Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,494
- 57,869
Appreciation Post kwa Marekani.
Kusema ukweli Watanganyika tunatawaliwa kwa nguvu na CCM.
Imefika wakati sasa maisha yetu yako mikononi mwa CCM na sio Mungu tena. Wanatuteka, Wanatuua, Wanatufungulia kesi za Uongo, Wanatushikiria kwenye Magereza na vituo vya polisi bila kuwepo na kesi dhidi yetu.
Kwa sasa Tanganyika Wananchi hatuko huru. Imefika hatua hata kama kuna huduma mbovu zinatolewa na Serikali huwezi kusema chochote maana utakapojaribu kutoa mawazo yako au kukosoa utatekwa na kupotezwa kama sio kufunguliwa kesi za uongo na kuozea gerezani.
Imefika hatua sasahivi thamani ya utu wa mwananchi haipo Tanganyika. Chaguzi zinaendeshwa kama kiini macho cha demokrasia. Wananchi hatuwezi kuwachagua Viongozi tunaowataka watuongoze na hatuwezi kuwawajibisha pale inapobidi wawajibishwe.
Imefika hatua wizi na ufisadi ni alama ya weredi hapa Tanganyika. Ukiwa mwizi na fisadi ndo unafisiwa, ndo unaabudiwa ndo unaonekana wewe ni mtu wa maana kwenye jamii. Hatuna Taasisi Tanganyika, hatuna uwajibikaji Tanganyika. Hakuna tena dhana ya kusimamia kwa uzalendo maslahi ya Wananchi kwa faida yao.
Tunaongozwa na wezi walioiba uchaguzi na wanaolazimisha kututawala kwa nguvu. Walio tayari kutuua na kutupoteza ili kulinda maslahi yao binafsi.
Uchawa ndo ajira yao rasmi. Badala wafanye jitihada kuwajaza vijana maarifa ili walete mabadiliko chanya kwa jamii wanawanyima vijana hizo fursa adhimu na wanawafanya kuwa machawa wao. Kuwalamba miguu na kuwasifia mitandao masaa 24.
Watanganyika tunapenda kuwashukuru sana Marekani kwa namna mnavyosimama kuwasema hawa kina Samia na CCM yao.
Tunajua kuwasema pekee haitoshi. Dunia ilipofika bila kuchukua hatua kama mnazochukua Venezuela itaenda kuwa sehemu mbaya sana ya kuishi na kwa maisha ya binadamu.
Tunaomba mfanye kama mlivyofanya kwa Makabulu wa Afrika Kusini hadi walipoona Dunia yote haipo upande wao na kuamua kuwaachia Wananchi wa Afrika kusini.
Tunaomba muwaweke Samia na Wakuu wake wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwenye orodha ya Watu hatari sio tu kwa Watanganyika na Marekani bali kwa Dunia nzima.
Tunaomba mkiweke CCM kuwa kama kikundi cha kigaidi kwa namna kinavyoendesha operesheni kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania kuwaua, kuwateka na kuwapoteza wananchi wanaokosoa Serikali yao dhalimu.
Tunaomba muilazimishe jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua kali sana dhidi ya Samia na genge lake ikiwemo kuvichukulia pia vyombo vya Ulinzi vya Tanganyika hasa TISS, JWTZ na Polisi kama vikundi vya kigaidi.
Mwisho tunaomba iwapendeze mfikirie kuchukua hatua mnazochukua Venezuela kwa Tanganyika ( Tanzania) ili kutukomboa sisi Watanganyika dhidi ya hawa Mashetani CCM na Serikali yao.
Mungu awabariki Marekani.
Mungu ibariki Tanganyika.