Tunawapenda sana wawekezaji wa Kitanzania kwa kuwa ni watanzania wenzetu , lakini kwa hiki kinachoendelea Serikali ikiangalie kwa jicho la 3

cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
2,072
1,697
Moja kwa moja niende kwenye mada, wawekezaji wa kitanzania ni ndugu zetu na hivyo hatunabudi kuwapenda na kuunga mkono jitihada zao

Ila chakusikitisha ni kwamba kumekuwa na malalamiko makubwa sana juu ya hawa wawekezaji wa kitanzania hasa kwenye makampuni, viwandani na kwenye miradi mikubwa

Malalamiko mengi hasa yanalenga kwenye maslahi ya wafanya kazi kwa ujumla mfano, kucheleweshwa kwa mishahara au wakati mwingine kudhurumiwa kabisa, kutokulipwa kwa malipo ya muda wa ziada yaan ( OT ) kunyanyaswa kwa wafanyakazi, wafanya kazi kutopewa mikataba hatimaye kupoteza haki zao za msingi kama Nssf nk

Kulipwa tarehe 50 kwa mwekezaji wa tanzania ni jambo la kawaida sana, wapo baadhi ya wafanyakazi wamewapeleka mabosi wao polisi, chakusikitisha hawajapata msaada wowote uko polisi

Matatizo haya hasa yapo kwenye miradi ya umeme , unakuta kampuni imepewa mradi wa bilioni za pesa lakini cha ajabu kampuni inawafanya kazi 10 na hata hao wafanya kazi wenyewe kuwalipa tu shida sasa mpaka unashangaa hivi hii ni kampuni au kitu gani?

Kampuni inashindwa kulipa wafanyakazi 10? sasa kama hata wafanyakazi 10 inashindwa kuwalipa iliwezaje kupata kazi ya bilioni za pesa?

Ni wakati sasa wa serikali kuangalia kwa jicho la tatu, kampuni nyingine ni za kitapeli sasa ni bora hizo kazi wapewe wageni tu huenda maslahi ya watanzania wenzetu yataboreka kuliko kuwapa wazawa.

Mheshimiwa January Makamba, vizara kayo ndio inaongoza kwa ubabaishaji kupitia miradi yako mikubwa ya umeme hivyo unapaswa kuwa makini sana juu ya kinachoendelea,

Watanzania wenzetu wanadhurumiwa sana haki zao kwenye ujenzi wa vituo vya kizalisha umeme yaan substation na line ,

Kama upo humu ndani pitia bandiko langu kisha lifanyie utafiti utagundua kuna madudu sana yanaendelea katika miradi yako
 
Tatizo mara nyingi linaanzia kwenye Tendering system. Mkandarasi anapunja mishahara/maslahi aliyo-quote ili kuongeza faida.
Ingekuwa vizuri wakaguzi wakawa wanapitia Tender documents na kisha kuwahoji wafanyakazi ili kuwawajibisha!
 
Back
Top Bottom