Tundu A. M. Lissu hapuuziki

Tundu A. M. Lissu hapuuziki

MAKAMANDA gani wahuni mnatukana waasisi wa Taifa la Tanzania.

Hebu nisaidie maana ya "Wahuni" na "Uhuni", kama unaweza lakini!!....Baada ya hapa tutaanza kuwaorodhesha wahuni pamoja na uhuni wao!!
 
Lissu hajatumia busara kutoa maneno ya kashfa kwa waasisi wa Taifa hili na hilo limemshushia heshima sana.....

Kwann mnatumia waasisi kama kinga kwahyo kumbe lissu ana ongea ya kweli sema abadili kauli zake ccm watakubali marekebisho ya muungano
 
Lissu hajatumia busara kutoa maneno ya kashfa kwa waasisi wa Taifa hili na hilo limemshushia heshima sana.....

Kuna mtu alipita nje ya nyumba yetu na kuchukua nguo zote nilizokuwa nimeanika kisha akatokomea nazo kusikojulikana na hadi leo sijazipata hizo nguo. je nikimuita mwizi huyo mtu nitakuwa nimemkashifu? kwamba kumuita Profesa Lipumba msomi ni kumkashifu? kuuita ukweli kwa jina lake ni kashfa? unaijua tafsiri ya kashfa? je nikisema hii hujatumia busara kuandika hii comment ntakuwa nimekukashifu?
 
Wakati wa Bunge la Katiba Ndugu Lissu kabla ya kuanza kuchangia hoja ya ama serikali mbili au tatu alisikika akisema "aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi" aliporekebishwa na mwenyekiti aliyaondoa maneno hayo na kutumia mengine yanayofanana na hayo kimantiki yaani "aliyezoea kuishi kwa uongo hawezi kuwa mkweli". Mara baada ya utangulizi huo aliendelea kunukuu maandiko ya Dr. Mwakyembe, Prof.Shivji kuthibitisha kauli yake ya awali kwa kuonesha ukigeugeu wao kuhusu muundo muafaka wa muungano. Baadaye akanukuu mahojiano ya Mwl. Nyerere huko nyuma mara baada ya muungano aliposema kuwa Zanzibar walikuwa na uhuru wakuchagua ama kuendelea na muungano au la na Tanzania isingewalazimisha kwa mabomu na akalinganisha na maamuzi yaliyofanyika baadaye kumuondoa madarakani Ndg. Aboud Jumbe kama mfano wa ukigeugeu wa Mwalimu. Nadhani hili la mwisho ndio wapinzani wa Lissu wanalitumia kujenga hoja kuwa alimkosea heshima Hayati Baba wa Taifa.

Mfano: Umekuja mjini miaka zaidi ya 10 kutafuta maisha,then ukaamua kurudi kijiji kwenu mara baada ya kufika ukakuta msingi wa nyumba yenu ya enzi na enzi umepasuka na nyumba ina nyufu mpk ukichungulia ndani unaona mbavu za mzazi wako,sasa kwa aibu na kutaka kuweka mambo sawa ukaamua kubomoa huo msingi na kuanza ujenzi wa nyumba ya kisasa itakayo dumu zaidi ya miaka50 kwa akili ya kawaida hapo utakuwa ufanya kosa ama?
Nyumba hyo ina umri zaidi ya miaka 50 iliyopita na watoto mko 30 na ww ni mtoto wa pili toka mwisho ila kwa hekima na busara Allah kakumbusha kwenu maana mkataa kwao ni mtumwa

Sasa kwa ccm hii inaitwa kutukana muasisi wa huo msingi,kuwa yeye alikuwa na akili ndiyo maana alijenga nyumba nyenye nyufu na kuta zilizopasuka kwa hyo huna haja ya kuja kuikarabati,unamtia aibu mzazi wako,"unamtukana muasisi wa msingi huu" wewe ni tahira,huna adabu kabisa,umjini umekuharibu...

Hapa mpaka uwe na akili yako mwenyewe ndiyo waweza elewa mfano wangu lakini kwa akili za kushikiliziwa na bwana mkubwa daima huambulii kitu
 
kitendo cha tundu lisu kumtukana nyerere kimewakasirisha sana watanzania.. nipo hapa jimboni kwa lisu wapigakura wake wamekasirika sana
 
Ndugu yangu hakuna haja ya kutumia maneno ya kashfa ili kufikisha ujumbe wako. Msomi wa kweli ni yule anayeweza kuelezea dhana ngumu za kitaalamu kwa kutumia lugha ya staha na maneno rahisi yanayoeleweka kwa mtu yoyote hata yule ambaye hajaenda shule kabisa. Labda nikuulize je na wewe unakubaliana na dhana ya Lissu kuwa Mwalimu Nyerere alizoea vya kunyonga na vya kuchinja hakuviweza? Je Lissu alishindwa kupata maneno mengine rahisi na ya staha kuelezea kitu hicho bila kuanza na kashfa?
 
Lissu hajatumia busara kutoa maneno ya kashfa kwa waasisi wa Taifa hili na hilo limemshushia heshima sana.....

Another sweeping statement intended to provide collective cleanliness!

Yaani unadhani nchi hii kuna ´watu ambao hatutakiwi kusema kashfa zao? Au hukumaanisha kashfa? Kashfa? Waasisi kitu gani wewe? Tunalazimisha watu fulani wawe watakatifu!

Wengine walikuwa wabakaji. leo eti ni waasisi tusiseme kashfa zao! utoto huo ndani ya JF.
 
Ndugu yangu hakuna haja ya kutumia maneno ya kashfa ili kufikisha ujumbe wako. Msomi wa kweli ni yule anayeweza kuelezea dhana ngumu za kitaalamu kwa kutumia lugha ya staha na maneno rahisi yanayoeleweka kwa mtu yoyote hata yule ambaye hajaenda shule kabisa. Labda nikuulize je na wewe unakubaliana na dhana ya Lissu kuwa Mwalimu Nyerere alizoea vya kunyonga na vya kuchinja hakuviweza? Je Lissu alishindwa kupata maneno mengine rahisi na ya staha kuelezea kitu hicho bila kuanza na kashfa?

Hayo maneno uliyo ya bold yanatamkwa na viongozi wako wa ngazi za juu kbs ndani ya chama chako pendwa,mie nimenukuu tu

Jibu la swali lako:
Neno kunyonga lina maana pana sana,serikali yetu ina sheria ya hukumu ya kifo"kunyongwa hadi kufa" iko halali kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yetu(lingekuwa tusi sheria isingelitambua)

Pili: Tundu alitumua maneno yale(vya kunyonga,ambalo sio tusi kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili,ikisindikizwe na sheria za nchi) ili ccm waelewa vizuri kwa vile wamekuwa wagumu wakuelewa maneno mengine yote na lengo la lissu sio kubomoa bali kurekebisha

Maneno hayo yapo mtaani,john komba na khadija kopa huyatumia kwenye nyimbo zao(sio matusi) labda kwa kiswahili sanifu uniambie ni maneno makali hapo utanilegeza kidogo japo nyie bila kupelekeshwa hamtaipeleka hii nchi kunakostahiri daima

Tatu: Neno "Kashfa" kama maneno "mwalimu hakuwa malaika bali ni binadamu kama sisi ndiyo maana leo tunamkosoa ili kudhihirisha ubinadamu wake" ni kashfa bs Mungu atamhukumu lissu kulingana na maneno yake japo mwalimu katika kitabu chake cha tujisahihishe alishawahi kusema" Kiongozi asiyekosolewa sio kiongozi" akasema tena " ccm sio baba yangu wala mama yangu" alikuwa binadamu ndiyo maana alikuwa akiona makosa yake baadhi na kuyasahihisha leo tindu lissu anataka tusahihishe makosa ya mwalimu ili tusonge mbele kama Taifa na sio ccm wala Ukawa...Wabheja sana
 
Nimegundua kuwa una matatizo makubwa kuliko nilivyodhani awali. Hunifahamu kwa sura wala msimamo wangu wa kisiasa lakini tayari umehitimisha kuwa mimi ni mwanachama au mfuasi wa chama ulichokibatiza jina la "Chama Pendwa" ambacho wala sikijui. Ni kweli neno kunyonga lina maana pana. Ila kama wewe ni mswahili mzuri utajua kuwa ili kuelewa maana halisi ya mtumiaji wa msemo wenye maneno yenye maana pana kama hilo huna budi kuangalia muktadha wa matumizi ya neno husika. Lissu hakuwa akiongelea kunyonga unakoongelea wewe alitumia neno hilo kama sehemu msemo wa kiswahili wenye maana tofauti na uavyosomeka au kusikika. Ndio maana Mwenyekiti alipomtaka aondoe maneno hayo hakubisha bali aliyabadilisha ili kufikisha ujumbe wa ni nini hasa alimaanisha alipotumia maneno hayo hapo awali. Hata wasanii kama huyo Hadija Kopa wanapotumia msemo huo huwa wanalenga kufikisha ujumbe kwa walengwa kama sehemu ya mipasho ya taarab. Huwa hawaongelei hukumu ya kimahakama ya mhalifu kunyongwa hadi kufa. Kwa ufupi Lissu hakutumia busara kuchagua msemo huo kumsema Mwl. Nyerere. Angeishia kwa Dr. Mwakyembe na Prof Shivji asingekuwa ameharibu. Kitendo cha kumhusisha Mwl Nyerere amewapa wapinzani wake silaha ya kumshambulia yeye binafsi na kufifisha ujumbe mkuu Lissu aliotaka kuwafikishia wananchi hasa wapenzi wa serikali tatu.
 
Hebu eleza ametoa kashfa gani ili nasi tufahamu. Msiishie kusema katukana au kakashfu waasisi bila kutaja ni tusi gani au kashfa gani!
 
Nimegundua kuwa una matatizo makubwa kuliko nilivyodhani awali. Hunifahamu kwa sura wala msimamo wangu wa kisiasa lakini tayari umehitimisha kuwa mimi ni mwanachama au mfuasi wa chama ulichokibatiza jina la "Chama Pendwa" ambacho wala sikijui. Ni kweli neno kunyonga lina maana pana. Ila kama wewe ni mswahili mzuri utajua kuwa ili kuelewa maana halisi ya mtumiaji wa msemo wenye maneno yenye maana pana kama hilo huna budi kuangalia muktadha wa matumizi ya neno husika. Lissu hakuwa akiongelea kunyonga unakoongelea wewe alitumia neno hilo kama sehemu msemo wa kiswahili wenye maana tofauti na uavyosomeka au kusikika. Ndio maana Mwenyekiti alipomtaka aondoe maneno hayo hakubisha bali aliyabadilisha ili kufikisha ujumbe wa ni nini hasa alimaanisha alipotumia maneno hayo hapo awali. Hata wasanii kama huyo Hadija Kopa wanapotumia msemo huo huwa wanalenga kufikisha ujumbe kwa walengwa kama sehemu ya mipasho ya taarab. Huwa hawaongelei hukumu ya kimahakama ya mhalifu kunyongwa hadi kufa. Kwa ufupi Lissu hakutumia busara kuchagua msemo huo kumsema Mwl. Nyerere. Angeishia kwa Dr. Mwakyembe na Prof Shivji asingekuwa ameharibu. Kitendo cha kumhusisha Mwl Nyerere amewapa wapinzani wake silaha ya kumshambulia yeye binafsi na kufifisha ujumbe mkuu Lissu aliotaka kuwafikishia wananchi hasa wapenzi wa serikali tatu.

Kwani ujumbe aliotaka kuufikisha si ulifika ndo maana alibadili neno alipoambiwa aondoe neno hilo? Ndio maana ulisikia yote hayo. Lakini pia, hakuufikisha ujumbe ambao wewe na wenzako mlitaka kuusikia kwa busara zenu. Mtu anao uhuru wa kusema lolote ili mradi havunji sheria. Elezea ni sheria gani inazuia misemo hiyo tumfikishe kwa pilato.
 
kitendo cha tundu lisu kumtukana nyerere kimewakasirisha sana watanzania.. nipo hapa jimboni kwa lisu wapigakura wake wamekasirika sana
Unajuaje kama hao uliokuwa nao walimpigia Lissu, kuchaguliwa kwa mtu hutokana na wengi kumpa kura za kumkubali lakini waliomkataa pia wapo, mfano ni hao uliokuwa nao.
 
Kwani ujumbe aliotaka kuufikisha si ulifika ndo maana alibadili neno alipoambiwa aondoe neno hilo? Ndio maana ulisikia yote hayo. Lakini pia, hakuufikisha ujumbe ambao wewe na wenzako mlitaka kuusikia kwa busara zenu. Mtu anao uhuru wa kusema lolote ili mradi havunji sheria. Elezea ni sheria gani inazuia misemo hiyo tumfikishe kwa pilato.
Ndugu Kubinika naona umedandia gari kwa mbele bila kujua linatoka wapi na kuelekea wapi. Mimi ninaongea mawazo yangu sijatumwa na mtu yoyote, simwakilishi mtu yeyote na wala sina mwenzangu JF forum. Hapa hatuongelei kuvunjwa kwa sheria nakushauri ufuatilie upya mjadala ili uweze kutoa hoja zinazoendana na mada husika.
.
 
Watanzania tunahitaji viongozi wa kweli na sio wale wanaopijdisha ukweli kwa maslahi yao, naomba nimtambue Lissu ni jasiri!

Sisi wazanzibar hatumwoni mtu wa ajabu Lissu bali tunamwona kiongozi shujaa na kwa upande mwingine ni mtetezi wa Wazanzibari.

Baadhi ya viongozi Zanzibar wanaogopa kusema ukweli kwa kulinda masilahi yao, lakini wakumbuke tu kamwe kuuficha ukweli, kwa sababu ukweli siku moja utajulikana tu.

Tunakupongeza sana Lissu na kwa mtazamo wangu siku moja utakuwa katika historia nzuri ya kuwatetea Wazanzibar.

Saumu Said
Znz
 
Back
Top Bottom