Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
tundu Lissu akiwa kwenye ofisi za Chama Cha Republican- International Republican Institute.
Pia amefanya mazungumzo na viongozi wakuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch, ambapo amezungumzia matukio ya ukiukwa wa haki za binadamu nchini Tanzania kama vile kuuawa kikatili kwa Alphonce Mawazo, Aquilina Aquiline na makumi ya watu huko Kibiti.
Matukio ya watu kupotea kama Ben Saanane, Azory Gwanda etc, na matukio ya watu kutekwa na wengine kuuawa na kutupwa kwenye mifuko ya sandarusi ufukweni mwa bahari.
Pia amezungumzia sheria kandamizi zinazokiuka haki za binadamu kama vile sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ambayo inaingilia uhuru wa habari na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015, ambayo inatumika vibaya kukamata wakosoaji wa serikali.
Kesho Lissu amealikwa kwa mazungumzo na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambapo atakutana na Naibu Waziri John J. Sullivan pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa wizara hiyo.
Pia amealikwa kwenye kituo cha utangazaji cha Sauti ya Amerika (VOA) kwenye kipindi cha Straight Talk Africa, kinachoongozwa na mtangazaji nguli Shaka Salli. #LissuOnInternationalArena #SurvivedToTellTheTale