili wapate maji safi na salama, ikumbukwe baadhi ya maeneo kuna jimboni kwake kuna chemchem za maji hasa maeneo ya Dung’unyi. Kipindi chote hicho hata jimboni kwake alikuwa haonekani, akiulizwa alidai eti yuko busy kukijenga chama.

Pili, ukifuatilia uchangiaji wa Lissu akiwa Bungeni hutaweza kusikia akiwa anaeleza kuhusu changamoto za wananchi walio mtuma kuwawakilisha Bungeni, utamsikia akiwatetea wachimbaji wa madini wa kigeni na kuikejeli Serikali tu, hali iliyowapelekea wananchi wajimboni kwake kukosa muwakilishi wa changamoto zao Bungeni.

Tatu, Lissu alijilimbikizia fedha za mfuko wa jimbo kwa matumizi yake binafsi na wamilia yake, wala hakuwahi kuchangia maendeleo jimboni kwake kwa kutoa fedha au vifaa vya kusaidia katika kuleta maendeleo kwa wananchi hal iliyosababisha jimbo hilo kudumaa kimaendeleo.

Lissu alishindwa hata kusuluhisha mgogoro wa ardhi uliokuwepo kati ya wananchi wa jimbo lake mpaka kupelekea mwaka 2016 mwananchi mmoja kuliwa kwa kuchomwa kisu kwa sababu ya mgogoro wa ardhi.
Hivi na wewe unaweza kujiita umeenda shule?hata kidato Cha nne?
Mbunge akasuruhishe mgogoro wa ardhi yeye mamlaka anaitoa wapi?hapimi ardhi,Hana polisi,Mbunge sio serikali ambayo ina vyombo vya kutekeleza hayo,kufuta Hari,kugawa Hari,kuhukumu,kupeleleza,kukusanya ushahidi,
Lisu alikuwa anapigania nchi,sio mkoa au Jimbo,anapigania wizi wa madini,na rasilimali nyingine,ambazo stendi imejengwa singida,lakini sio Tabora Wala Kagera,
 
Back
Top Bottom