๐—ง๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐˜„๐—ฒ๐˜‡๐—ฎ ๐—ธ๐˜‚๐˜๐—ฎ๐—ณ๐˜‚๐˜๐—ฎ ๐—ง๐˜ƒ ๐—ถ๐—น๐—ถ๐˜†๐—ผ๐—ฝ๐—ผ๐˜๐—ฒ๐—ฎ!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
Unarudi nyumbani toka kwenye mihangaiko yako unatufungua mlango kuingia ndani Tv hakuna nani kachukua hujui? Utafanyaje?

20230712_123313.jpg


Je Kuna njia tunaweza tumia ku track Tv iliyoibiwa ? Na kumkamata mwizi ??

Hakuna njia ramsi ya kuweza kuifuatilia Tv yako ikitokea imeibiwa kama haijafungwa mfumo wa Gps tracker, ila unaweza kuifuatilia kutokana na app zilizopo mule ndani ikitokea muhusika ameunganisha na intaneti kwenye Tv.

Apa tutaweza kuifuatilia Tv kupitia njia Online baada ya kuibiwa Tv na kuanza kutumika kwaiyo lazima Tv iwe On na iwe imeunganishwa na intaneti.

View attachment 2685693

1) ip address
Inabidi huwe na ip address ya Tv yako Ili polisi waweze kukusaidia kuitafuta tv yako baada ya kuibiwa au kupoteza. Polisi wtakusaidia kuifuatilia au mamlaka yoyote nyingine inayohusika na kesi za utapeli , wizi kupitia Ip address ya Tv yako.

Ni muhimu huwe na
โ€ข Tv serial number
โ€ข Jina la Tv na model yake
โ€ข Gharama uliyonunulia Tv pamoja na Risiti
โ€ข ip address

View attachment 2685691

2) Google
Google wametengeneza njia kadhaa ya kuwasaidia watumiaji wake kuweza kujilinda dhidi ya uhalifu wa mitandao au mitaani nk ivyo inawapa watu nguvu ya kuweza kufuatilia vifaa vyao vilivyopotea kwa namna moja au nyingine.

View attachment 2685694

Kuna feature ya kukusaidia ku track na kutambua kifaa kilijiunganisha na kifaa chako, location yake Iko maeneo Gani mfano (Samsung smart tv)pia utaweza kujua mkoa au nchini Gani ipo nk.
  • fungua simu au kompyuta ingia Google
  • kisha login kwenye Google Akaunti yako kupitia browser ingia kwenye Google secure.
  • tafuta Tv yako kwenye list of devices,ata kama muhalifu ata log out kwenye Akaunti yako
3) Netflix
Kupitia mtandao wa Netflix ni njia Rahisi ya kuweza kufuatilia Smart Tv yako iliyopotea utaweza kupata taarifa nyingi sana kupitia Akaunti yako.

smarttv2%20%E2%80%93%202.jpg


Taarifa muhimu kuanzia mda na siku ambayo account yako imetumika , ip address na location ya kifaa eneo liliopo. Kwaiyo ikitokea jamaa akaingia kwenye Akaunti yako ya Netflix unaweza kumkamata.

- chukua kompyuta ingia Google tafuta Netflix ingia kwenye Akaunti na email ile ile Kisha chagua Any profile

- juu kwenye profile menu upande wa kulia mwa skrini yako chagua account Toka menu ya chini Kisha ingia setting

- chagua recent device streaming activity utaweza kuona vifaa vyote ambavyo vimeingia kwenye Akaunti yako ya Netflix utaweza kuona ip address pamoja na location.

Toa taarifa kwa watengezaji / wasambazaji wa Tv uliyopoteza au kuibiwa watakusaidia kuweza kuifunga au kuifuatilia Tv yako iliyopotea au kuibiwa.

Ebu tuambie ukibiwa Tv huwa unafanya nini kuifuatilia au umeshawahi kuibiwa Tv tuachie maoni yako? View attachment 2685692
 
Ukiibiwa TV kibongobongo imetoka iyo..Njia zote ulizoweka zinahitaji Internet connection..sasa unafikiri alieiba anaweza kuconnect na internet??Au ataishia tu kuchomeka flash na kisimbuzi...

BTW unaweza kulinda TV yako kwa kupachika GPS ni chip ndogo sana zinapatikana Ebay,Alibaba,Amazon n.k unaita fundi wiring anakuwekea ndani ya TV apo mwizi akijimix kaisha

Ila mambo ya IP,risiti sjui netflix sijui google UTASUBIRI SANA
 
Ukiibiwa TV kibongobongo imetoka iyo..Njia zote ulizoweka zinahitaji Internet connection..sasa unafikiri alieiba anaweza kuconnect na internet??Au ataishia tu kuchomeka flash na kisimbuzi...

BTW unaweza kulinda TV yako kwa kupachika GPS ni chip ndogo sana zinapatikana Ebay,Alibaba,Amazon n.k unaita fundi wiring anakuwekea ndani ya TV apo mwizi akijimix kaisha

Ila mambo ya IP,risiti sjui netflix sijui google UTASUBIRI SANA
Hii yako nzuri na imetulia ila sio mbaya na idea ya mdau pia maana ipo siku isiyo na jina Kuna mwanafamilia atajichanganya ata stream tu
 
Back
Top Bottom