Tundu Lissu avuliwe uongozi CHADEMA

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,143
1,291
Mpaka sasa Wanachadema hawajui hatma ya makamu mwenyekiti wao. Tundu Lissu aidha amegeuka mkimbizi au bado ni Mtanzania.

CHADEMA sasa hivi inapita kipindi kigumu sana kufuatia Mbowe kukabiliwa na kesi ya Ugaidi.

Wengi tulitegemea Lissu angekuwepo kwenye jopo la mawakili katika kumtetea Mbowe lakini hayuko nchini.

Je, CHADEMA sasa hivi inaongozwa kwa remote control toka Ubelgiji?

Kwanini Lissu asikae pembeni kama mwanachama wa kawaida na kumpisha Mch Msigwa ili asikosekane mtu wa kukisemea chama toka nafasi ya juu.

Mtu kama Lissu akirudi 2025 mtampa kweli nafasi ya kugombea urais!?
 
Ili iweje ,soma historia ,viongozi wapigania uhuru waliishi katika kuongoza vuguvugu hizo kwa miaka mingapi.

Lisu ni mmojawapo anepigania UHURU wa nchi hii kutoka kwa mkoloni mweusi anaetuhenyesha tokea waunganishe vyama. nani hakuwa TANU au ASP ? Kama si wewe basi babako nae kama sie basi mamako nae kama sie basi Raisi wako.

Tena nawasihi sana vyama vya Upinzani msijaribu kubadilibadili Wenyeviti wa Vyama hilo ni kosa kubwa sana,hadi pale mmefika kwenye lengo lenu,hapo mnaweza kufanya mabadiliko na kuwapisha vijana,wengine mtakuwa WaZee wa Chama.
 
Ili iweje ,soma historia ,viongozi wapigania uhuru waliishi katika kuongoza vuguvugu hizo kwa miaka mingapi.
Lisu ni mmojawapo anepigania UHURU wa nchi hii kutoka kwa mkoloni mweusi anaetuhenyesha tokea waunganishe vyama. nani hakuwa TANU au ASP...
Mbona chagadema nako bado mkoloni mweusi anaendelea kuongoza?

Piganieni uhuru wa chagadema kwanza kabla ya kukurupuka!
 
MSIGWA ili asikosekane mtu wa kikisemea chama toka nafasi ya juu. Mtu kama LISSU akirudi 2025 mtampa kweli nafasi ya kugombea urais
Katiba ya chadema inasemaje endapo mwenyekiti na makamu wake wasiookuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao? Nani anapaswa kushika nafasi ya uongozi wa chama hicho hali hiyo ikijiyokeza?
 
Mpaka sasa Wanachadema hawajui hatma ya makamu mwenyekiti wao .Tundu LISSU Aidha amegeuka mkimbizi au bado ni mtanzania .Chadema sasa hivi inapita kipindi kigumu sana kufuatia Mbowe kukabiliwa na kesi ya Ugaidi...
Naona umeamua kutumia makapi ya akili badala ya ubongo uliopewa na muumba wako
 
Maccm yanahangaika utadhani kuku anataka kutaga maana wamebanwa kila sehemu
Hawajui hawa kuwa Lissu anaipaisha sasa Chadema kuwa ya kimataifa kabla haijaanza kubomoa kabisa CCM

 
Back
Top Bottom