Tundu 'Frankenstein' Lissu

Nyomi?

Anafikia hata robo ya lile la Slaa 2010 na Lowasa 2015

Anafika vizuri sana, labda useme kwamba wakati ule ulikuwa na idadi kamili, na sasa una idadi kamili. Kinyume na hapo ni wivu kama wivu mwingine. Na isitoshe wakati wa Slaa na Lowassa hakukuwa na ndege, flyover, bwawa la umeme, reli, na wala hakukuwa na Katazo la kufanya siasa kwa wapinzani kama sasa.
 
Aaaaah nyie watesi wa lissu mnateseka sana.
 
Wacha kiherehere! Unadandia usiyoyafahamu! Mbona huyu ndiye amekuwa akisema eti Tundu Lissu anajitafutia umaarufu? Na wewe una akili fupi pia?
Wapi nimesema Tundu Lissu anajitafutia umaarufu?
 
Hatimaye, three years later utabiri wako unatimia. Lissu amepona na kurudi Tanzania, na mbaya zaidi amekuwa zaidi ya tishio kwa Magufuli na Serikali.

Watanzania wanampenda zaidi na anaenda kuwa Raisi wa Tanzania kwenye uchaguzi wa October 2020
Lisu kuwa Rais wa Tanzania sio rahisi na haitakuja kutokea
 
Wewe ni Mafiga Matatu no. 2 hapa Jamiiforums. Mafiga Matatu no.1 aliandika mambo 2012 yanayotabiri aina ya serikali itakayofuata baada ya Kikwete kuwa itakuwa katili na pia alitabiri 4 possible candidates akiwemo Magufuli. In short akipita mulemule.

Sasa wewe naye haya maandishi uliyaandika 2017 kuhusu Lisu na ugumu wa serikali ya John kumdhibiti atakaporejea. Na ndiyo tunayaona.

Big up man. Ulipita mulemule.
 
Naombea mambo yawe hivyo hivyo kama ulivyoandika, hatuwezi kutaliwa na lichama limoja miaka nenda rudi hadi watu wanajisahau.
 

Haya mahesabu nimekupa vizuri kwenye uzi ule.
 
Nyomi?

Anafikia hata robo ya lile la Slaa 2010 na Lowasa 2015
Acha presha na papara mkuu na uwe mwepesi wa kuelewa. Umemsoma niliyemquote? Umeelewa kwa mujibu wa maelezo yake Tundu Lissu angekuwa wapi?

Nimesema hivyo ili kumrudisha ajisome na ajidharau sana kwa kujaribu kuingilia majukumu ya Mungu lakini Mungu amemuinua aliyemtabiria kuwa 'its over' sasa si tu its not over, wala si kushindwa kuinuka tena, bali anatembea bila hata magongo na anakusanya nyomi kila anapokwenda.

Sijaja kushindanisha nyomi la fulani na la fulani na la fulani lipi kubwa.
 
Mkuu tindo, kwanza nikupongeze kwa kuwa mfuasi kindakindaki wa CHADEMA na hasa Lissu. Hongera za dhati.

Je, unamshauri ajiandaeje, kampeni zikianza, kuhusu mambo kadhaa ikiwemo:
√ Sera na Mikakati mbadala ya maendeleo badala ya kung'ang'ania shutuma dhidi ya Serikali na viongozi wake, hasa Rais Magufuli na viongozi wa dini;
√ Kujibu tuhuma za ufisadi ndani ya chama chake dhidi ya M/Kiti wake, kama zilivyotolewa na zitaanikwa upya, wakati wa kampeni, na wanasiasa waliokihama chama;
√ Ushindani dhidi ya wagombea Urais wa vyama vingine vya upinzani ambao wanatofautiana kwa mbali na jinsi anavyojinasibu kwa wapiga kura, kuelekea kampeni za Uchaguzi Mkuu;
√ Ukimya wa Jeshi la Polisi kuhusu shambulio lilolenga kuondoa uhai wake; na
√ Kesi zake ambazo wadhamini walijiondoa, hivyo kisheria dhamana imefutwa. Isitoshe mara mwisho hakuhudhuria mahakamani kwa kisingizio za kiafya, lakini ameonekana akishiriki shughuli za kisiasa tofauti na hayo madai.

FUMBO MFUMBIE MJINGA ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…