Tundu Lissu akutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya chama cha Republican

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899

tundu Lissu akiwa kwenye ofisi za Chama Cha Republican- International Republican Institute.
Baada ya Lissu kufanya mdahalo chuo kikuu cha George Washington jana, leo amekutana na Sekretarieti ya chama cha Republican ambacho ndicho kinachoongoza seriiali ya Marekani.

Pia amefanya mazungumzo na viongozi wakuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch, ambapo amezungumzia matukio ya ukiukwa wa haki za binadamu nchini Tanzania kama vile kuuawa kikatili kwa Alphonce Mawazo, Aquilina Aquiline na makumi ya watu huko Kibiti.

Matukio ya watu kupotea kama Ben Saanane, Azory Gwanda etc, na matukio ya watu kutekwa na wengine kuuawa na kutupwa kwenye mifuko ya sandarusi ufukweni mwa bahari.

Pia amezungumzia sheria kandamizi zinazokiuka haki za binadamu kama vile sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ambayo inaingilia uhuru wa habari na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015, ambayo inatumika vibaya kukamata wakosoaji wa serikali.

Kesho Lissu amealikwa kwa mazungumzo na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambapo atakutana na Naibu Waziri John J. Sullivan pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa wizara hiyo.

Pia amealikwa kwenye kituo cha utangazaji cha Sauti ya Amerika (VOA) kwenye kipindi cha Straight Talk Africa, kinachoongozwa na mtangazaji nguli Shaka Salli. #LissuOnInternationalArena #SurvivedToTellTheTale
 
Mwambieni wanajua huko..na hayo matatizo wanajua hayako tanzania tu..ni afrika na dunia nzima..kupotea au kuuawa mtu mmoja mmoja ni kawaida..ila kama ni mauaji ya halaiki hilo ni swala jingine..au mtu kachinjwa hadharani na mamlaka za serikali hilo ni suala jingine.
Wazungu wanajua hizo ni changamoto za afrika..kenya waliuawa masheikh kwa kupigwa risasi..zanzibar waliuawa maaskofu kwa kupigwa risasi..kibiti waliuawa maafisa wa serikali( polisi) kwa kupigwa risasi..albino waliuawa sana..wazungu wanajua..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atulie auguze majeraha..hao waingereza na wamarekani hawakumpa hata sh kumi alipoumwa..akianza tena kuumwa watakaosumbuka ni serikali ya ujerumani..bora aende ujerumani akawashukuru wananchi na serikali kwa kutumia pesa za walipa kodi wa ujerumani kumtibia yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani umesikia tena mauaji huko kibiti..?waliyamaliza wazungu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…