Tundu 'Frankenstein' Lissu

Naona unaandika kwa furaha Kweli Kweli,nyie watu ni mashetani!
 
Wow!

I wrote this almost 3 years ago!

So prescient....

JokaKuu unaikumbuka hii mada?

Nilichokisema hapa ndicho hichi kinachotokea sasa hivi.

Nakumbuka wewe ulinishambulia kwa sababu nilitumia mfano wa Frankestein.....
 
Bado unaamini maneno yako haya Mkuu?
 
Wow!

I wrote this almost 3 years ago!

So prescient....

JokaKuu unaikumbuka hii mada?

Nilichokisema hapa ndicho hichi kinachotokea sasa hivi.

Nakumbuka wewe ulinishambulia kwa sababu nilitumia mfano wa Frankestein.....

..basi mimi nakutaka radhi.

..unajua TIME heals a lot of things.

..labda wakati ule tulikuwa ktk machungu ya TL kujiuguza, hivyo emotions zikatawala hoja zangu.

..lakini kila nikimuangalia TL kuna kitu sijisikii vizuri.

..Nilimuona akielekea kwenye kaburi la Mzee Ndesamburo, jinsi alivyokuwa akitembea, ilinisikitisha sana.
 
Uliona mbali
 
Naam!

Kwa kweli ukimuangalia tu jinsi alivyo sasa hivi, kama wewe ni binadamu wa kawaida, ni lazima ujawe na simanzi.

Kapewa kilema cha maisha.

Licha ya madhila yote hayo, bado anaonekana ni mtu mwenye bashasha tele, ari, na nguvu mpya.

Na kwa jinsi alivyo sasa, serikali ya CCM naona haijui hata ikabiliane naye vipi.

Nani kwa mfano atathubutu kwenda kumkamata na kumpa misukosuko? Ataanzia wapi huyo mtu?

Zamani kabla ya yale madhila ya kupigwa risasi, alikuwa akikamatwa kamatwa sana na kuwekwa ndani kwa sababu uchwara.

Sasa hivi sidhani kabisa atapewa misukosuko kama hiyo.

CCM wenyewe ndo ‘wamemtengeneza’ Lissu na sasa hawajui namna ya kumdhibiti.

Hence ule mfano wa mimi kutumia Frankenstein na yule mwanasayansi aliyemtengeneza na mwishowe kutojua jinsi ya kumdhibiti.

Sikuwa namwita Lissu ‘Frankestein’. Ulikuwa ni mfano tu wa mazingira yaliyowatengeneza.
 
Daah watu wamefukua kaburi ila nyani uliona mbali, na kweli karejea na anaendeleza alipoishia, moto anauwasha kweli kweli

All in all Lissu ni mwanaume wa shoka, mwamba kweli kweli ni jasiri sana, sikutarajia kama angerejea Tanzania ya Magufuli isitoshe na ujasiri ule ule kama hakuna kilichomkuta uko nyuma

Kuna siku Lissu alikamatwa akapelekwa Central, kipindi hicho Lissu alikua na makesi kibao, wandishi wakamuliza Mkewe kuhusu misimamo ya Lissu kwamba ndio inam'cost, mkewe akajibu huyu ndio Lissu anayemfaham toka ujanani wao, akaendelea akasema siku Lissu akibadilika akapiga magoti kwa watawala yeye atakua wa kwanza kudai talaka, nilishangaa kauli ile ya mkewe
 
..wamdhibiti kwa hoja.

..Ila some ppl are so misguided wanaamini kwamba matumizi ya vyombo vya dola na mabavu ni njia halali za kumdhibiti TL.
Aisee sasa hivi wakitumia mabavu kumdhibiti tunaweza kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na hata kutengwa na jumuia ya kimataifa.

Sasa hivi tu hali ya mahusiano yetu na mataifa mengine si nzuri.

Wakimfanyia mabaya Lissu itakuwa ni hatari sana kwa taifa.

Watumie hoja kupambana naye. Siyo nguvu.
 

..lakini ilikuwaje wasimpe hata matibabu?

..TL siyo mtu mgeni kwa watu wote wanaofanya maamuzi.

..halafu wengine wakaanza hata kumtukana na kumkejeli kwenye majukwaa na vyombo mbalimbali vya habari.

..Hata bungeni mawaziri na wabunge walitoa kauli zenye ukakasi mkubwa dhidi yake, and there was no voice of wisdom to tell them to stop.

..Sikuamini alivyopigwa risasi, lakini pia sikuamini ubaya aliotendewa baada ya hapo.

..What was Magufuli, Samia, Majaliwa, and Ndugai, thought process mara baada tukio, na wakati TL yuko unconscious Nairobi?
 
Mmh
 
Vipi kamanda je unakumbuka haya maneno yako?
 
Daaah weacha tu mkuu ..kweli m/mungu ni wa rehema ..kurudi kwa Lissu ni ishara tosha kuwa hata masiha atarudi
 
They botched the handling of the aftermath..

Na ndo maana watu wanawashuku kuwa wao [serikali ya CCM] ndo walihusika.

Lolote baya litalompata Lissu sasa hivi, serikali ya CCM itakuwa mshukiwa namba 1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…