Tunawahitaji wanaharakati zaidi kuliko wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunawahitaji wanaharakati zaidi kuliko wanasiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Matteo, Oct 11, 2011.

 1. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Katika Tanzania yetu ya leo, ambayo kila Mwanasiasa jicho liko kwenye chaguzi, nafikiri tunahitaji wanaharakati zaidi ya tunavyo wahitaji wanasiasa. Mimi ninavyo jua walio wapinzani leo, kesho watakuwa watawala (nkimaanisha ipo siku nao watatawala0 na wakisha tawala kuna uwezekano mkubwa nao wakalewa mvinyo wa Uongozi na matatizo yetu ya kila siku yakabaki vilevile.

  Mimi ninachoona ni kwa wanasiasa karibu wote ni kutafuta popular support of making them reach their goals, na kwa walio wengi 'goal' huwa ni kinyakuwa madaraka na si kutatua matatizo ya waliowapelekea kunyakua hayo madaraka.

  Tukiwa kama great thinker nafikiri tunawahitaji wanaharakati zaidi, kwa sababu hakuna siku wanaharakati watachoka kuikosoa serikali iwe ya CCM, CHADEMA, CUF, UPDP, NCCCR, waendelea tu kuikosoa. Leo hii CHADEMA ikiingia madarakani kelele zote za kuikosoa Serikali zitakwisha, labda CCM wanaweza kuanzisha hizo kelele ila lengo lao litakua kurudi tena madarakani na si kumkwamua mwananchi masikini wa Tanzania.
   
 2. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Usichojua ni kwamba hata wanaharakati pia ni wanasiasa pia?
  Haya bwana nimekusoma..... Sasa sijui hao wanaharakati ndio watatuletea maendeleo kama tunadhani vyama vya siasa haviwezi?
  Endelea tukusikie labda kuna hoja kubwa zaidi....
   
 3. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2011
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kaa La Moto, mi huwa si mtaalamu sana wa siasa, ila kwa Uchunguzi wangu naona kama kuna aina mbili za siasa, Siasa za majukwaani na Siasa za utekelezaji sera. Na hizi aina huwa kwa hapa nyumbani zinatofautiana sana.. Nkimaanisha kuwa kile viongozi wanacho kihubiri majukwaani si kile kinacho tekelezwa. Na mara nyingi kama wanasiasa hawajakumbushwa kumbushwa, ili mradi maslai yao binafsi yako vizuri wanaweza wasitekeleze chochote kati ya vile walivyo ahidi. Sina uhakika ni wanaharakati gani amabao ni wanasiasa ila wanaharakati wengi ni kama whistle blower.. kuikumbusha Serikali na Wanasiasa kutekeleza ahadi zao...na kama umefualia wanaharakati waliokuwa wanasiasa basi siasa ziliwashinda na kurudia kazi zao za Harakati akiwemo Che Guavara na Wangari Maathai kwa uchache wao. Kama serikali na wanasiasa watapata watu wa kuwashtua kutekeleza ahadi zao basi maendeleo yatakuja.
   
Loading...