Tunawasaidiaje hawa Yatima?

Tunawasaidiaje hawa Yatima?

miss_mbeya

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2015
Posts
1,072
Reaction score
1,021
Habari wana Jamii forums, nilikuwa naomba mawazo yenu namna nitakavowqshauri hawa Vijana yatima. Ipo hivi kuna kijana ni wa mwisho kuzliwa kwao, wazazi wake walimuacha akiwa fomr one walifariki kwa HIV positive.

Familia hizi ni zile kila familia wanajijua wao yaani baba mkubwa na watoto hajali familia ya ba mdogo, kila familia wanapambana kivyao, sasa hawa walikuwa ni majirani zetu, huyo kijana alivyoachwa na wazazi, baba alimuacha darasa la sita na mama anakamuacha form one, sasa akawa anafanya vibarua ndiyo anasoma, kasoma shule ya kata bahat nzuri vijana hawa walikuwa bright darasani.

Dadake 1 alivoona maisha magumu alianza kujiuza, hivi huyu kijana wa kiume alipambana akapata two ,akapangiwa A-Level masomo ya arts, akapata two akomba duce ualimu kote huko alikuwa anafanya vibarua no one care about him, alivokuwa anaomba chuo nilimwambia ambatanishe death certificate, akapata mkopo 100% kwa kweli kijana ile hela aliliitimia vizuri akanunua mpka kiwanja kijijini kwa kujibana, alimaliza chuo 2015 mpaka leo anahangaika ajira ya ualimu.

Nawaza ni nani atakaemsaidia huyu kijana atoboe ukiangalia amekua kwa mazingira magumu bado ajira akiomba anatemwa yaani amekata tamaa, nilimpa laki 4 kama mtaji anapambana mdogomdogo.

Wanajamii Forums namsaidiaje huyu kijana? Naomba mawazo yenu
 
Wanajamii Forum namsaidiaje huyu kijana ?
Ulinipa 400,000 means ni pesa ya investment, Ila 4 means stability & predictability inamaanisha 4 stand for saving, deposits & for family budget, 4 doesn't promise great wealth

Sasa ushauri; mpe 500,000 alafu mwambie awekeze yaan afanye investment, 5 is associated with fortune & money, 5 suitable for investment & deposits, wazo la biashara auze hata maziwa fresh na mtindi atatoboa huku akisubiria Ajira au afungue hata saloon ya kunyoa sio vibaya ni wazo tu
 
Habari wana Jamii forum, nilikuwa naomba mawazo yenu namna nitakavowqshauri hawa Vijana yatima.Ipo hivi kuna kijana ni wa mwisho kuzliwa kwao ,wazazi wake walimuacha akiwa fomr one ,walifariki kwa hiv positive .Familia hizi ni zile
Ana umri gani Mkuu. Anafundisha masomo gani je unashindwa kumtaftia connection ? Unabidi kumpa njia za kupita ili asibaki na regrets
 
Ulinipa 400,000 means ni pesa ya investment, Ila 4 means stability & predictability inamaanisha 4 stand for saving, deposits & for family budget, 4 doesn't promise great wealth

Sasa ushauri; mpe 500,000 alafu mwambie awekeze yaan afanye investment, 5 is associated with fortune & money, 5 suitable for investment & deposits, wazo la biashara auze hata maziwa fresh na mtindi atatoboa huku akisubiria Ajira au afungue hata saloon ya kunyoa sio vibaya ni wazo tu
Ahsante mkuu kwa ushauri wako ,nilisahau kuelezea kuwa nilimpa kama mtaji akasema naenda kufanya biashara Mbeya mjini ,ya suruali za mtumba ,na anaendelea ila anasema biashara ngumu wakati mngine hauzi kabisa
 
Ana umri gani Mkuu
Anafundisha masomo gani je unashindwa kumtaftia connection ? Unabidi kumpa njia za kupita ili asibaki na regrets
Ni kijana aliezaliwa 1991,masomo ya arts ,connection nimeshindwa mkuu kama unaweza nisaidia please naomba msaidie
 
Ahsante mkuu kwa ushauri wako ,nilisahau kuelezea kuwa nilimpa kama mtaji akasema naenda kufanya biashara Mbeya mjini ,ya suruali za mtumba ,na anaendelea ila anasema biashara ngumu wakati mngine hauzi kabisa
Biashara inahitaji uvumilivu lakini pia mwambie ajiongeze km ana taaluma ya ualimu anaweza akaanzisha kitu kinachohusiana na taaluma yake km kutengeneza material za shule na kuziuza mkononi au kupitia whatsapp pia anaweza akaanzisha madarasa ya mtandao km WhatsApp kwa kuanzisha topics na kuwafundisha wanafunzi watamlipa kidogo kidogo na katika hao wapo watakao taka awafundishe physical (hii niliifanya nilipokua shinyanga huko Ilamata na maeneo ya Malampaka) kwa wanafunzi atapata pesa in a side hustle, kwan amesomea ualimu wa nini ?
 
Unatoa Taarifa nusu nusu ebu Mwambie huyo Jamaa ajiunge Jamii forum ili ajielezee vizuri
 
Back
Top Bottom