Uchaguzi 2020 Tundu Lissu aendelea na kampeni katika viwanja vya Bank, Mombo Korogwe vijijini na viwanja vya Mwanjani Tanga

Uchumi wa Mombo umeuliwa na CCM kufungia Mabasi kusafiri Usiku
Badala ya kudhibiti Majambazi wanawazuia Wananchi wasisafiri Usiku
Iko TRENI wewe acha uzushi.Halafu toka Mombo hadi dar unafika mchana kweupe ukitaka usiku panda treni.Huelewi hata kinachoendelea nchi hii uko gizani kabisa.
Huelewi kuwa treni upo usiku?
 
ndege kanda ya ziwa zinabeba samaki kupeleka ulaya na abiria wanaozipanda hubeba samaki kibao wa mwanza kuja nao Dar es salaam mbona kule anazipiga vita wakati ndege huwasaidia soko la samaki zao watu walioko kule ambao wengi ni wavuvi na wafanyabiashara za samaki?

Taabu ilani yao iliandikwa ulaya sasa muda unayoyoma ndio akili zinaanza kumrudia!!

Anakumbuka shuka wakati kumekucha!!!

..lakini ni makosa kutumia 490 billions kununua midege toka kwa mabeberu wakati hatujatatua matatizo ya msingi ya wananchi kama upatikanaji wa maji safi na salama. hiyo ndiyo dhana nzima ya maendeleo ya vitu vs maendeleo ya watu.
 
Lissu keshapoteza sifa za kuwa Rais wa nchi hii.

Mizunguko yote anatukana tu.
Kama kwenye mikutano yake inajumuhisha maelfu ya wasikilizaji,ilhali anahubiri matusi basi wanaomsikiliza wanayapenda matusi.
Aendelee kutukana.
 
NEC kuweni makini Chadema wamesha ona kipigo kizito ndani ya sanduku la kura wanatafuta mtu wa kumrushia Lawama msipoangalia wanaweza susia uchaguzi dakika yoyote kutoka sasa ili Lawama ziwe juu yenu.
 
Picha za angle!
CCM wangekosa akili na kutumia muda mwingi kuaminisha kwa picha, hata bila kuchuja na kutupia 'za angle' , mass media zisingetosha kwa mapicha!
 
Inaelekea hauko theoretically equipped juu suala hili unalotaka kulijadili.
 
Ona utapeli wa Lisu si alisema hahitaji maendeleo ya vitu?
Wewe ndo huelewi na hutaacha kuweweseka! Hapo amesema maendeleo ya watu, kwamba kwa Mombo jambo la msingi ni maji na siyo ndege! Anacho Sema Lissu ni, vipaumbele, mfano; Chato wanaitaji maji na siyo uwanja wa ndege au uwanja wa mpira!!
 
Wacha uongo.. Kuna bombardier yoyote inapeleka samaki ulaya?!
kaipande toka mwanza uone watu wanavyobeba samaki.Ndege zinazopeleka samaki kwa sasa ni za mizigo za Rwanda na za ulaya.Sasa ukimwambia msukuma ndege hazina faida wakati anaziona zinabeba samaki kupeleka ulaya na Magufuli kaahidi kununua ndege za mizigo ili ziwe zetu ndio zinabeba wanakuona mjinga tu

Hoja ya kuponda ndege itaenda kumuomyesha cha mtema kuni LIsu usukumani wana hasira naye ya kufa mtu.Sehemu zote za starehe agenda ni hasira waliyonayo kuziponda ndege alikoongelea kanda ya ziwa.

Tarehe 28 october maeneo wanaojua umuhimu wa ndege yafuatayo ajiandae kupigwa chini

Watu wanaoelewa umuhimu wa ndege ni mikoa ifuatayo

1.Mikoa ya kanda ya ziwa yote
2.Dar es salaam
3.Mikoa ya kanda ya kaskazini ambayo ni KILIMANJARO ,ARUSHA NA manyara
4.Mbeya
5.Zanzibar

Hiyo mikoa Chadema wajiandae kufunga virago.Hoja moja iliyowaporomosha ni Lisu kuponda ndege sababu ni wapanda ndege maarufu na ndege hufurika sana huko kwa ajili ya watalii na mizigo zikiwemo za Air Tanzania

Mikoa hiyo ndiko kipigo cha mbwa koko kitatokea kwa mbelgiji Tundu LISU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom