Tundu Lissu anaogopa nini kumtaja aliyemshambulia kwa risasi?

Unaisi serikali hii yenye nguvu ya kununua wabunge ingeshindwa kumnunua uyoo dereva aseme kuwa waliofanya ni chadema waache kuzunguka ili tukio lilipangwa na wakubwa wa hii nchi
Naongelea ushahidi bila mashaka.

Naongelea hoja ya kutodhurika kwa dereva.

Naongelea hoja ya tuhuma kuwa dereva anaweza kuwa alihusika au anawajua ila anaogopa kuwataja kwa kuogopa usalama wa familia yake baada ya mission kufeli.

Zaidi naongelea kusamehe na kuanza ukurasa mpya hasa kwa familia yake.
Wengependa wawe huru kuendelea kumshukuru Mungu na kuishi kwa amani ya nafsi katika nchi yao.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maswali atakayokabiliana nayo huyu jamaa ni kama yalivyoibuliwa na mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani hivi karibuni kuwa ilikuwaje dereva wake asipatwe na majeraha yoyote,zaidi ni kuwa kwanini asingegeuza gari lao kuelekea sehemu ya usalama hasa polisi au eneo la bunge uzembe ambao ulipelekea kwa yaliyomkuta boss wake.

Naamini kuna hoja zenye mashiko hapa.
Natamani Lissu atufafanulie kuwa ni kwa nini anamuogopa huyo dereva hasa inasemekana kuwa huenda walikuwa nyuma ya hili badala yake anamficha huko aliko.

Akitoa ushirikiano kwa vyombo husika naamini hakuna atakayethubutu kumlipizia bali atapata ulinzi zaidi kutoka jeshi letu la polisi kuliko kuendelea kukifia chama chake kwa kuogopa kukisaliti.

Pia familia yake itakuwa na amani na kusonga mbele na maisha ya kawaida kuliko njia ya woga inayomtesa kwa sasa.

Pia kama binadamu akubali tu kuwa yaliyomtokea ni sehemu ya maisha na asamehe na kusahau ili mke na familia yake wawe na amani ya kuyaendeleza maisha yao kuliko kuendeleza uadui wa kuwataja asiokuwa na uhakika nao hasa akiwa kama mwanasheria anayeamini katika ushahidi usio na mashaka.

Mikasa na ajali ni sehemu ya maisha.

Kikubwa amshukuru Mungu kuwa yuko hai,alinusurika kutoka makusudi ya adui zake ambao hadi sasa ameshindwa kuwathibitisha kisheria.

Kusamehe na kusahau ni ushindi dhidi ya shetani na jeshi lake.

Karibu njoo tuijenge nchi yetu nzuri aliyotuweka Baba Mungu.
Tuhuma zinaleta uadui badala ya kuponya mioyo ya pande zote mbili ukiwepo upande wa mtuhumu.

Nikamuangalia Mungu katika imani yangu ya Kikristu naona kama anakusubiri wewe utubu dhambi ya kutokuachili kwa kusamehe.ie "Letting it go".

Naamini ukienda kutaka ushauri wa kiongozi wako wa kiroho atakuelekeza hivi.

Una familia nzuri Mungu kakuthamini ktk maisha yako hapa duniani.

Hebu waachie legacy hiyo ya kusamehe na kusahau. Hautakuwa mshindwaji bali mshindi.

Bwana wetu Yesu Kristo alitamka maneno ya msamaha na ukombozi pale msalabani juu ya watesi wake aliokuwa anawaona.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
Just thinning,,, sidhani kama TL anawajua exactly waliomshambulia ,,kama ni polis ,,usalama wa taifa ,, chadema ,,ccm ama maadui zake wengine,, Ila ninachokifahamu POLIS wanawajibika kufanya uchunguzi na kupata majibu ya haya maswali tunayojiulizaa,, ila cha ajabu na wao wanamshangaa TL kama wewe unavyoshangaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mtu maarufu kafanyiwa hivi na kuna wengine mnahitaji asamehe na kusahau yaliyompata, inakuwaje kwa sisi ambao hata kwenye nyumba kumi hatujulikani. Sheria lazima ifuate mkondo wake na si kuweka mambo ya siasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom