Mbunge wa Jimbo la Mtwara vijijini CUF aahidi kumuunga mkono Rais Samia mwaka 2025

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,849
Mbunge wa Mtwara Vijijini kupitia tiketi ya CUF, Shamsia Mtamba amepata nafasi ya kutoa neno wakati msatara wa Rais Samia Suluhu Hassan uliposimama barabarani kwenye ziara ya kikazi jimboni humo, ambapo Shamsia amekiri kuridhishwa na uchapakazi wa Rais Samia huku akimuambia kuwa kwenye uchaguzi ujao wa 2025 atamuunga mkono.

Mbunge Shamsia ametaja baadhi ya changamoto zinazowakabiri wananchi wa jimbo lake ikiwemo kukosekana kwa vitambulisho wa NIDA kwa wananchi wengi na uhaba wa maji safi na salama hivyo amemuomba Rais Samia aongeze jitihada kumaliza matatizo hayo jimboni kwake.
 
Back
Top Bottom