PreGE2025 Tundu Lissu akamatwa na Polisi akielekea Mbinga, Ruvuma

PreGE2025 Tundu Lissu akamatwa na Polisi akielekea Mbinga, Ruvuma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
780
Reaction score
1,831
Jeshi la Polisi limepiga mabomu na kumkamata Tundu Lissu muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake huko Mbamba Bay mkoani Ruvuma sasa hivi.

Screenshot_20250409_185605_Instagram.jpg

TAARIFA KUTOKA CHADEMA
BreakingNews Mwenyekiti wa Chama wa Taifa Mhe. Tundu A. Lissu amekamatwa na Jeshi la Polisi wilaya Mbinga. Mhe. Lissu amekamatwa wakati alipomaliza mkutano wa hadhara uliofanyika leo tarehe 09 Aprili 2025 Jimbo la Mbinga, mpaka sasa haijulikani amepelekwa kituo gani cha Polisi. Mwenyekiti amekamatwa pamoja na wanachama wengine, kwa sasa Jeshi hilo linaendelewa kutawanya wananchi kwa mabomu uwanjani hapo.

--

VIDEO: Muda mchache kabla ya Lissu kukamatwa​

Muendelezo Wa Taarifa Iliyotolewa Na Godbless Lema Kuhusu Kukamatwa Kwa Tundu Lissu

Baada ya mkutano leo jioni saa 12:00 wilaya ya Mbinga, wakati wa kufunga mkutano OCD alimfuata Mwenyekiti Tundu Lissu Jukwani akamwambia tafadhali ukishuka hapo jukwani Ingia kwenye gari ya Polisi nakutaka Polisi kwa mahojiano.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Baadhi wa wananchi waliofika kwenye mkutano huo wadaiwa kujeruhiwa wakati polisi wakitawanya wananchi​

Mh Lissu alimwambia nimefanya nini ? Huku akiendelea kuchangisha fedha ktk hadhara ‘ Tone Tone. baada ya kuona hiyo zogo , Kamanda Sosopi alimfuata OCD nakumwambia kama Lissu analo jambo na nyie pls mnaweza kuja pale tulipofikia mkamchukua kwa utaratibu hapa mtazua tafrani kubwa maana halaiki hapa ni kubwa,

Pia Mimi nilisisitiza Ushauri huo kwa OCD na wasaidizi wake wengine, alionekana kama anaelewa lakini ghafla mabomu ya machozi mengi yalianza kurindima.

Mh Lissu amekamatwa na sasa yuko kituo cha Polisi Mbinga.
 

Attachments

  • 1744220929333.jpg
    1744220929333.jpg
    80.9 KB · Views: 22
Ma CCM sasa uvumilivu umeshayashinda, yameanza hekaheka mapema!
 
Tundu Lisu anatoa hoja. wao wanaleta VITOJA kuna wanaomuita MWANAHARAKATI, hawajui kwamba walio wengi wanavutiwa na siasa za harakat.
huyu ndiyo Tundu LISU mwana wa Tanganyika akisema chawa wote wana ufyataaaaa
anapaswa kufuata sheria mikutano mwisho saa 12, hii saa moja anafanya nini? akifa mtu tunampeleka ICC
 
Anaandika John Heche Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,.

Nimepewa taarifa ya kukamatwa kwa mhe Tundu Lissu Mwenyekiti wetu wa chama Taifa... mda huu huko Mbinga, tunafuatilia na tutatoa taarifa kamili ya tukio mda sio mrefu.

Lolote baya likimtokea Mwenyekiti serikali inawajibika kwa asilimia 100.
 
Back
Top Bottom