Tundu Lissu amjibu Rais Kikwete

Tundu Lissu amjibu Rais Kikwete

CONSTRUCTIVE THOUGHT

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2015
Posts
1,158
Reaction score
417
1.jpg

Siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kumtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amtaje mhusika wa Richmond anayezunguka naye kwenye kampeni, Mbunge huyo wa Singida Mashariki ameibuka na kudai kuwa Rais huyo ndiye mhusika kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka ya kuteua na kuwawajibisha mawaziri.

Juzi, akiwa Kigoma, Rais Kikwete alieleza kumshangaa Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mtu huyo anazunguka naye kwenye mikutano ya kampeni na kumtaka amtaje la sivyo yeye (Rais), atamtaja.

Akihutubia mkutano wa kumnadi mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, mwanasheria hiyo alianza kwa kusema: “Sasa ndugu zangu naomba leo nimjibu Kikwete na tumalizane na hii habari ya Richmond."

Alisema mkuu huyo wa nchi ndiye mhusika kutokana na mamlaka yake na; “si ya huyu Lowassa anayedai natembea naye kwenye kampeni. Hapa kwenye mkono wangu nina taarifa ya mwaka 2008 ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, sasa ni miaka zaidi ya saba tangu isomwe bungeni.”

Lissu aliyekuwa akishangiliwa na umati wa watu waliohudhuria mkutano huo katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege, alinukuu maelezo ya taarifa ya Mwakyembe kifungu kwa kifungu na kueleza namna ambavyo taarifa hiyo haikuweza kumtia hatiani Lowasa, bali aliwajibika kutokana na makosa ya watendaji wake.

Baada ya kueleza kwa kina taarifa hiyo, Mwanasheria huyo alisema Rais Kikwete ndiye pekee mwenye mamlaka ya kuwateua mawaziri, akisema alimteua Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha na ndiye mwenye mamlaka ya kuwawajibisha.

Karamagi na Dk Msabaha walikuwa wameshika uwaziri wa Nishati na Madini kwa nyakati tofauti wakati wa sakata la Richmond na walijiuzulu pamoja na Lowassa.

“Waziri mkuu Lowassa baada ya kutokea kwa sakata hilo alimwendea Rais Kikwete na kumweleza kuwa ‘kimenuka’ tuvunje mkataba baada ya wabunge wa upinzani kuchachamaa kuhusu sakata hilo, lakini alikataa na kumweleza kuwa hizo kelele za wapinzani zitaisha tu,” alisema.

Alisema baada ya Lowassa kujiuzulu mwaka 2008, tayari mashine za kutengeneza umeme zilishafika nchini na baada ya kujiuzulu haikufahamika zilikokwenda na kwamba baadaye mkataba wa Richmond ukahamishiwa kwa kampuni ya Dowans ambayo iliendelea kulipwa mabilioni ya shilingi.

Alimtaka Rais Kiwete awaambie Watanzania kwa nini Serikali yake iliendelea kuilipa Dowans mabilioni ambayo ilikuwa ya mfukoni na kwamba kama Lowassa alifanya makosa kwa nini hajapelekwa mahakamani kwa miaka minane tangu ajiuzulu.

“Rais Kikwete asitake kumaliza hizi siku chache za kampeni zilizobaki kwa shari na mimi na naomba niwaambie, Lowassa amefanya kazi katika umri wake wote wa miaka 62 ndani ya CCM na Serikali yake, lakini ameamua kuhamia huku kwa ajili ya kuleta mabadiliko na kuacha marupurupu yake yote,” alisema

Source: Oscar Aloyce - TANZANIA DEMOCRATIC REVOLUTION.
 
MAKAMBA:LOWASA ALIFUKUZWA KAZI,
HAKUJIUZULU!
Katibu mkuu mstaafu wa CCM luteni mst Yussuf Makamba amesema kuwa aliyekua Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa alikua ameshafukuzwa kazi kabla ya kujiuzulu.
Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais za CCM katika kiwanja cha Kawawa mjini Kigoma.
Akifafanua suala hilo mzee Makamba amesema kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM katika kikao kilichokaa mjini Dodoma, baada ya kuridhika kuwa Lowasa alihusika na kashfa ya Richmond,iliteua watu watatu kwenda kumuona Rais Kikwete kumueleza kuwa kwa maslahi ya nchi na chama amfute kazi Waziri Mkuu wake Edward Lowasa kwakua kamati ya uongozi imeridhika kuwa alimuita na kashfa ya Richmond na kulifedhehesha taifa.
Watu hao watatu walikua katibu mkuu wa CCM wakati huo mzee Makamba, mzee Samuel Malecela na mama Anna Abdallah.
"Tulipofika kwa Rais Kikwete tulikutana na Lowasa nje akitokea ndani kwa Rais, tukaingia na kumkuta bwana mkubwa. Tukapewa kahawa. Kisha tukamueleza kuwa tumetumwa na kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kuwa Waziri mkuu amehusika na kashfa ya Richmond na kwa heshima ya CCM na taifa amfukuze kazi.
Rais Kikwete akatuuliza,
...hamjakutana nae hapo nje?
Tukajibu...tumekutana nae anatoka...
Akasema...nimekwisha kumwambia kuwa kwa heshima ya taifa na CCM hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu tena na kwamba nateua waziri mkuu mwingine...
Makamba alisema kuwa baada ya Rais kumfukuza kazi Lowasa, kesho yake asubuhi Lowasa aliamkia bungeni na alipopewa nafasi ya kujitetea alisema tatizo nu uwaziri mkuu na kwamba amemuandikia barua Rais aachie ngazi.
"Ukweli ni kwamba Rais alishamfukuza kazi Lowasa usiku wa kuamkia siku aliyotangaza kiachia ngazi na kujiuzulu. Lakini tuliamua kumsitiri. Sasa kwakua kaamua kusema, nasi tumekuja kueleza akiba tuliyoweka."

Na Mwandishi wetu,
Kigoma
 
Duh! Lowassa habari zake zinachanganya
 
.
mbona umeacha maneno ya makamba katika utetezi wake wa kuitetea ccn alivyosema kuwa katibu mkuu alitaja mafisadi 11mwembe yanga Lowasa akiwa wa tisa?
kama hayo mafisadi alikua 11kwa muji ya makamba hivi yake 10 yaliyo ndani y ccm na mmoja aliyeondoka ni wapi uozo ulipoweka kichwa kama sii ccm yenye hao kumi?

Swali lako zuri.
 
Back
Top Bottom