Tundu Lissu akutana na kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya chama cha Republican

..sawa.

..sasa kwanini Polisi wasiwakamate waliomshambulia TL?

..hudhani kwamba wakiwakamata TL hatakuwa na sababu ya kwenda kulalamika kwa wazungu?
Jibu swali langu then uje na lako.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
View attachment 1014891
tundu Lissu akiwa kwenye ofisi za Chama Cha Republican- International Republican Institute.
Baada ya Lissu kufanya mdahalo chuo kikuu cha George Washington jana, leo amekutana na Sekretarieti ya chama cha Republican ambacho ndicho kinachoongoza seriiali ya Marekani.

Pia amefanya mazungumzo na viongozi wakuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch, ambapo amezungumzia matukio ya ukiukwa wa haki za binadamu nchini Tanzania kama vile kuuawa kikatili kwa Alphonce Mawazo, Aquilina Aquiline na makumi ya watu huko Kibiti.

Matukio ya watu kupotea kama Ben Saanane, Azory Gwanda etc, na matukio ya watu kutekwa na wengine kuuawa na kutupwa kwenye mifuko ya sandarusi ufukweni mwa bahari.

Pia amezungumzia sheria kandamizi zinazokiuka haki za binadamu kama vile sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ambayo inaingilia uhuru wa habari na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015, ambayo inatumika vibaya kukamata wakosoaji wa serikali.

Kesho Lissu amealikwa kwa mazungumzo na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambapo atakutana na Naibu Waziri John J. Sullivan pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa wizara hiyo.

Pia amealikwa kwenye kituo cha utangazaji cha Sauti ya Amerika (VOA) kwenye kipindi cha Straight Talk Africa, kinachoongozwa na mtangazaji nguli Shaka Salli. #LissuOnInternationalArena #SurvivedToTellTheTale

Tangu lini IRI ikawa ndio Sekretarieti ya Republican Party? Unajua ulichooandika au umepewa memo na wewe ukaanza kugonga keyboard?
 
Sasa hivi mnajidai anayoongea Lissu hayana mana ,subirini mtakapoenda kutembeza bakuri halafu likarudi tupu ndio Lumumba na Jiwe wenu akili itawasogea .
 
..sawa.

..sasa kwanini Polisi wasiwakamate waliomshambulia TL?

..hudhani kwamba wakiwakamata TL hatakuwa na sababu ya kwenda kulalamika kwa wazungu?

Waliomshambulia wako Brussels, wakiongozwa na yule dereva na sasa wanatembeza kila kona.
 
View attachment 1014891
tundu Lissu akiwa kwenye ofisi za Chama Cha Republican- International Republican Institute.
Baada ya Lissu kufanya mdahalo chuo kikuu cha George Washington jana, leo amekutana na Sekretarieti ya chama cha Republican ambacho ndicho kinachoongoza seriiali ya Marekani.

Pia amefanya mazungumzo na viongozi wakuu wa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch, ambapo amezungumzia matukio ya ukiukwa wa haki za binadamu nchini Tanzania kama vile kuuawa kikatili kwa Alphonce Mawazo, Aquilina Aquiline na makumi ya watu huko Kibiti.

Matukio ya watu kupotea kama Ben Saanane, Azory Gwanda etc, na matukio ya watu kutekwa na wengine kuuawa na kutupwa kwenye mifuko ya sandarusi ufukweni mwa bahari.

Pia amezungumzia sheria kandamizi zinazokiuka haki za binadamu kama vile sheria ya huduma ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ambayo inaingilia uhuru wa habari na sheria ya makosa ya mitandao ya mwaka 2015, ambayo inatumika vibaya kukamata wakosoaji wa serikali.

Kesho Lissu amealikwa kwa mazungumzo na Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, ambapo atakutana na Naibu Waziri John J. Sullivan pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu wa wizara hiyo.

Pia amealikwa kwenye kituo cha utangazaji cha Sauti ya Amerika (VOA) kwenye kipindi cha Straight Talk Africa, kinachoongozwa na mtangazaji nguli Shaka Salli. #LissuOnInternationalArena #SurvivedToTellTheTale
Katika yoooote...eti wale ndugu zetu na askari wa Kibiti waliuawa na Serikali?
Nilimsikia Lissu BBC HT na DW na nikapatwa na ukakasi
 
Hivi huko ufipa hamna hata mmoja mwenye AKILI?Kila swali mnaloulizwa majibu ni lisu mara camera mara hajapewa matibabu. Unaulizwa ni nchi gani iliwahi kutatuliwa mattz yao na wazungu,we unakuja na habari za lisu.We ni MPUMBAVU KIWANGO CHA SGR.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Acha kupaniki wewe hapa ni sehemu ya mijadala usitake kulazimisha watu wote wafanane na wewe kifkra

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kupaniki wewe hapa ni sehemu ya mijadala usitake kulazimisha watu wote wafanane na wewe kifkra

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli hii ni sehemu ya mijadala na hatuwez kuwa sawa KIFIKRA. Ukiulizwa swali inatakiwa ujibu swali kama ulivyo ulizwa na hii ndio principle ya MIJADALA MINGI YA KISOMI. Unaulizwa hiki nawe unakuja na swali lingine tofauti kabisa,wat if nami nikija na swali lingine nawe hivo hivo?Je utakua mjadala huo?Unaulizwa kuna nchi iliyowahi kutatua tatizo lake kwa msaada wa mzungu?We unakuja na swali kwanini serikali haifanyi uchunguz swala la lisu.Haya ndio majibu sahihi?Mkiitwa Nyumb****** tunakosea?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Hilo tu ndio likufanye upaniki?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna nilipopanic mkuu sema nimeona ndio staili ya vijana wa ufipa kwa kila unachomuuliza. Yaani hata umuulize swali gani,Jibu lake linaishia na kiulizo na ubaya swali lenyewe linakuwa la kipuuzi. Bavicha yyt saiz kichwani kakariri CCTV, walinzi walitolewa, Kwanini hamjampa matibabu, kwanini mlimpiga risasi. Yaani tayari haya majibu yashaandaliwa, so ukimuuliza kwanini hiki kiko hivi tegemea naye akuulize hayo maswali juu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Naelewa Lissu anachokifanya lakini nahofia hatma ya anachokifanya.
 
Yaani Lissu anaongea na chama tawala cha Marekani? Chama cha Trump eeee hii sasa si mchezo..
 
Mwambieni wanajua huko..na hayo matatizo wanajua hayako tanzania tu..ni afrika na dunia nzima..kupotea au kuuawa mtu mmoja mmoja ni kawaida..ila kama ni mauaji ya halaiki hilo ni swala jingine..au mtu kachinjwa hadharani na mamlaka za serikali hilo ni suala jingine.
Wazungu wanajua hizo ni changamoto za afrika..kenya waliuawa masheikh kwa kupigwa risasi..zanzibar waliuawa maaskofu kwa kupigwa risasi..kibiti waliuawa maafisa wa serikali( polisi) kwa kupigwa risasi..albino waliuawa sana..wazungu wanajua..

Sent using Jamii Forums mobile app

Unaofanya huo ni UTAPELI. Unalipwa elfu 7 kila siku ili utetee kwa hoja nzitonzito sio hizi.. Unawatapeli waliokulipa. Tendea haki malipo hayo mkuu
 
Back
Top Bottom